ASANTE SAMIA 2022.
Kwa kipindi cha miaka miwili ya Uongozi wa Rais Samia Suluhu ikiwa hii ni term yake ya pili, nichukue fursa hii kumpongeza kwa haya aliyoyakamilisha ndani ya Mwaka huu wa 2022. Ni wazi ana Maono makubwa katika kutuletea maendeleo ndani ya nchi yetu tuendelee kumuunga mkono kwa dhati.
tuna kila sababu ya kumpongeza na kujivunia.
Kwa Mwaka 2022 Tumeyashuhudia haya.
-• Daraja la Wami limekamilika
-• Mradi wa Bwawa la Mwalimu Nyerere asilimia 78.
-• Matibabu ya Fistula kupatika nchi nzima.
-• Neema Kwa Walimu Rais Samia amelipa Tsh Bil 117.6/- za malimbikizo ya mishahara na madeni mengine ya Walimu 88,297.
lengo ni kuboresha maslahi ya Walimu.
-• Amejenga nyumba 800 za Walimu na kupandisha mishahara na madaraja ya walimu.
-• Mwaka 2022 Rais Samia Suluhu amefanya mapinduzi makubwa sekta ya afya sasa Hospitali zote za Rufaa za Mikoa zimepelekewa mashine za CT Scan ili kutoa huduma ya uchunguzi kwa wananchi.
-• Kukamilisha mradi wa maji Same-Mwanga- Korogwe baada ya kukwama kwa zaidi ya miaka 10.
-• Mpango wa Kuwawezesha Wamachinga Kupata Mikopo na Ujenzi wa Masoko.
-• Kuthibiti Mfumuko wa Bei kwa asilimia 4.8 kuwa chini ya asilimia 5.
-• Mpango wa Mama kusambaza Gesi asilia majumbani.
-• Elimu Bure hadi kidato cha Sita
-• Kuondoa Vikwazo vya Kikodi na Visivyo vya kikodi, kuboresha miundombinu na Mahusiano kati ya Tanzania na Congo, DRC
-• Kufanikisha soko la Korosho kuuzwa Marekani baaada ya kushindwa kufanya hivyo zaidi ya miaka 30.
-• Kuufungua Mkoa wa kigoma kwa Ujenzi wa Barabara za Lami na mikoa inayoiunganika na Mkoa wa Kigoma.
Ukarabati wa Meli ya abiria 600 yenye uwezo wa kubeba tani 400. Ukarabati wa Meli ya kubeba mafuta MV Sangara. Ujenzi wa Meli ya kubeba Mizigo tani 3000 kwenda DRC na Zambia. Ukarabati wa Meli ya kubeba abiria Mv Liemba.
-• Ujenzi wa Reli ya Kisasa SGR kutoka Tabora hadi Kigoma.
-• Ujenzi wa Reli ya Kisasa kwenda Burundi na DRC.
-• Ujenzi wa Bandari za Kibirizi, Katoshi, na Ujiji.
-• Upanuzi na ukarabati wa Uwanja wa ndege Kigoma.
-• Ufadhili wa Wanafunzi waliofaulu vizuri masomo yao kidato cha Sita (Samia Scholarship).
- Rais Samia Amefuta maadui watatu (Ujinga, Maradhi na Umaskini) kwa kujenga Vituo vya Afya, Madarasa nchi nzima na kujenga Uchumi.
-• Ujenzi wa Vyuo vya Ufundi Stadi (VETA) kila Wilaya.
-• Rais Samia ametoa ruzuku ya viuatilifu vya mazao ya korosho kutoka bilioni 59 hadi bilioni 90 Mwaka 2022.
-• Rais Samia ameidhinisha bilioni 160 kwa ajili ya Ujenzi wa madarasa 8000 nchi nzima.
-• Upelelezi kutokuzidi siku 90
-• Kuboresha Mahusiano ya Kidpomasia na kibiashara Kati ya Tanzania na Kenya.
-• Jumla ya Miradi 256 ilisajiliwa yenye thamani ya shilingi bilioni 8.7 na kuzalisha zaidi ya ajira 53,200 mwaka 2021
-• Ruzuku ya Bilioni 100 kila Mwezi kupambana na mfumuko wa bei ya mafuta.
-• Mauzo ya Tumbaku kati ya Tanzania na Japan yameongezeka kutoka tani 14000 hadi tani 30,000.
-• Kuleta usawa wa kijinsi katika kufanya maamuzi, kumiliki mali na rasilimali.
