Asha Baraka nakuchukia sana

sokwe

JF-Expert Member
Joined
Mar 21, 2011
Posts
2,022
Reaction score
1,059
Nimesikitishwa sana na kifo cha binamu yangu khamis Kayumbu Amigoras kwa matatizo ya moyo, Amigoras ni ndugu yako na amefanya kazi kwenye band yako kwa miaka 18!

Unajua tatizo lake la afya, lakini umeshindwa kumsaidia hata kumchangia pesa za matibabu kwenda India kwa vile Amigoras alihama band yako! Kwanini huwezi kuwa na shukrani kwa mtu aliyekutumikia kwa miaka yote hiyo na mafanikio yote uliopata?

Kuna ubaya gani kujitoa katika band yako na kujitafutia maendeleo yake sehemu nyingine? Umekuwa kinara wa michango wakati wa uhai wa Gurumo na hata kufanya show ya band yako ili kukusanya fedha za kumsaidia!

Kwanini umeshindwa kumsaidia nduguyo lakini umeweza kumsaidia mtu baki? Ni kwasababu hutaki watu watoke band yako, unataka waendelee kuwa watumwa wako milele!

Khamis sio mtu wa kwenda magazetini kuomba msaada wa fedha za matibabu, na ulivyokuwa huna aibu kwenye msiba wake pesa za awali za maandalizi ya msiba umetoa! Ulikuwa unataka kuonesha nini? Kwanini hukumsaidia wakati wa uhai wake?

Nilikuwa nasoma kwenye magazeti jinsi ulivyokuwa mtu wa chuki na visasi wanamuziki wako wakihama band, nakuchukia sana.
 
Msaada ni hiari, sio shuruti.

Huwezi kumchagulia mtu wa kumsaidia.

Kutomsaidia mtu sio dhambi.

Ukimchukia hutafaidika na chochote.

Bahati mbaya sana kwako kuna wengine wanampenda

RIP Amigolas. sote tuko njia moja. Pamoja na Asha Baraka.
 
Sasa hapa wamueleza Asha au sisi walimwengu!?
 
kwani kumsaidia Mtu Lazima?
Kwanini Wewe Na Nduguzo Mlishindwa Kuchanga Pesa?
Muache Mama Wa Watu Naye Ana Watu Wanaomtegemea!
 
Hata kama angemsaidia matibabu unadhani yule angepona na kale kaugonjwa kake kale?
Siku zote unatakiwa utoe pesa/michango baada ya mtu kufa maana ye kasepa hana chake tena sio kwa mgonjwa,ndo maana waswazi wakasema"hujafa hujasifiwa"
 
Nimeshashtuka
mtoa Mada Kakosa Gao La Rambirambi
kaamua Hasira Zake Kuzihamishia Kwa Mama Asha Baraka
 

Kabla ya kumnyoshea kidole Asha Baraka ambaye ni mtu baki tu kwa Amigo,we sokwe na ndugu zako mlichanga shilling ngapi?

Halafu kwa nini umlalamikie manager wake wa zamani ilhali tayari alikuwa chini ya management nyingine?

Usipende kulaumu watu kwa mambo ambayo hayawahusu kihiiiivyo.

Ukisikia kila mtu atabeba msalaba wake maana yake ndo hiyo.

Huwezi mpangia mtu asaidie wakati gani ilhali pesa ni zake unapaswa umshukuru hata kwa hicho alichofanya.
 
Last edited by a moderator:

Unaweza kumsaidia mtu baki ukamuacha ndugu yako na maradhi? Ivi unajua Asha na Amigoras ni ndugu?
 

Ukisema Mimi na ndugu zangu ukamuacha Asha baraka ni ujinga! Kwasababu sote ni ndugu umenielewa? Halafu Amigoras amefanya kazi kwa Asha miaka 18! Nafikiria Kama una akili timamu unaweza kujua mchango wake kwenye mafanikio ya Asha, anawezaje kumsaidia gurumo na kumuacha ndugu yake? Kisa amehama band.
 
Last edited by a moderator:
Nimeshashtuka
mtoa Mada Kakosa Gao La Rambirambi
kaamua Hasira Zake Kuzihamishia Kwa Mama Asha Baraka

Acha ujinga ndugu! Nani aliekuambia Nina shida za pesa ya rambirambi? Na usifikiri sikumchangia wakati anahitaji pesa za matibabu
 
Hata kama angemsaidia matibabu unadhani yule angepona na kale kaugonjwa kake kale?
Siku zote unatakiwa utoe pesa/michango baada ya mtu kufa maana ye kasepa hana chake tena sio kwa mgonjwa,ndo maana waswazi wakasema"hujafa hujasifiwa"

Ugonjwa gani? Kupenda kuzushia watu tu! Inajulikana alikuwa na matatizo ya moyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…