Ndebile
JF-Expert Member
- Sep 14, 2011
- 7,745
- 11,267
Nashukuru nimemalizana na genge haramu la ccm. Ukweli umezidi kudhihirika kuwa idadi ya wapiga kura 29m+ ni idadi ya kupika. Idadi ya wapiga kura ni chache kuliko maelezo. Nawapongeza watanzania kwa kupuuza zoezi la kupiga kura kwani limetawaliwa na ghiliba kupitia ccm, tume ya uchaguzi na serekali. Hii maana yake ni kuwa tutakuwa na viongozi walioko kisheria, lakini wasio na uhalali wa umma. Hakuna uwezekano wa wapiga kura kufika 15m. Hongera watanzania kwa kupuuza dhuluma.