Asante Serikali, soda imepanda kwa 40%

Asante Serikali, soda imepanda kwa 40%

Wanywa soda bar tunanunua chupa moja buku siku nyingi sana.
 
Mbona sehemu nyingine za starehe soda inauzwa buku toka kitambo

Kama vipi kunywa juice cola au u fresh za watoto zile
 
Vinywaji kama Soda vipewe kibandiko cha tahadhari kwa afya (Unywaji wa Soda ni hatari kwa Afya) kama ilivyo kwa sigara!

View attachment 2327218

Si rahisi kuamini kwa kuwa ni kinywaji kilichozoeleka karibu kila dunia nzima na anayekikosoa anatakiwa awe na rundo la hoja kushawishi watumiaji kudhibiti unywaji.

Lakini ni dhahiri kwamba soda imekuwa ikihusishwa na magonjwa lukuki; saratani, figo, mifupa, mstuko wa moyo.

Pia, unywaji wa vitu vya sukari pia unasababisha kuwa na unene, kitambi na upungufu wa madini muhimu mwilini. Soda haina lishe muhimu wala faida yoyote mwilini, ndivyo wanavyosema wataalamu.

Orodha hiyo ya athari za unywaji soda pia inahusisha kuzeeka haraka, kwa mujibu wa utafitiki uliofanywa na Chuo Kikuu cha Havard cha Uingereza.

Utafiti huo unaonyesha kuwa unywaji wa soda kwa kiwango kikubwa huongeza kasi ya uzee.

Unaeleza kuwa sumu zilizo kwenye soda zinazeesha mapema. Yaani kijana mdogo wa miaka 20 hujikuta anaonekana kama wa miaka 40.

“Soda inaponyweka inaongeza uzito wa nusu kilo kwa siku, hivyo watu wanaozinywa hunenepa mara mbili zaidi ya wale ambao hawanywi. Hivyo akinenepa kupita kiasi anasababisha mwili wake kuonekana na maumbile ya uzee,” unaeleza utafiti huo.

Pia, daktari wa kutoka Kenya, Theo Wangata anasema kunywa soda kwa wingi kunaweza kusababisha kisukari.

“Kunywa soda moja ni sawa na kunywa vijiko 10 vya sukari, baada ya kunywa sukari hupanda sana mwilini na kongosho hutoa homoni ya insulini nyingi. Muda unavyozidi kwenda insulini huendelea kuishiwa nguvu (insulin resisitance) na hali hii husababisha wewe kupatwa na ugonjwa wa kisukari,”anasema.

Takwimu zinaonyesha kuwa binadamu wa kawaida hunywa vinywaji visivyolewesha, kama soda, chupa 42 kwa mwaka (sawa na gramu 1,638 ya sukari au vijiko 92 vya sukari). Tafiti pia zinaeleza kuwa mtu anayekunywa soda moja kwa siku, anakunywa zaidi ya galoni au dumu 56 za soda kwa mwaka.

“Soda ina kemikali inayoitwa phosporic acid ambayo huzuia mwili kuchukua madini ya calcium kwenye chakula. Madini hayo ni muhimu kwa ajili ya mifupa na misuli yenye afya kwenye mwili wa binadamu,” anasema daktari bingwa kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Delilah Kimambo.

Anasema soda haina lishe wala faida yeyote ile kwenye mwili wa binadamu, hivyo huongeza kiasi kikubwa cha sumu mwilini ambacho ni hatari sana kwa afya mtumiaji.

Sumu hizo huongeza hatari ya kupata ugonjwa wa moyo na kuua figo,” anasema Dk Kimambo.

Pia, anaeleza soda hupunguza kiwango cha maji mwilini kwa kuwa ina kiwango kikubwa cha madini ya sodium ambacho humfanya mtu abaki na maji kidogo na kwa muda mrefu atapata matatizo mengine ya kiafya kama mawe ya kwenye figo (kidney stone) na mawe kwenye nyongo ya binadamu.

Dk Kimambo anashauri ni vizuri kubadili mfumo wa maisha na kuanza kunywa vitu ambavyo haviharibu mwili kama vile kunywa juisi ya matunda badala ya soda.
Source: Mwanachi.
Title: elmis
 
Soda ambayo kipindi kifupi kilichopita tuliuziwa sh. 500 sasa ni sh. 700.

Kwa hesabu za harakahara hapa kuna ongezeko la sh. 200 ambayo ni asilimia 40% ya sh. 500.

Ni kweli production costs zimeongezeka kwa 40% au ni mwanya tu wajanja wanautumia kutengeneza fedha watoto wao wapelekwe chekechea za Kiingereza bila maumivu?
Anaupiga mwingi
 
Nilichogundua hawa wenye maduka sometimes wanapandisha bei lakin haiendani na uhalisia kabisa .kama wanajipangia tu hizi soda kitambo ni 600 mtaani

Utashangaa hata hizi sabuni wanazotengeneza mtaani na bei nazo zinapanda kila kukicha ukiauliza wanakumbia wameongeza bei huko.
Hapana wholesaler wamepandisha.
 
Nikiwa na hamu ya kitu chenye sukari napiga juice ya miwa tu
 
Tuache soda tunywe tongwa,huwa naweza nikamaliza mwaka sijui ladha ya soda
 
Nilichogundua hawa wenye maduka sometimes wanapandisha bei lakin haiendani na uhalisia kabisa .kama wanajipangia tu hizi soda kitambo ni 600 mtaani

Utashangaa hata hizi sabuni wanazotengeneza mtaani na bei nazo zinapanda kila kukicha ukiauliza wanakumbia wameongeza bei huko.
Faida ya bidhaa kwa rejareja huwa ni ndogo.
Wale wa jumla wakipandisha buku au jero, inawaua sana huku chini nao wanakua hawana budi kupandisha 100 au 200 kufix kale kafaida.

Na huwa hawapandishi kiholela kama unavyodhani coz nao wanaumia kwasababu wateja wao wengi ni watu wa hali ya chini hivyo bei ikiwa juu wanashindwa kuafford na wateja hawanunui.
 
Bi Mkubwa anaupiga mwingi.

Mitano tena kwake🤣🤣🤣
 
Kama soda imekushnda nenda kanywe gongo ni 500 tu,haijawahi panda bei

Sio kwamba soda imemshinda analalamikia mfumuko wa Bei. Kutoka 500 Hadi 700 ni hatari mpaka mwisho wa mwaka itakuwa 1000, thamani ya pesa itashuka na uwezo wa kununua kwa wateja itashuka pia na viwanda kupata hasara na mwishoe kupunguza wafanyakazi.
 
Soda ambayo kipindi kifupi kilichopita tuliuziwa sh. 500 sasa ni sh. 700.

Kwa hesabu za harakahara hapa kuna ongezeko la sh. 200 ambayo ni asilimia 40% ya sh. 500.

Ni kweli production costs zimeongezeka kwa 40% au ni mwanya tu wajanja wanautumia kutengeneza fedha watoto wao wapelekwe chekechea za Kiingereza bila maumivu?
CM 1774858 anasema taarifa aina hii ni uzandiki.

CCM imeleta maendeleo na mama anaipaisha nchi.
 
Back
Top Bottom