Asante 2022, nilipata mil. 4.5 kimasihara

Asante 2022, nilipata mil. 4.5 kimasihara

Aisee sasa nifanyeje na nilishaitumia na sijawahi pigiwa na mtu kwamba kakosea kutuma
Mimi sijui kwa sababu kwangu pia Sina uhakika Kama nilipata misukosuko kwa sababu ya ile hela au ikitokea tu.

FUATA MOYO WAKO
 
Munadanganyana sana mara sijui karma mara hivi,hebu niwaambie kitu kimoja acheni imani za kijinga mimi ukikosea muamala kuanzia laki 2 sikurudishii hata iweje nakumbuka kuna demu mmoja wa kichaga alikosea hela akatuma kwangu laki 5 aisee nilikodi bodaboda mpakka town kwenda kuipakua hela yangu ya bure yule dada alipiga simu sana ananiomba nimrudishie nikawa namuambia niko barabarani dada nikifika hom tu nakurudishia kumbe nipo barabarani kwenda kwa wakala na mpaka leo hakuna cha karma wala nini
Mmh
 
Duh pole mkuu ni fundisho hilo

Mimi leo yamenikuta lakini kwa aina nyingine

Iko hivi...

Kwenye biashara nnazo fanya natumia sana Instagram kutangaza na nalipia matangazo mara kwa mara,sasa kuna siku nimeweka hela Kwenye visa card yangu ili niweze kulipia tangazo

Nimeclick confirm payment,ikaonyesha malipo yamekamilika lakini hela haikukatwa kwenye account yangu lakini Instagram inaonesha tangazo limeshalipiwa,tangazo likaendelea kwahyo nikawa nimepata tangazo bure maana hela imebaki

Nilifurahi sana japokua haikuwa nia yangu kutowalipa ni wao wenyewe system zao zilijichanganya


Sasa leo nilitaka nilipie tangazo lingine nakutana na deni ile hela yao ya siku ile ambayo hawakuchukua ndo inabidi niilipe ili niweze kuendelea na matangazo mengine sina namna inabidi nilipe tu japokua inauma[emoji28]
Huwa wanakata pesa per engagement au per view mkuu.
 
Sawa umetapeli hela ya watu lakini acha kumshirikisha Mwenyezi MUNGU kwenye ujinga wako. 😮‍💨
 
Mkuu mbona makasiriko tena nimemtapeli nani na mbona hadi leo sijapigiwa simu kwamba mtu kakosea kutuma pesa, punguza wivu kidogo au una njaa nikutumie hata 10k
 
Awali nilidhani dunia ni sehemu ya kutendeana mema hadi pale nilipolipwa mabaya hadi na ndugu zangu na watu wa karibu.

Najilaumu ile 100k nilishindwaje kuichomoa hatimae ikarudi ilikotoka.

Mathalan hujamlazimisha mtu kukutumia hiyo hela, au hujaiba wala kupora hayo ndo malipo yako sasa. Utajuaje labda serikali au UN imekupa mafao yako ya kutokua na ajira?
 
Nikiwa nimepitia misukosuko mingi tangu Januari ya mwaka 2022 Nitaikumbuka zaidi siku ya Alhamis tar 29 majira ya saa saba za mchana, nikiwa nimekaa kijiweni na jamaa zangu huku nikiwa sina ramani ya kazi na sikuwa hata na uhakika wa mlo wa mchana kwa siku hiyo iliingia sms ya muamala kwenye simu yangu kuwa nimepokea kiasi cha ml 4.5 kutoka kwa wakala.

Hakika sikuamini nilichokiona, kwa haraka hiyo pesa nikaihamishia kwenye lain yangu ya tigo pesa ml 2 na laini ya voda nikahamishia ml 2, mbio hadi kwa wakala nikaitoa pesa kwenye lain zote na ile iliyokuwa imebaki kwenye namba niliyotumiwa ya airtel nayo nikaitoa.

Na laini iliyopokea muamala sijaiweka hewani hadi sasa na kabla sijaitoa hewani sikupigiwa na mtu kwamba ametuma hela kwangu kimakosa na wala mimi sikuwa na ahadi na mtu eti anitumie hela.

Kwahiyo ninashukuru sana aliyenitumia hiyo hela, kiukweli hata kama angenipigia na kuniambia eti kakosea muamala asingeambulia kitu. Mungu amlinde sana nilikuwa nina Magumu sana asante Mungu, na nitakukumbuka 2022.
Wee jamaa nirudishie pesa yangu.Naomba unirudishie hata nusu yake tu.
 
Awali nilidhani dunia ni sehemu ya kutendeana mema hadi pale nilipolipwa mabaya hadi na ndugu zangu na watu wa karibu.

Najilaumu ile 100k nilishindwaje kuichomoa hatimae ikarudi ilikotoka.

Mathalan hujamlazimisha mtu kukutumia hiyo hela, au hujaiba wala kupora hayo ndo malipo yako sasa. Utajuaje labda serikali au UN imekupa mafao yako ya kutokua na ajira?
😂😂😂
 
Back
Top Bottom