ASAS kuwapa Polisi Gari na Pikipiki ni kutaka kuiweka mfukoni dola

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Sidhani kaka ni sawa kwa hiki kilchofanyika tena hadharani, Kampuni ya ASAS kutoa msaada wa Pikipiki na Gari kwa Jeshi la Polisi sio jambo la kukaliwa kimya. Hii ni taasisi ya Utoaji Haki inapotokea wanatoa msaada huo je wakipatwa na makosa yanayohitaji Polisi kuwawajibisha watachukua hatua sawa au watawalinda kwakuwa ni wadau wao?

Kwenye nchi zinazofuata misingi ya Utawala Bora hili jambo lilitakiwa kupingwa kwa nguvu zote. Kitendo hicho kinamaanisha ASAS watakuwa hawachukuliwi hatua kwa lolote.
 
Kwa kusaidia taasisi au vip?. Sheria ni kitu kingine na nguv ya kuifanya sheria kuwa butu ni kitu kingine.
 
Sidhani kaka ni sawa kwa hiki kilchofanyika tena hadharani, Kampuni ya ASAS kutoa msaada wa Pikipiki na Gari kwa Jeshi la Polisi sio jambo la kukaliwa kimya. Hii ni taasisi ya Utoaji Haki inapotokea wanatoa msaada huo je wakipatwa na makosa yanayohitaji Polisi kuwawajibisha watachukua hatua sawa au watawalinda kwakuwa ni wadau wao?

Kwenye nchi zinazofuata misingi ya Utawala Bora hili jambo lilitakiwa kupingwa kwa nguvu zote. Kitendo hicho kinamaanisha ASAS watakuwa hawachukuliwi hatua kwa lolote.
Alternatively; wanaweza wakawa na mfuko kwa ajili ya huduma za jamii, ambao fedha zake watakuwa wanaipatia Serikali moja kwa moja huku wakiwa wamependekeza matumizi ya fedha hizo kwa serikali, like tunataka fedha zetu tulizotoa zitumike kwa ajili ya kununua magari ya Jeshi la Polisi

Nch yetu ni maskini, usiwazuie watu kutoa msaada wanapokuwa wana nafas bali unatakiwa uwapongeze. Unachotakiwa kufanya ni kuwashauri utaratibu wa namna wanavyoweza kusaidia, kama unaona utaratibu uliotumika siyo, ila usizuie watu kutoa msaada utaua watu
 
Sidhani kaka ni sawa kwa hiki kilchofanyika tena hadharani, Kampuni ya ASAS kutoa msaada wa Pikipiki na Gari kwa Jeshi la Polisi sio jambo la kukaliwa kimya. Hii ni taasisi ya Utoaji Haki inapotokea wanatoa msaada huo je wakipatwa na makosa yanayohitaji Polisi kuwawajibisha watachukua hatua sawa au watawalinda kwakuwa ni wadau wao?

Kwenye nchi zinazofuata misingi ya Utawala Bora hili jambo lilitakiwa kupingwa kwa nguvu zote. Kitendo hicho kinamaanisha ASAS watakuwa hawachukuliwi hatua kwa lolote.
Mbumbumbu kazini
 
Huyo huyo jamaa ukipita morogoro road pale kituo cha bucha service road ya kushoto uende hadi sheli ya resoti ni yeye katengenezabilw barabara ili magari yake yapaki,siku hizi utakuta trafic kasimama pale shell ya resoti anaongoza malori ya mafuta ya huyu bwana ili yapaki pale shel vizuri wakati huyo huku nyuma kuna foleni hadi barudi kisa magaribya huyu jamaa yanapaki risoti pale.
Kwa kweli huyu jamaa kasaweka dola mfukoni
 
Kwani yeye,ndy mtu wa kwanza kuwapa polisi msaada kama huo

Ova

Yeye labda niwa 2maana wa kwanza namjua aliewahi kuwa mkuu wa mkoa fulani aliwapa magari ya kining'inia kama yale ya watalii kule ngorongoro
 
Huu utaratibu utafanya wafanyabiashara waidharau serikali........na pia wanajenga wigo wa kukwepa kodi maana ukienda kuwadai watasema washatoa msaada kwa serikali.
 
Polisi hakuna shukrani.
yule jamaa pale magomeni jina limenitoka alikuwa muuza unga sio wakete ni jumla. polisi kituo cha magomeni walikuwa wanamlinda na vituo vyote vikubwa kutokana na mchango wake kama kuwalipa kila mwisho mwezi,kuboresha kituo,mafuta ya difender.
ila alipoingia magufuli hakuna cha nini ndani?.
mara ya mwisho nilikutana naye segerea kanunua mpaka TV ya wafungwa sikosei
 
Kimsingi hiyo itatafsirika kama ni rushwa wala si msaada. Serikali na vyombo vyake huwa havipokei msaada moja kwa moja hivyo. Kuna namna ya kutoa msaada toka mtu binafsi au taasisi isiyo ya kiserikali kwenda kwa serikali ikiwa msaada huo ni wa dharura. Wanaopaswa kupokea misaada ya namna hii ni halmashauri au taasisi nyingine ndogo ya serikali iliyo karibu na wananchi
 
Police Kwan wako mbali na wananchi..police wakisaidiwa huoni kua Ni jamiii ndio imesaidiwa ..Kuna kipind watu walilalamika police wako kwenye mazingira magum ya kazi ..anatokea mtu was kutoa msaada kwa taifa lake bdo mnakosoa
 
kile ni chombo cha serikali, ni ukakasi kupokea msaada huo. Misaada kama hiyo hutolewa na nchi fulani kupitia balozi zao. Ikitokea mtu binafsi/kampuni au taasisi isiyo ya kiserikali inatoa msaada kwa shule au dispensari ya serikali huwa inapitishia kwenye halmashauri na kama ni maafa misaada hupitia ofisi ya waziri mkuu au chombo chenye jukumu la maafa cha serikali. How come kampuni kubwa la kimataifa liwe la nje au la ndani likatoa msaada wa zana za kijeshi bila mkono wa serikali yao itaelewakaje? Serikali ni kubwa haipaswi kupokea misaada toka kwa kampuni binafsi kwa mtindo huo. Ikumbukwe hiyo kampuni inalipa kodi serikalini
 
Ukisikia nataka kuiweka serikali mfukoni hii ndo maana yake sasa. Chama cha mambuzi oyee.
 
Back
Top Bottom