Asante Serikali ya CCM kwa kupunguza bei ya Vinywaji, punguzeni na bei ya mafuta

Natamani nifungue cha Kwangu, nasikia ni gharama ndogo tu
Kwani kuna viwanda basi? Wananunua Ethanol 95% wanai dilute kienyeji kisha wanaweka flavours na rangi . Hivyo vinywaji ni vibaya na hatari sana kwani wengi wanatumia Ethanol ambayo ni Technical grade badala ya ile beverage grade. Vifungashio wanaviapata kwa magendo na hizo stickers. Watu wananyweshwa sana sumu
 
Aiseeee ndio maana rate ya vifo ya Vijana inatisha sana
 
Lucas Mwashambwa njoo huku unaitwa.
 
Walete na wine na bia za kutoka majuu (ulaya, marekani, Australia) badala ya kila siku kunyweshwa hizi kangala zetu zilizozalishwa locally, nchi za wenzetu unakuta consumable products kutoka mataifa mbalimbali duniani ili kuwapa watu wigo mpana wa kuchagua kutokana na preferences na uwezo wao wa vipato.​
 
Hiyo technical grade alcohol unaipata wapi kwa wingi kiasi hicho, nafikiri hiyo ni kwa kazi za maabara na haiuzwi kienyeji.
 
Hiyo technical grade alcohol unaipata wapi kwa wingi kiasi hicho, nafikiri hiyo ni kwa kazi za maabara na haiuzwi kienyeji.
Zipo, wanazipata kimagendo kwani zinatumika hata kwenye printing,zinauzwa kwenye drums za ltr 200. Hii nchi imelemewa sana na maovu. Hizi K Vant, Konyagi feki zimetapakaa kwenye maduka na mabar huwezi kuzitambua hadi ukiziweka kinywani ndiyo unagundua kuwa siyo og. Kuna maiti nyingi tu zinatembea mitaani zinazotokana na unywaji wa vinywaji hivyo.
 
Haishangazi matatizo ya figo yanaongezeka kila uchwao..
 
Mithali 31: 6-7
Mpe kileo yeye aliye karibu na kupotea;
Kampe divai yeye aliye na uchungu nafsini.
7Anywe akausahau umaskini wake;
Asiikumbuke tena taabu yake.
Hili ni agano la kale achana nalo agano jipya halijakataza mkuu, we kula bia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…