TOKA MAKTABA :
Tumewatuma watu wetu wengi kuwa waangalizi wa chaguzi Mauritius, Botswana, Mozambique hivi karibuni mwisho wa mwaka 2024.
Je tutajifunza na kuomba utaalamu waliokusanya katika nchi hizo, au ni drama tu
TOKA MAKTABA:
Novemba 12, 2024
Port Louis, Republic of Mauritius
Taarifa ya Awali ya Ujumbe wa Waangalizi wa Uchaguzi wa SADC kwenye Uchaguzi mkuu wa Jamhuri ya Mauritius.

Taarifa ya Awali ya Ujumbe wa Waangalizi wa Uchaguzi wa SADC kwenye Uchaguzi wa mkuu wa Jamhuri ya Mauritius.
Mkuu wa Ujumbe wa Waangalizi wa Uchaguzi wa SADC (SEOM) katika Uchaguzi wa Bunge la Jamhuri ya Mauritius, Mheshimiwa Mohammed Chande Othman, Jaji Mkuu wa zamani wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tarehe 12 Novemba 2024 alitoa Taarifa ya Awali kuhusu mwenendo wa uchaguzi mkuu ( waBunge) wa nchini Mauritius .
Uchaguzi wa Bunge la Kitaifa nchini Mauritius uliofanyika tarehe 10 Novemba 2024.
Kutolewa kwa Taarifa ya Awali ya SEOM kulifanywa kwa pamoja na Wajumbe wa Mabalozi wengine watatu wa Kimataifa wa Waangalizi wa Uchaguzi katika Uchaguzi wa Bunge la Jamhuri ya Mauritius ambao ni pamoja na Mheshimiwa Dkt Joice Mujuru, Mkuu wa Ujumbe wa Waangalizi wa Uchaguzi wa Umoja wa Afrika na Makamu wa Rais wa zamani wa Jamhuri ya Zimbabwe, Mheshimiwa Nicolae Popescu, Mkuu wa Ujumbe wa Waangalizi wa Uchaguzi wa Francophonie na Naibu Waziri Mkuu wa Zamani na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Moldova; na Askofu Sipho Tembe Mkuu wa Ujumbe wa Jukwaa la Tume za Uchaguzi za Nchi za SADC na Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi na Mipaka ya Ufalme wa Eswatini.
Utoaji wa Taarifa za Awali na Mabalozi wa Kimataifa wa Waangalizi wa Kimataifa ulihudhuriwa na watu mbalimbali ambao ni pamoja na Katibu Mtendaji wa SADC, Mheshimiwa Elias Magosi, Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa UN nchini Mauritius, Bibi Lisa Simrique Singh, Mabalozi na mabalozi wa nchi za jumuiya za madola . Makamishna walioidhinishwa na Jamhuri ya Mauritius, Wajumbe wa Troika ya Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC kutoka Jamhuri ya Malawi, Zambia, na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Wajumbe wa Baraza la Ushauri la Uchaguzi la SADC (SEAC). wa Asasi za Kiraia na Mashirika ya Kidini na vyombo vya habari.
Taarifa ya Awali ya Mkuu wa Ujumbe wa Waangalizi wa Uchaguzi wa SADC kwenye Uchaguzi wa Bunge la Jamhuri ya Mauritius, Mheshimiwa Mohammed Chande Othman inaweza kupakuliwa kwenye kiungo hapa chini :
Nyaraka
Preliminary Statement of the SADC Electoral Observation Mission to the National Assembly Elections in the Republic of Mauritius | SADC