-• Jumla ya Watanzania milion 5.9 waliokidhi vigezo walinufaika na shilingi bilioni 903 zilizotolewa na Serikali kama mkopo nafuu kwa Vijana, Wanawake, Walemavu na Wazee.
-• Jumla ya kampuni 2,019 za kitanzania ziliingia mikataba ya kutoa huduma kwenye miradi mbalimbali nchini.
-• Ongezeko la asilimia 234 ya mizigo katika bandari ya Mtwara.
-• Kufunguka kwa fursa ya kibiashara kati ya Tanzania na Msumbiji.
-• Ukuaji wa miamala ya kifedha hadi Tzs trilioni 11.6
-• Ongezeko la shehena ya mizigo kwa asilimia 49.9 kwenda DRC
-• Umeme wa Uhakika ndani ya Mkoa wa Kigoma.
-• Kuondoa Ada za mitihani katika shule zote za Umma
-• Ugawaji wa Vishikwambi kwa Walimu wote nchi nzima hii itasaidia Walimu kuwa na uwezo wa kufundisha kupitia vitabu vya mtandaoni.
-• Usafirishaji wa Nyama nje ya nchi umekuwa kwa asilimia 57.
-• Serikali kujenga Kampasi za vyuo vikuu katika mikoa 14 nchini.
-• Mauzo ya thamani ya Karafuu yamepanda kutoka bilion 3.5 Mwaka 2020 hadi bilioni 145 Tzs.
-• Ununuzi wa mabasi mapya 177 ya Mwendokasi kutoka kuhudumia abiria 200,000 kwa siku hadi abiria 500,000.
-• Kurekebisha mifumo ya Kodi na Tozo katika kutatua Changamoto za Biashara kwa Vijana na Wanawake.
-• Kupungua Lawama kwa mhimili wa Mahakama, Serikali imetaka mtu akamatwe na kuswekwa rumande Upelelezi na ushahidi uwe ni wa kutosha.
-• Serikali imetoa bilioni 150 kwa ajili ya Mbolea ya Ruzuku
-• Akiba ya chakula Tanzania imeimarika maradufu chini ya Rais Samia.
-• Kukamilika kwa Mradi wa Kimkakati wa Umeme wa Rusumo unaozalisha megawatt 80
-• Mchakato wa mradi wa Kufua Umeme Wa Rumakali na Ruhiji Mradi huu ilikwama kwa zaidi ya miaka 24 utekelezaji wake utagharimu Trilioni 1.4 Tzs.
-• Kuwasili kwa mabehewa 20 ya Reli ya kati (MGR)
-• Bilioni 174.9 kuboresha uzalishaji wa mbegu na mbolea kutoka AFDB.
-• Mambo Manne ambayo Rais Samia ameyafanikisha kwenye mkutano wa 42 wa SADC 1. Kiswahili kuwa Lugha rasmi. 2. Mafanikio ya usawa wa kijinsia 3. Uwekezaji kwenye Uchumi wa buluu. 4. Usalama wa chakula.
-• Kufunga Mtandao wa Intaneti juu ya kilele cha Mlima Kilimanjaro.
-• Air Tanzania kuongeza safari zake Nigeria, Ghana na DRC
-• Utoaji wa huduma ya Afya umekua kutoka asilimia 4.8 hadi asilimia 5.1
-• Mradi wa Ujenzi wa nyumba nafuu zaidi ya 500 Samia Housing Scheme.
-• Uchumi wa Tanzania umekuwa kwa asilimia 5.4
-• Mfumo mmoja wa Forodha kati ya Tanzania na Zambia eneo la Nakonde.
-• Ongezeko la Mapato ya Bandari ya Mtwara kukua kwa asilimia 64.
-• Kupata Fursa za masoko ya mbogamboga Ulaya kupitia Fit for Market Place.
-• Ujenzi wa Maabara za TBS kanda 7 nchi nzima.
-• Kukuza Uhuru wa Vyombo vya Habari.
-• Ongezeko la Mizigo katika viwanja vya ndege kwa asilimia 20%
-• Ongezeko la Watalii nchini maradufu
-• Ongezeko la Mauzo ya Tanzania katika soko la Afrika mashariki kwa asilimia 42.9
-• Kutangazwa kwa Mkoa wa Arusha na Zanzibar kuwa sehemu za vivutio bora Duniani kwa Mwaka 2022.
-•Kurejesha Mafao ya waliondolewa kazini kwa vyeti feki.
- Kufungua fursa ya Masoko kwa bidhaa za Tanzania kwenda China kuingizwa bila kulipiwa ushuru.
Karibu 2023.