Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 28,722
- 20,610
Kwanza pole kwa kazi mh Rais wetu na Asante kwa Hotuba yako ya kutuhamasisha ili tujiandae kuhesabiwa, mh Rais napenda kukuambia kuwa watanzania huku mitaani wamehamasika vizuri na wameelewa umuhimu wa sensa na wapo tayari kuhesabiwa
Mh Rais napenda kukufahamisha pia kuwa zoezi Hilo limepokelewa na watu wote kwa mikono miwili bila kujali itikadi ya vyama vya siasa, kwani sisi kwa sisi tunahamasishana kuwepo nyumbani au kuacha mtu atakayekuwa na uelewa na taarifa zote zinazohitajika, kwa kuwa pia tumeshayaona maswali husika kupitia mitandao, kwa hiyo ushirikiano utakuwa mkubwa utakao tolewa na kupewa makarani wa sensa.
Asante kwa kujenga umoja wa kitaifa ulio Rahisisha watu kuwa na hamasa maana sote Ni wamoja na wote tunaona zoezi hili Ni letu sote kwa manufaa yetu wote kwa pamoja katika kupanga mipango ya maendeleo kwa Taifa letu.
Mwisho ni ushauri wangu kwako mh Rais kutoa maagizo kwa waratibu wa zoezi hili ngazi za mikoa wahakikishe makarani wote wanapatiwa vifaa vyote muhimu katika kufanikisha zoezi hili, pia kutomfumbia macho atakayeleta dosari katika zoezi hili nyeti na muhimu kwa mstakabari wa Taifa letu, Asante.