LOTH HEMA
JF-Expert Member
- Dec 6, 2015
- 18,611
- 27,615
Huu mtindo wa serikali kupokea misaada toka kwa kampuni au taasisi zisizo za kiserikali au mtu binafsi ni kutengeneza mianya ya ukwepaji kodi kwa dhana ya kulipa fadhila kwa kupokea hiyo misaada. Makampuni yataona ni kawaida kuisaidia serikali. Hayo makampuni kama yanaona ya misaada yapeleke kwa taasisi zingine zisizo za kiserikali, zipo za kuhudumia watoto, wazee na makundi mengine yanayohitaji misaada. Kwanza msaada huo ni kituko, ni sawa na kupeleka maji kwenye bahari kwa kutumia kikombe cha chai ili ijae maji wakati serikali ni kubwa na ina rasilimali nyingi kuweza kuhudumia vyombo vyake