Uchaguzi 2020 Asante sana Rais Magufuli, kiukweli ninashukuru

Uchaguzi 2020 Asante sana Rais Magufuli, kiukweli ninashukuru

TumainiEl

JF-Expert Member
Joined
Jan 13, 2010
Posts
6,782
Reaction score
12,716
Ninapenda tumia muda huu kukushukuru Mzee wangu Rais wa Jamuhuri ya Muungano ya watu watanzania kwa safari ndefu ya miaka mitano kutuongoza wa Tanzania hasa ktk kipindi kigumu chakubadilisha fikra za watanzania nakutufanya kufanya kazi kwa bidii na kutopenda kuwa omba omba. Hii haikuwa Rahisi na kamwe haitokuwa rahisi kwa awaye yote.

Mengi yametokea mengi yamesemwa ila ukweli utabakai kuwa ukweli wewe ni aina ya kiongoz umesimamia kwa mkono wa chuma yale kama kiongoz una yaamini na uwenda sisi kama taifa kuna nyakati tumekuchukia na kusema huyu nikiongoz asie na huruma kwa watu wengine au kusema hata wewe sio baba mwenye huruma ila siri na ukweli ya kile umekisimamia itabaki kuwa kwako na vyombo vya ulinzi na usalama.

Palipo na ukweli tuseme ukweli hili taifa lilikuwa ktk mahali palimuhitaji Rais kama wewe na nikweli chamoto tumekiona ila pamoja na yote umetufungua macho wengi na sasa tuna elewa maana ya vijana kuwa wabunifu na kuchapa kazi.

Rushwa ni adui wa haki na kwa hakika kwa maneno mafupi sana waliokula rushwa cha moto wamekiona na uwenda watasimulia vizazi vyao yale yamewakuta kwa kupenda Rushwa.

Uzembe na ulevi wa madaraka ulifanya Raia waka ktk msongo wa mawazo wasijuwe nani wakuwasaidia leo adabu nikama zote na Raia ndio mfalme afikapo ktk ofisi ya serikali.

Mafisadi wa ardhi walitesa Raia masikini na kufanya masikini kukosa mahali pakupeleka malalamiko ofisi za ardhi zilijaa rushwa na mafisadi walizitumia ofisi za ardhi kujinufaisha kwa ardhi isio kuwa yako ila umesimama pitia Waziri Lukuvi na ardhi pamekuwa mahali pakuheshimika. Binafsi nishuhuda wa haya na mara kadha pale ikulu tukija kama raia wakawaida tulipata huduma bora sana.

Kwa miaka mitano umeme umekuwa vizuri sana kiukwel kama sio wewe kusimamia kodi zetu na ruzuku unawapa tanesco umeme ungekuwa janga na bill kupanda bila sababu. Leo umeme ni historia kukatika na walanguz wa magenerator wamekuwa wanyonge.

Umeme wa Rea vijijini umesaidia sana kutanuwa upatikanaji wa umeme vijijini na sasa vijiji vingi vina umeme yule kijana alikuwa anamiliki smart phone mjin pia sasa anamiliki kijijini. Hakuna tofauti ya kijijini na mjini.

Umefanya mambo mazuri mengi ila usisahau kutengeneza akina Magufuli wengi. Marekani ina marais zaid ya arobain na tati laikin wanao kumbukwa hawazidi watano hivyo sio bure na wewe ukaingia ktk historia za taifa hili kwa kuwa Rais ulie thubutu na ukafanikiwa.
 
Hata Mwl hafikii kasi ya Dr Magufuli

Nasikiliza Hotuba ya Rais wangu

Hii ni hotuba bora zaid ya Rais wangu, facts tupu, Allah ampe Rais wetu Afya njema

Hotuba hii ni Hotuba bora zaid kuwahi kutolewa, nafananisha na hotuba Ya Rais Kikwete ya Bunge la Katiba na ile aliyoitoa kwny Msiba wa Mandela

Kumshindanisha Rais Magufuli na Walevi kwny Uchaguzi Mkuu ujao ni kumvunjia Heshma kwa kweli!
Magufuli ndie rais alieitendea haki Tanzania baada ya mwalimu
 
