Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 40,476
- 26,173
Ndugu zangu Watanzania,
Kwa hakika Rais Samia analeta raha sana kwa Taifa hili. Huyu Mama ni neema na nuru kwa hili Taifa. Mama Samia Ni Taa na Mwanga gizani. Yaani kwa hakika kama siyo katiba ilipaswa Rais wetu Mpendwa aendelee kuliongoza Taifa letu mpaka achoke mwenyewe na kuomba kupumzika.
Sasa leo baada ya kuongeza mishahara kwa watumishi wa umma kwa asilimia nono nono zenye kuwatoa mate na kuwapa kicheko na tabasamu watumishi wa umma. Imepelekea watu wengine kutoka secta binafsi kumuunga mkono Rais wetu Mpendwa kwa kuanza kuongeza mishahara kwa watumishi wao .
Embu soma hapa chini uone namna Nchi ambavyo inaendelea kutabasamu kila kona ya mitaa.
👉Ikiwa leo Mei mosi ni siku ya Wafanyakazi Duniani, ASAS Group of Companies yenye Makao yake Makuu Iringa Tanzania, imetangaza kuwaongezea Madereva wake wote mshahara kwa zaidi ya asilimia 80.
Taarifa rasmi ya ASAS ambao wana zaidi ya miaka 80 toka waanze kuwahudumia Watanzania katika nyanja mbalimbali ikiwemo ya usafirishaji na bidhaa za maziwa, imeeleza kuwa Madereva wake ni Mashujaa wake na wanastahili heshima ya kweli.
"Kwa zaidi ya miaka 80, usafirishaji kwetu si biashara tu ni maisha yetu, sio mtindo wa muda, sio majaribio, ni damu yetu, siku hii ya Wafanyakazi, tunawapa heshima ya kweli Mashujaa wetu Madereva wa malori kwa kuongeza mishahara yao kwa zaidi ya 80%, hatukufanya kwa makofi, tulifanya kwa sababu ni haki"
"Tunawashukuru familia ya ASAS, Bodi yetu ya Wakurugenzi kwa kuunga mkono uamuzi huu wa kishujaa na Mheshimiwa Rais Samia kwa kuweka mazingira ya Taifa yanayowajali Wafanyakazi, heshima haitolewi kwa maneno, inatolewa kwa vitendo na leo tunairudisha kwa wale wanaostahili, leo hatuadhimishi kazi tu tunatambua heshima iliyo nyuma ya jasho, tunainamia kila mkono unaojenga taifa hili, hii sio Mei Mosi ya sherehe tu.... ni salamu ya heshima kwa roho ya kazi na wanaoibeba kwa moyo wa kweli" - ASAS
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.