Uchaguzi 2020 Asante sana Rais Magufuli, kiukweli ninashukuru

Uchaguzi 2020 Asante sana Rais Magufuli, kiukweli ninashukuru

Utawala wa Rais John Pombe Magufuli umetufundisha umuhimu wa freedom of expression and human rights kwa vitendo.
Yaah! Tunaji-express tu humu bila shida yeyote.
Hakuna anayetuzuia kusemma chochote.
 
Ninapenda tumia muda huu kukushukuru Mzee wangu Rais wa Jamuhuri ya Muungano ya watu watanzania kwa safari ndefu ya miaka mitano kutuongoza wa Tanzania hasa ktk kipindi kigumu chakubadilisha fikra za watanzania nakutufanya kufanya kazi kwa bidii na kutopenda kuwa omba omba. Hii haikuwa Rahisi na kamwe haitokuwa rahisi kwa awaye yote.

Mengi yametokea mengi yamesemwa ila ukweli utabakai kuwa ukweli wewe ni aina ya kiongoz umesimamia kwa mkono wa chuma yale kama kiongoz una yaamini na uwenda sisi kama taifa kuna nyakati tumekuchukia na kusema huyu nikiongoz asie na huruma kwa watu wengine au kusema hata wewe sio baba mwenye huruma ila siri na ukweli ya kile umekisimamia itabaki kuwa kwako na vyombo vya ulinzi na usalama.

Palipo na ukweli tuseme ukweli hili taifa lilikuwa ktk mahali palimuhitaji Rais kama wewe na nikweli chamoto tumekiona ila pamoja na yote umetufungua macho wengi na sasa tuna elewa maana ya vijana kuwa wabunifu na kuchapa kazi.

Rushwa ni adui wa haki na kwa hakika kwa maneno mafupi sana waliokula rushwa cha moto wamekiona na uwenda watasimulia vizazi vyao yale yamewakuta kwa kupenda Rushwa.

Uzembe na ulevi wa madaraka ulifanya Raia waka ktk msongo wa mawazo wasijuwe nani wakuwasaidia leo adabu nikama zote na Raia ndio mfalme afikapo ktk ofisi ya serikali.

Mafisadi wa ardhi walitesa Raia masikini na kufanya masikini kukosa mahali pakupeleka malalamiko ofisi za ardhi zilijaa rushwa na mafisadi walizitumia ofisi za ardhi kujinufaisha kwa ardhi isio kuwa yako ila umesimama pitia Waziri Lukuvi na ardhi pamekuwa mahali pakuheshimika. Binafsi nishuhuda wa haya na mara kadha pale ikulu tukija kama raia wakawaida tulipata huduma bora sana.

Kwa miaka mitano umeme umekuwa vizuri sana kiukwel kama sio wewe kusimamia kodi zetu na ruzuku unawapa tanesco umeme ungekuwa janga na bill kupanda bila sababu. Leo umeme ni historia kukatika na walanguz wa magenerator wamekuwa wanyonge.

Umeme wa Rea vijijini umesaidia sana kutanuwa upatikanaji wa umeme vijijini na sasa vijiji vingi vina umeme yule kijana alikuwa anamiliki smart phone mjin pia sasa anamiliki kijijini. Hakuna tofauti ya kijijini na mjini.

Umefanya mambo mazuri mengi ila usisahau kutengeneza akina Magufuli wengi. Marekani ina marais zaid ya arobain na tati laikin wanao kumbukwa hawazidi watano hivyo sio bure na wewe ukaingia ktk historia za taifa hili kwa kuwa Rais ulie thubutu na ukafanikiwa.
Magazeti na propaganda zinakuchanganya ndugu.
Rushwa bado ipo.
Ajira tatizo limeongezeka
Umeme bado changamoto.
OMBA OMBA ndio kabisaa au na wewe ni miongoni mwa wasiofatilia ambao huwa mnatuambia "Mfugale imejengwa kwa fedha za ndani"?Ilhali tukipita pale tunaona bango kuwa Japan nae kachangia.
Mradi kama wa REA kafanya usimamizi tu...huu ni mradi una nguvu kubwa ya wafadhili.
Nadhani tungempima kwa mambo haya:-
Ukuaji wa uchumi.
Hali ya maisha ya watanzania(Welfare);makazi,chakula,huduma za afya,ongezeko la kipato n.k
*Katika ongezeko la kipato je watu wanaokuzunguka unaonaje katika miaka hii inayoelekea kutimia mitano,kipato chao kimeongezeka au "alie nacho ataongezewa na mwenye kidogo atanyang'anywa?
VIWANDA:Ikiwa ni dira yake kuu je kuna sera(policy) imeanzishwa na kutekelezeka na tukapata viwanda, na ni vingapi?Nitajie viwanda vitatu vya uwezo wa kati au mkubwa vilivyoanzishwa(hata vya wanyama na mazao yake sababu alisema tuna mifugo mingi ngozi na pembe ziongezewe thamani kabla ya ku export).
FDI ngapi zimekuja nchini mkuu,mwekezaji gani "mzito" amekuja huku kuwekeza Boss, sana sana hata Dangote alitoa kilio cha kutamani kuondoka🙄.
Au ndio yale ya mkazi wa mavanga, tinde ndanindani,nyamwaga(tarime),longido ndani ndani,Kiteto nae ashangilie mwendokasi,flyover e.t.c huku maisha yake yakiwa chini na hayana tumaini.Naam anatakiwa afurahie kama nchi lakini vipi kuhusu eneo lake?
 
Back
Top Bottom