Asha Baraka: "Sitaki Ali Choki afie kwangu''

Asha Baraka: "Sitaki Ali Choki afie kwangu''

sidhani kama unamjua Ally Choki, amechoka vibaya. Last time nimemuona yupo na King Kikii bar fulani nikawa nabisha sio yeye hadi alivyojitambulisha na kuimba kidogo.
Duh!! Amepoteza utambulisho wa sura hadi aimbe ndio anatambulika mkuu?
 
Aliyefariki ni bi shuea, mama milionea wa bandari aliyekuwa anaishi na choki kinyumba kwenye kasri lake maeneo ya tuangoma kigamboni..extra bongo na kila kitu ilikuwa ni huyu mama..alifariki 2014 kwa Kansa..kutokea hapo alichoki akachoka na extra bongo chali..akarudi kuishi uswazi
 
View attachment 687538 Baada ya msanii wa mziki wa Dance Ali Choki kupiga stori na eNEWZ wiki chache zilizopita na kusema mwaka 2018 atafanya kazi zake mwenyewe kama Mama Asha Baraka ataendelea kulala, kiongozi huyo wa Twanga Pepeta amemjibu Choki.

Mama Asha Baraka baada ya kusikia kauli hiyo amesema anamshangaa sana Ali Choki kusema maneno hayo kwani tangu mwaka jana alishamruhusu akafanye kitu anachotaka hata kama ikiwa ni pamoja na kazi zake binafsi.

''Namshangaa sana Ali Choki mimi nishampa ruhusa afanye kazi nyingine yoyote bila kujali mkataba wetu unasemaje hivyo yeye aendelee na mambo yake wala asinifikirie'' amesema.

Asha Baraka pia amesema kuwa hataki Ali Choki afie Twanga Pepeta hivyo kama ana uwezo arudi akaifufue Extra Band kwani alimpa uongozi ndani ya Twanga Pepeta akashindwa kuiongoza.

Ali Choki tayari ameshaonekana akiingia studio na msanii Beka Flavour kuandaa kazi zake binafsi hivyo huenda akawa tayari ameshajiandaa na maisha bila ya Twanga Pepeta.


EATV.
Wagombanapo........chukua jembe ukalime,Choki na Asha wanajuana kama kidole na pete,hayo yao hayatuhusu sisi tunataka rumba tu
 
Huyu Choki alitembelea nyota ya Banza Stone na huyu Asha Baraka hana lolote na mikorogo yake, wote zilipendwa.
 
Choki na Asha wanajuana kindaki ndaki watu waliokuwa wapenzi ugomvi wao sio wa kuingilia hata watoleane kashfa vipi
 
Back
Top Bottom