Asante 2022, nilipata mil. 4.5 kimasihara

Nipo na 45,000 hapa, ilituwa toka Equity Bank na sijui nani aliituma. Ipo tu sijaipatia matumizi.
 
Mkuu naona una laki tano kabisa imetulia kwenye account ,hujui namna ya kuitumia ....
 
Magumu umeshayamaliza? Na pesa imeshaisha na magumu bado yapo. Uaminifu hufungua Baraka zaidi.
Tusiendekeze sana njaa.
We mwaminifu una sh ngapi hadi sasa
 
Hayo mafomula wakati mwengine huwa hayana maana yoyote, ninachoogopa ni kudhulumu nafsi, au mtu mnayefahamiana, the spirit or her work well on attacking others endapo kama kuna uovu.
Yalishanikuta believe me.... Nilijiona mjanja kama wewe, ila nikajuta my return ilikuja...
 
Hiyo pesa sana sana ulinunua pamba na kunywea pombe na malaya,WAAFRIKA WANA LAANA YA MILELE
 
Nikiwa nimepitia misukosuko mingi tangu Januari ya mwaka 2022 Nitaikumbuka zaidi siku ya Alhamis tar 29 majira ya saa saba za mchana, nikiwa nimekaa kijiweni na jamaa zangu huku nikiwa sina ramani ya kazi na sikuwa hata na uhakika wa mlo wa mchana kwa siku hiyo iliingia sms ya muamala kwenye simu yangu kuwa nimepokea kiasi cha ml 4.5 kutoka kwa wakala.

Hakika sikuamini nilichokiona, kwa haraka hiyo pesa nikaihamishia kwenye lain yangu ya tigo pesa ml 2 na laini ya voda nikahamishia ml 2, mbio hadi kwa wakala nikaitoa pesa kwenye lain zote na ile iliyokuwa imebaki kwenye namba niliyotumiwa ya airtel nayo nikaitoa.

Na laini iliyopokea muamala sijaiweka hewani hadi sasa na kabla sijaitoa hewani sikupigiwa na mtu kwamba ametuma hela kwangu kimakosa na wala mimi sikuwa na ahadi na mtu eti anitumie hela.

Kwahiyo ninashukuru sana aliyenitumia hiyo hela, kiukweli hata kama angenipigia na kuniambia eti kakosea muamala asingeambulia kitu. Mungu amlinde sana nilikuwa nina Magumu sana asante Mungu, na nitakukumbuka 2022.
Asije mtu akakutisha ooh sijui utapata laana au sijui utailipa kwa njia gani ,,hakuna kitu kama hicho ,,pesa si haramu hata siku moja kwakua haija umbwa ,,fedha imetengenezwa ...
 
Kipindi nipo chuoo niliwahi kutumiwa pesa kimakosa laki 8 nikajifanya mjanja nikaitoa nikakusanya marafiki nikaenda nao kunywa pombe ile laini niliswitch off kwa wiki 3.ikapita miezi 8 kimya..baadae bibi alipata shida ya figo ilitakiwa afanyiwe dialysis kila mwezi so michango ya kifamilia ikatembea, bila kujua ili wala lile shangazi akanitumia mchango pesa ya matibabu laki 9.5 niitoe ili nimpatie mzee kumbe alituma katika ile line niliyotumiwa pesa kwa bahati mbaya..tigo hawajuchelewesha sms ikaingia hapo hapo
Ndugu mteja umekatwa sh laki 8 salio lako jipya ni laki na nusu niliishiwa pozi aisee.
Ili kuuawa soo nikaingia hasara nikatoa pesa yangu ya mkopo nikampatia mzee uku moyoni nina maumivu.
Juzi kati kuna mtu alikosea tena akanitumia pesa kimakosa mwenyewe nikamtafuta nikampigia cm nikamwambia umenitumia pesa kimakosa nakurudishia pesa yako..yaanini mie
Duh pole mkuu ni fundisho hilo

Mimi leo yamenikuta lakini kwa aina nyingine

Iko hivi...

