Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,857
- 121,995
Wanabodi,
Hii ni Nipashe ya wiki iliyopita
Wanabodi,
Hili ni bandiko la Pongezi kwa Rais wetu, Mama Samia.
Kama mtu uliwahi kuandika kuhusu jambo fulani, halafu hilo jambo likafanyika, kwa jinsi ile ile ulivyoandika na ulivyoshauri, hata kama halikufanyika kwasababu ya andiko lako au ushauri wako, lakini limefanyika, hauna budi kupongeza.
Kwa jambo lenyewe anzia hapa, Asante sana Rais Samia kwa kuliponya Taifa. Umeonesha kwa kauli na matendo; tunajenga nyumba moja, hakuna sababu ya kugombea fito!
Kisha nenda hapa Kumbe DPP kutenda haki kunawezekana! Hongera sana, kazi umeianza vizuri. Sasa haki sio tu inatendeka, inaonekana! Kazi Iendelee…
Kisha hapa, Ushauri kwa DPP: Kutekeleza nia njema ya Rais Samia, kuona Haki ikitendeka; je, tumchagize DPP kutumia Nolle kufuta kesi zote zinazosuasua?
Kisha hapa Watanzania tumshukuru Mungu kupata mtu mwenye moyo wa kusamehe. Je, tumuombe asamehe tu bila kuombwa msamaha au akomae naye?
Hatimaye kesi ya Mbowe imefutwa!.
Kuna msemo wa Kiswahili usemao, "Ukiaminiwa, Jiaminishe", Tanzania ni nchi ya wote, Watanzania wote, binadamu wote ni sawa, CCM na Wapinzani wote ni sawa, na wote tuna lengo moja la kuijenga Tanzania yetu ambayo ni moja hivyo tunajenga nchi moja, tunajenga nyumba moja hatuna sababu ya kugombea fito.
Serikali ya awamu ya 5, ina mazuri yake, na ina mabaya yake kwasababu haikuwa serikali ya kimalaika, likuwa inaongozwa na binaadamu hivyo inawezekana kuna mahali ilikosea hivyo ikafanya makosa. Kuna watu walipotea katika mazingira ya utatanishi, hivyo kuhisiwa ni walipotezwa!. Kuna watu waliumizwa, wengine kwa kumiminiwa pyu pyu za kutosha na watu wasiojulikana na kuhisiwa hawa wasiojulikana sio wasiojulikana bali ni 'wasiojulikana'!.
Kwenye uendeshaji wa siasa zetu, kulikuwepo mgawanyiko wa makundi ya wenye nchi, watoto wa nyumbani CCM, na watoto wa kambo, wapinzani!.
Watoto wa nyumbani, wao walijisikia wako nyumbani kwao, wana rukhsa ya kufanya chochote, kila kitu, ikiwemo mikutano ya hadhara na kwenda popote, wakati watoto wa kambo, wao walizuiliwa, hata kufanya, mikutano hata kufanya mikutano ya ndani!, ilihali mikutano ni kitu kilichoruhusiwa na katiba.
Wengi wa viongozi wa wapinzani ilikuwa ni kila uchao, kukamatwa na wengi waliozea magerezani.
Tulipoalikwa Ikulu, kuuzungumzia mwaka mmoja wa Awamu ya 5, mimi ni miongoni mwa tuliobahatika kupata fursa ya kuuliza maswali, mimi swali langu lilikuwa moja tuu, "Rais wa JMT anachaguliwa kwa mujibu wa katiba na anaapa kuilinda, kuitetea na kuitelekeza katiba ya JMT, hivyo jambo ambalo limeruhusiwa na katiba, Rais wa JMT, anapata wapi mamlaka ya kulizuia?. Sikumbuki nilijibiwaje...., ila kwa awamu ile, CCM na wapinzani walikuwa ni kama paka na panya.
Baada ya kutokea kilichotokea, tukapata mabadiliko na Mama Samia kuingia, siku ile analihutubia Bunge la JMT, Rais Mama Samia kwa kauli na matendo, ameonyesha nia na dhamira safi ya kuliponya taifa kwa madhila tuliyopitia, na kuwaunganisha Watanzania tuwe wamoja tena.
Akatamka yuko tayari kukutana na wapinzani kwa kusisitiza, tunajenga nyumba moja, kwanini tugombee fito?.