Nina penda tumia muda huu kukushukuru Mzee wangu Rais wa Jamuhuri ya Muungano ya watu watanzania kwa safari ndefu ya miaka mitano kutuongoza wa Tanzania hasa ktk kipindi kigumu chakubadilisha fikra za watanzania nakutufanya kufanya kazi kwa bidii na kutopenda kuwa omba omba. Hii haikuwa Rahisi na kamwe haitokuwa rahisi kwa awaye yote.
...
Umefanya mambo mazuri mengi ila usisahau kutengeneza akina Magufuli wengi. Marekani ina marais zaid ya arobain na tati laikin wanao kumbukwa hawazidi watano hivyo sio bure na wewe ukaingia ktk historia za taifa hili kwa kuwa Rais ulie thubutu na ukafanikiwa.

Ni mtu wa aina pekee kwani amejaliwa vipaji vingi sana. Leo ananishangaza kuhutubia Bunge, hotuba iliyosheheni takwimu, kwa kutumia kifaa maalamu cha kusomea, ambacho kinahitaji utaalamu na uzoefu kukitumia, kama alivyofanya yeye akaonekana anayoyasema yanatoka kichwani.
 
Yani ukisikia watu vuguvugu ambao si moto si baridi ni wewe TumainiEl huwa hueleweki umesimamia nini.
Mimi nilijua ni yale machizi ya matanga, kumbe ni kiumbe huyo ambaye yeye ni timamu lakini njaa ndiyo inamtesa na kumtoa ufahamu. Kamwe mtu kama yeye hawezi hongerea 1.5 tr
 
Kumshindanisha Rais Magufuli na Walevi kwny Uchaguzi Mkuu ujao ni kumvunjia Heshma kwa kweli!

Haya maneno,yanafikirika lkn.......
 
Utawala wa Rais John Pombe Magufuli umetufundisha umuhimu wa freedom of expression and human rights kwa vitendo.
Sky Eclat
Naomba nikuuliza..

Ni nini makusudio ya neno Uhuru(Freedom Of Expr....)?!!!
 
Utawala wa Rais John Pombe Magufuli umetufundisha umuhimu wa freedom of expression and human rights kwa vitendo.
Sky Eclat
Naomba nikuuliza..

Ni nini makusudio ya neno Uhuru(Freedom Of Expr....)?!!!
 
Ni mtu wa aina pekee kwani amejaliwa vipaji vingi sana. Leo ananishangaza kuhutubia Bunge bila kusoma na kwa takwimu.
Mkuu, sio kwamba kipo kifaa Mbele yake ambacho Pengine Sisi hatukioni tu,

Maana Kwa kumtizama, ni kama hasomi popote kweli, lakini, itakuweje ameze hotuba yooote hiyo yenye vipengele viiingi namna hiyo
 
Hata Mwl hafikii kasi ya Dr Magufuli

Nasikiliza Hotuba ya Rais wangu

Hii ni hotuba bora zaid ya Rais wangu, facts tupu, Allah ampe Rais wetu Afya njema

Hotuba hii ni Hotuba bora zaid kuwahi kutolewa, nafananisha na hotuba Ya Rais Kikwete ya Bunge la Katiba na ile aliyoitoa kwny Msiba wa Mandela

Kumshindanisha Rais Magufuli na Walevi kwny Uchaguzi Mkuu ujao ni kumvunjia Heshma kwa kweli!
Unit aliyoitengeneza Mwalimu huwezi kulinganisha na any material things hapa Tanzania.
 
Mkuu, sio kwamba kipo kifaa Mbele yake ambacho Pengine Sisi hatukioni tu,

Maana Kwa kumtizama, ni kama hasomi popote kweli, lakini, itakuweje ameze hotuba yooote hiyo yenye vipengele viiingi namna hiyo
Nami namtizama kwa umakini kama kuna kitu mbele yake anasoma. Yawezekana kifaa kama screen mbele yake kinamwezesha na nadhani ni cha kisasa sana kwa maana ya kubadili kurasa.
 
Rais wangu ananikosha sana......

hasa alipozima hayo ma genereta ya AGGREKO,SYMBION POWER na mengine...akasave hizo pesa.

BRAVO....
 
Back
Top Bottom