Kwenye biashara nnazo fanya natumia sana Instagram kutangaza na nalipia matangazo mara kwa mara,sasa kuna siku nimeweka hela Kwenye visa card yangu ili niweze kulipia tangazo

Nimeclick confirm payment,ikaonyesha malipo yamekamilika lakini hela haikukatwa kwenye account yangu lakini Instagram inaonesha tangazo limeshalipiwa,tangazo likaendelea kwahyo nikawa nimepata tangazo bure maana hela imebaki

Nilifurahi sana japokua haikuwa nia yangu kutowalipa ni wao wenyewe system zao zilijichanganya

Sasa leo nilitaka nilipie tangazo lingine nakutana na deni ile hela yao ya siku ile ambayo hawakuchukua ndo inabidi niilipe ili niweze kuendelea na matangazo mengine sina namna inabidi nilipe tu japokua inauma[emoji28]
 
Niliwahi ingiziwa milioni , 4 NMB Kimakosa Wala sikujua imetoka wapi Ile pesa

Kwanza nilidhani ni utani nikaicheki Salio nikakuta IPO.

Nikawaza sana nikaoitee niitafune au vipi.

Nikaamua kuicha maana sio yangu na sijui alituma atakuwa katika wakati Ila nilijioa muda kwamba ikipita wiki nzima haijatolewa na wenyewe naitafuna itakuwa lost money.

Basi nikaamua kesho asubuhi kucheki Salio nikakuta haipo nikaishia kusonya tu[emoji1]

Anyway hio Hela mzee utailipa tu In one way or another direct or indirectly ila utaikunya tu just a matter of time

Muda utasema.
 
Kipindi nipo chuoo niliwahi kutumiwa pesa kimakosa laki 8 nikajifanya mjanja nikaitoa nikakusanya marafiki nikaenda nao kunywa pombe ile laini niliswitch off kwa wiki 3.ikapita miezi 8 kimya..baadae bibi alipata shida ya figo ilitakiwa afanyiwe dialysis kila mwezi so michango ya kifamilia ikatembea, bila kujua ili wala lile shangazi akanitumia mchango pesa ya matibabu laki 9.5 niitoe ili nimpatie mzee kumbe alituma katika ile line niliyotumiwa pesa kwa bahati mbaya..tigo hawajuchelewesha sms ikaingia hapo hapo
Ndugu mteja umekatwa sh laki 8 salio lako jipya ni laki na nusu niliishiwa pozi aisee.
Ili kuuawa soo nikaingia hasara nikatoa pesa yangu ya mkopo nikampatia mzee uku moyoni nina maumivu.
Juzi kati kuna mtu alikosea tena akanitumia pesa kimakosa mwenyewe nikamtafuta nikampigia cm nikamwambia umenitumia pesa kimakosa nakurudishia pesa yako..yaanini mie
Hahahah yaani jamaa anajisifu lazima aje ailipe hio kitu
 
Nikiwa nimepitia misukosuko mingi tangu Januari ya mwaka 2022 Nitaikumbuka zaidi siku ya Alhamis tar 29 majira ya saa saba za mchana, nikiwa nimekaa kijiweni na jamaa zangu huku nikiwa sina ramani ya kazi na sikuwa hata na uhakika wa mlo wa mchana kwa siku hiyo iliingia sms ya muamala kwenye simu yangu kuwa nimepokea kiasi cha ml 4.5 kutoka kwa wakala.

Hakika sikuamini nilichokiona, kwa haraka hiyo pesa nikaihamishia kwenye lain yangu ya tigo pesa ml 2 na laini ya voda nikahamishia ml 2, mbio hadi kwa wakala nikaitoa pesa kwenye lain zote na ile iliyokuwa imebaki kwenye namba niliyotumiwa ya airtel nayo nikaitoa.

Na laini iliyopokea muamala sijaiweka hewani hadi sasa na kabla sijaitoa hewani sikupigiwa na mtu kwamba ametuma hela kwangu kimakosa na wala mimi sikuwa na ahadi na mtu eti anitumie hela.

Kwahiyo ninashukuru sana aliyenitumia hiyo hela, kiukweli hata kama angenipigia na kuniambia eti kakosea muamala asingeambulia kitu. Mungu amlinde sana nilikuwa nina Magumu sana asante Mungu, na nitakukumbuka 2022.
Kabla ujafaa utailipa ndugy
Hizi hela kama ukimwi ukienda kavu mawili upone utoke nao....
Nikopaolee kwa mangiiiiii nambegee...utanijulishaa
 
Back
Top Bottom