Siku ya siku ya kukutana na wapinzani ikawadia, Msajili wa Vyama akavikalisha vyama vyote vya siasa pamoja pale Dodoma. Chama Kikuu cha Upinzani kwa huku Tanzania Bara, Chadema wakasusia mkutano ule kwa hoja ya hawata hudhuria kwasababu Mwenyekiti wao wa Chadema, Freeman Mbowe yuko mahabusu.
Sisi washauri wa bure tulishauri, badala ya kususa na kuzungumzia pembeni, kwa vile Rais Samia ameishaonyesha nia njema, mkutano huo ni fursa nzuri kwa Chadema kuwasilisha hoja zao mezani kwa rais. Chadema, P'se, Msisusie Mkutano wa Vyama, Wasilisheni Hoja Zenu Mezani, Zitamfikia Samia, Ana Nia Njema na Nchi Hii, Mpeni Ushirikiano!.
Chadema wa huku nyumbani, hawakuiona fursa hiyo hivyo hawakuitumia.
Kiongozi Mkuu wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe akaitumia fursa hiyo kikamilifu ikiwemo kumzungumzia Mbowe, na rais Samia akajibu pale pale, "Kusameheana kupo". Hiyo kauli ya "Kusameheana Kupo", tukaiandikia makala Watanzania tumshukuru Mungu kupata mtu mwenye moyo wa kusamehe. Je, tumuombe asamehe tu bila kuombwa msamaha au akomae naye?
Kitendo cha Chadema kuendelea kususa hata baada ya kuiona nia Njema ya Rais Samia, ni uthibitisho wa kutojiamini na kutoaminiana, kitendo cha Chadema ya nyumbani Tanzania kususia mkutano wa vyama na Rais Samia, huku ni kuonyesha Chadema ya nyumbani Tanzania, haina imani na nia njema ya kweli ya Rais Samia kuliponya taifa, hivyo kususa kule, was a missed opportunity!
Kwa jinsi Mungu alivyo mkubwa, ikatokea fursa ya Rais Samia akafanya ziara ya Ubelgiji, M/Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu, akaichangamkia fursa hiyo, akaomba kuonana na Rais Samia. Na Samia alivyo ni mtu wa hiyana, akakubali kuonana na Lissu bila Guyana na kufanya nae mazungumzo ya faragha.
Kitendo tuu cha Rais Samia kukubali kukutana na Tundu Lissu, ni uthibitisho wa ile nia njema ya dhati ya kuliponya taifa kwa kufuata ile filosofia ya Rais Samia ni rais Watanzania wote, ni rais wa wana CCM, ni rais wa wapinzani ni rais wa Watanzania wote hata wasio na vyama, lengo la kila Mtanzania ni kuijenga Tanzania yetu, hivyo CCM na wapinzani, tunajenga nyumba moja, hatuna sababu yoyote ya kuendelea kugombea fito!.
Kwa vile ni mazungumzo ya faragha, Taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu chini ya Mkurugenzi mpya, Zuhura Yunus (hongera), ikaeleza kuhusu mkutano huo wa Rais Samia na Tundu Lissu bila kueleza kilicho zungumzwa.
Rais wa JMT, ndiye raia number moja wa JMT na ndie Mkuu kuliko mtu mwingine yeyote ndani ya JMT, kimamlaka na kimadaraka. Sasa inapotokea mtu yeyote umeomba kumuona rais na kuongea nae jambo lako lolote na rais akakukubalia kumuona na kuongea nae, ile tuu kuongea na rais ni heshima kubwa, ina maana umeaminiwa.
Hivyo Tundu Lissu kukubaliwa kukutana na rais Samia, ni Lissu ameaminiwa. "Ukiaminiwa, jiaminishe". Baada ya mazungumzo, of course, lazima kuna hoja na maombi aliwasilisha kwa rais Samia.
Kwa vile Lissu ni mtu mdogo compared to Samia, na amekutana na mtu mkubwa, rais wa JMT, baada ya kikao, ukiona mkubwa amenyamaza, na wewe mdogo nyamaza!. Hapa natoa somo kwa wanasiasa wetu, tujifunze kunyamaza!. Somo hili la kujifunza kunyamaza nilianza kulitoa siku nyingi!. Mara baada ya uchaguzi Mkuu wa 2015, mgombea wa Chadema, Edward Lowassa kulalamika kuwa ni yeye alishinda kwa kura nyingi lakini kura zake akapewa mpinzani wake, nilimshauri anyamaze Elections 2015 - Kama Hii ni Kweli, Then, Serikali Yetu ni Serikali Dhalimu?, Haramu?. Hukumu ya Karma ii Juu Yake!
