Asante sana Toyota Cars

Asante sana Toyota Cars

Nimetoka sehemu na gari yangu,kufika home nacheki tairi ya nyuma kushoto,dah yote imelowa oil,
Kumwita fundi anasema ni oil ya diff,seal ya ekseli imekufa.
Nikicheki mfukoni,mambo yako ovyo vibaya sana,fundi akatoa oil seal,kwenda dukani wananiambia sh 5000/(elfu tano),nilijua labda wamekosea bei,kumbe ni sawa,nikampa fundi akafunga,nae nikampoza 5000/=,jumla nimetumia 10 tu,
Kweli kuna gari kali sana duniani,ila mwacheni toyota abaki kuwa toyota.
Toyota wanahusikaje hapo?
 
Hakuna mtu anayeweza kukudharau kama hujajidharau mwenyewe. Jamaa kasema ukweli. Na mimi nakazia. Ukiona una gari halafu kununua mafuta au spare kunakufanya uwe na ''ugonjwa wa moyo'' basi ulikuwa huko tayari ki-uwezo kununua gari. Haijalishi kama ni shida au hitaji fulani la lazima lililokufanya ukanunua!
Kwahiyo mkuu ili uwe tayari kumiliki gari ,haitakiwi uwe na pesa za mawazo za kununua spare?
 
Kwa umasikini wako unaona ni tambo ila ungekua vizuri ungeona ni jambo la kawaida,

Nyie ndio mtu akileta thd hapa kua kapigika na maisha hua wazuri wa kufariji,mara komaa mkuu utatoka tu,

Ila mtu akiongelea kidogo tu kua yupo vizuri kwa mtazamo wake mnaanza ngonjera zenu,mnapenda sana kusikia habari za watu wanadhiki japo mpate kujifariji kua kumbe kuna watu nao wanateseka! Badili hiyo fixed mind mentality ili upate kwenda mbele japo kidogo,

Halafu hiyo comment yangu nimemjibu kapuku mwenzako kutokana na swali lake alivyouliza.
Umeandika kipumbavu na kwa majivuno lakini UMESEMA UKWELI.

Japo wewe ni MPUMBAVU lakini nimekupa like kwa KUSEMA UKWELI.
 
Mkuu gari ni hitaji kama mahitaji mengine tu ya familia,na mtu inatakiwa anunue gari kulingana na mahitaji yake,sijajua wewe gari unalichukuliaje yaani,dunia imebadirika
Gari ni chombo cha usafiri tu wala sio dalili ya utajiri,mimi nimemaanisha kua mtu kama hujajipanga kumiliki gari unaweza kuona ni kama mateso au gari likakufilisi hata kidogo ulichonacho.
 
Gari ni chombo cha usafiri tu wala sio dalili ya utajiri,mimi nimemaanisha kua mtu kama hujajipanga kumiliki gari unaweza kuona ni kama mateso au gari likakufilisi hata kidogo ulichonacho.
Yeye hajaona mateso lakini na hajalalamika,ila katika hali yake hiyo amesifia kampuni,by the way ni sawa kutofautiana mtizamo
 
Yeye hajaona mateso lakini na hajalalamika,ila katika hali yake hiyo amesifia kampuni,by the way ni sawa kutofautiana mtizamo
Kuna mabinti wamepanic coz wamekariri kua mtu akisema ana Gari maana yake ni tambo au anajisifu! Hizi ni fixed mind mentality za kimasikini sana,Dunia ya leo kumiliki Gari si jambo kubwa sana au kua ni kitu cha ajabu,ila mtu akisema kapigika na maisha wao huona ni sawa coz ndio habari zinazowafariji hizo.
 
Hakuna mtu anayeweza kukudharau kama hujajidharau mwenyewe. Jamaa kasema ukweli. Na mimi nakazia. Ukiona una gari halafu kununua mafuta au spare kunakufanya uwe na ''ugonjwa wa moyo'' basi ulikuwa huko tayari ki-uwezo kununua gari. Haijalishi kama ni shida au hitaji fulani la lazima lililokufanya ukanunua!
duh kwa hiyo wewe ndo umechaguliwa na watengeneza magari ili uweke vigezo kwa mtu anaetaka kumiliki gari?kwa vigezo vyako kwamba ukiwa na gari lolote,ghafla likaharibika na ukakwama kwa muda kununua spea hitajika,basi hufai kumilliki gari,nafikiri dunia hii wenye magari ingekuwa mmoja kwa elfu moja...
 
Back
Top Bottom