FMES: ina maana umekata tamaa kiasi cha kuona ni sawa kuendelea kuwa na BORA RAIS badala ya kuangalia jinsi gani ya kuzuia hilo na kuhakikisha tunakuwa na mfumo bora utakaotupatia RAIS BORA.....
Wewe utazuia na nini? Wakati Mwinyi anamaliza term yake ya pili, tuliambiwa na viongozi wetu wengi kuwa haitakuja kutokea tena kuwa na rais kama yeye, na sasa tunaye na atakapotoka atamuweka mwingine kama yeye na wananchi tutampigia kura, utazuiaje hilo wakati pamoja na uchafu wote wa mafisadi bado CCM wameshinda Kiteto, tena bila kutoa jasho, mkuu ninaishi na political realities za bongo, na besides ni haki ya kila mwananchi kugombea urais au nafasi yoyote ya uongozi wa siasa Tanzania.
WILDCARD: Hivi unamjua MANONGI ama umewahi kufuatilia sifa za kiutendaji? Unadhani MIGIRO alimpendekeza kwa ajili ya kabila lake tu? Nahsauri kama unataka kutoa maoni kuhusiana na watu ni bora ukafanya kautafiti kidogo ambacho nakuhakikishia ungelifanya ungelijua kuwa hata kama uongozi umejaa vijifisadi na mafisadi lakini bado kuna watu wa kuwaamini na maslahi ya nchi yetu kama kina MANONGI.
Hapa una point, labda niongezee tu ni kwamba wakati Mama Migiro anakwenda UN, Balozi Mnongi, alikuwa ndio kwanza anamaliza uwakilishi wake kwenye Baraza Kuu La Usalama, kama Balozi maalum kwenye urais wetu, yaani Tanzania kwenye Baraza la Usalama, alikuwa tayari anajitayarisha kwenda Adis kuwa Blaozi wetu kule, lakini wakuu wengi wa UN walimshauri Mama Migiro, kumuomba rais wetu, ili amruhusu Balozi Manongi, kuwa mmoja wa wasaidizi wake, na wakuu hao akiwemo General Gambari, walimpigia simu wao wenyewe rais wetu kumtaka amruhusu Balozi Manongi, kubaki na Mama Migiro, ni kweli kuwa huyu ni mmoja wa viongozi wachache sana bongo ambao wanaingia kwenye list ya uadilifu kwa taifa letu, hakukuwa na ukabila wala anything, UN nzima ilimshauri Mama Migiro na rais wetu kumabakihsa huyu mkuu.
Wengine: Inaelekea ule ujumbe wangu kuwa katika hali mbaya kama tuliyonayo Tanzania ni rahisi tukakimbilia kukumbatia moto wa MASIHA FEKI....Yaani ANNA KILANGO-MALECELA katoka kuwa "first late in forever waiting" hadi Presidential material......ama kweli hali ni mbaya......na hatari mno....
Haya mkuu ndio ninyaita matusi ya nguoni kwa sababu kwanza inaonyesha kuwa wewe ni binadamu usiyekuwa na heshima kabisaa au ustaarabu, ingawa una elimu kubwa sana lakini naona bado hijakusaidia kabisa mkuu, Mama Kilango, ili kuwa mbunge wa Same East, alimuondoa Waziri wa serikali ya Mkapa, aliyekuwa rafiki wa karibu sana na hata mshiriki wa kibiashara wa Mkapa akiwa rais, sasa wewe leo ambaye huna hata ukatibu tarafa, kukurupuka na maneno mazito namna hii utafikiri huyu mama ameua mtu ni ulofa mkuu wa mawazo ya kisiasa,
Mama Kilango ana haki ya kugombea urais at anytime anapotaka na ni haki ya kila Mtanzania, ningekuelewa kama ungesema makosa yake ya siasa, halafu ndio utoe hukumu, lakini kurupu na nonesense unajua unajisema kuwa wewe ni bin-adam wa aina gani mkuu, mama ni mbunge wa kuchaguliwa na wananchi, Mwinyi alikuwa mbunge kwanza kabla ya kuwa rais, Mkapa alikuwa mbunge kwanza kabla ya kuwa rais, Kikwete pia alikuwa mbunge kwanza kabla ya kuwa rais, sasa Mama Kilango ambaye ni mbunge sasa kwa nini asiwe rais akiamua kugombea? Mlituambia haya haya maneno yenu kuwa Kikwete hawezi kuwa rais na akawa, mnaongea as if baada ya muungwana itatokea miujiza basi urais utakuwa wa alliens tu, mkuu kubali ukweli kiongozi yoyote wa bongo sasa hivi mwenye level ya ubunge anaweza kuwa rais at anytime na wewe huwezi fanya anything!
Sikutaka kuiguza hii ila umeniita mwenyewe mkuu.
Ahsante Sana.