Asanteni Kampuni ya Pepsi (SBC) kwa hii bidhaa yenu mpya sokoni iitwayo Supa Comando

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2015
Posts
8,018
Reaction score
16,802
Ni Kinywaji ambacho hakiishii tu kuwa Kitamu Ulimini na Kooni bali pia huchoki hata Kukinunua na Kunywa mara kwa mara.

Hakika Kinywaji kipya cha SUPA COMANDO kinachotengenezwa na Kampuni ya Pepsi (SBC) ndiyo Habari ya Mjini kwa sasa.

Na walipomaliza kabisa Mchezo hawajaishia tu Kututengenezea Kinywaji hiki Kitamu cha SUPA COMANDO bali hata Bei yake wale Masikini Wenzangu /Wanyonge wanaweza Kumudu kwani ni Shilingi Mia Tano (Jero) tu.

Na hata ilivyo katika Chupa na inavyoonekana ukiishika unaonekana kama vile ni Mtu wa Mbele (namaanisha Ulaya na Marekani) na Kukutofautisha na Waswahili na Vinywaji vyao ambavyo havikawii Kuchacha Frijini visiponunuliwa na Kuwadodea.

Shikamoo SUPA COMANDO Drink.
 
Screenshot_2023-03-04_145931.jpg
 
Athari zake za kiafya zikoje?
 
Kina faida gani kiafya mwilini mkuu ama Hawa waarabu na wahindi wanacheza na afya zetu.
Yaani Kama mie niliye na miaka zaidi ya 25 sijawahi kunywa vinywaji ivyo ambavyo zimetokea kiwandani ninakosa faida gani ambayo nazidiwa na anayekunywa.
Hebu elezea kitalaamu mkuu Mana tusifanye Mambo Kama watu hata sayansi ya darasa la tano Ni basic mno kwa maisha yetu.

Katika makundi ya vyakula sikuionaga soda
 
Hapo upate na mashitombola ( mavitumbua) sita au saba yaulale .Inakuwa burudaani .
 
Kinapatikana mikoa ioi kwa sasa huku mwisho wa Reli bado sijakiona !
 
Ni Kinywaji ambacho hakiishii tu kuwa Kitamu Ulimini na Kooni bali pia huchoki hata Kukinunua na Kunywa mara kwa mara.

Hakika Kinywaji kipya cha SUPA COMANDO kinachotengenezwa na Kampuni ya Pepsi (SBC) ndiyo Habari ya Mjini kwa sasa.

Na walipomaliza kabisa Mchezo hawajaishia tu Kututengenezea Kinywaji hiki Kitamu cha SUPA COMANDO bali hata Bei yake wale Masikini Wenzangu /Wanyonge wanaweza Kumudu kwani ni Shilingi Mia Tano (Jero) tu.

Na hata ilivyo katika Chupa na inavyoonekana ukiishika unaonekana kama vile ni Mtu wa Mbele (namaanisha Ulaya na Marekani) na Kukutofautisha na Waswahili na Vinywaji vyao ambavyo havikawii Kuchacha Frijini visiponunuliwa na Kuwadodea.

Shikamoo SUPA COMANDO Drink.
Lipia tangazo la biashara. Tunajua PEPSI wamekupa bahasha ya khaki
 
Back
Top Bottom