Moja ya mapungufu makubwa ya upinzani wa Tanzania, ni kupayuka payuka sana, kuropoka ropoka na kupiga sana kelele kuhusu karibu kila kitu!.
Kuna mambo ya kupigia kelele na kelele zikasaidia, lakini kuna mambo ya kufanywa kimya kimya, sio kila kitu ni kupayuka, kuropoka na kupiga kelele.
Kama Lissu ameaminiwa na kuzungumzia na rais Samia in confidence, kitendo cha kusema alichozungumza ni breach of confidence. Mambo mengine ni kujifunza kunyamaza, ukiaminiwa jiaminishe.
Kwa vile Mtangulizi wa Mama Samia, JPM, hutukumpangia, hivyo nashauri na Samia, tusimpangie!. Ukiomba kitu kwa mkubwa, hautoki na kuanza kupayuka umeomba nini!, Ukiomba kitu kistaarabu ni kunyamaza na kusubiria majibu ya ombi lako kimya kimya.
Hata katika kuomba vitu, zile enzi zetu za ujana, kwani huwa unatangaza umeomba nini na kwa nani?, si unaomba kimya kimya, na ukikubaliwa ndipo unatangaza tena ni kutangaza kwa barua ya posa na sio kupayuka!.
Hivyo ukiomba kitu kwa mkubwa, kisha wewe muombaji kutangazia umma umeomba nini, ni kama ama kumpangia ama kumshinikiza, hii inaweza kubadili matokeo, hata mjibu maombi angekuwa amepanga kuyatekeleza maombi yote kama muombaji alivyoomba, lakini kitendo cha muombaji kupayuka, kunaweza kumpelekea mjibu maombi akaamua asitekeleze maombi yako, maana akitekeleza, itaonekana ni kama alipangiwa!.
CCM, wapinzani, sisi sote ni wamoja, tunajenga nyumba moja, hatuna sababu ya kugombea fito, tuaminiane, CCM muwaaminie wapinzani ni Watanzania wenzetu, wana nia njema na taifa hili, na nyinyi wapinzani, muaminieni CCM ya Mama Samia, muamimieni Mama Samia kwa vile tayari ameisha onyesha kwa kauli na matendo, nia njema ya kuliponya taifa, hata ile hoja ya kuzuiwa mikutano ya hadhara, inaponyeka, hoja za wapinzani kunyanyaswa, zinaponyeka, uwezekano wa kuifumua Tume ya Uchaguzi na kuifanya huru na shirikishi inawezekana, ujenzi wa uwanja sawa (level playing ground) yakucheza mchezo wa siasa, unawezekana.
Wiki iliyopita DPP kaifuta kwa Nolle kesi ya Mbowe, na Mbowe na washtakiwa wenzake kuachiwa huru, japo kikatiba, kisheria, kikanuni na kiutaratibu ni DPP ndie pekee mwenye mamlaka ya Nolle, lakini watu wote wenye jicho la tatu wanamjua ni nani aliyeifuta kesi ya Mbowe na aliyemuachia Mbowe awe huru!.
Mbowe mwenyewe mara tuu baada ya kuachiwa huru, siku hiyo hiyo alikwenda Ikulu kuzungumza na Rais Samia, kila mtu mwenye akili, alijua Mbowe, alikwenda Ikulu kuzungumza nini na Samia, lakini hatukumsikia Mbowe, akizungumzia walicho zungumza Samia. Mbowe anajua kunyamaza, Lissu ajifunze kunyamaza!.
Kitendo cha kuachiwa kwa Freeman Mbowe ni the biggest political milestone ya rais Samia, mikutano ya hadhara itaruhusiwa, Tume huru na Shirikishi ya Uchaguzi itaundwa, Sheria ya Uchaguzi itarekebishwa na mwisho kabisa ni Rais Samia atakwenda kutupatia katiba mpya!.
Asante sana Rais Samia, Big Up Sana.
Mungu Mbariki Rais Samia ili ayaweze yote katika YEYE,
Mungu ibariki Tanzania.
Wasalaam
Paskali