Asha Mkwizu Hauli-Na kesi ya kumuua hawara wa mumewe

Asha Mkwizu Hauli-Na kesi ya kumuua hawara wa mumewe

Umenikumbusha mbali sana.Bado najiuliza, Asha aliwezaje kumshawishi hasimu wake kwenda nyumbani kwake?

Hapo mie pia nimejiuliza sana,
Inawezekana yule dada alikuwa na imani sana
Kwani maneno ya ushawishi ya yule mama aliamini kwa nia njema

Eh mungu hii dunia!
 
hii story nimeisikia clouds wiki iliyopita na jana iliendelea vizuri sana kuna msikilizaji alikuw anasimulia alishuhudia enzi hizo akiwa form one.mtuhumiwa alifungwa gereza la isanga dodoma but sasa yupo huru alitoka kwa msamaha.
 
huyo anayesimulia alikumbuka nini..?! ni uongo mtupu wameipakuwa humu! mtambuzi alirusha huu uzi kitambo sana...
 
hii story nimeisikia clouds wiki iliyopita na jana iliendelea vizuri sana kuna msikilizaji alikuw anasimulia alishuhudia enzi hizo akiwa form one.mtuhumiwa alifungwa gereza la isanga dodoma but sasa yupo huru alitoka kwa msamaha.
Kwani alikuwa wapi siku zote asisimulie..................?
 
da!hii kesi inaliza.

nimemsimulia mama yangu nikashangaa analia sana, nimepata faida kubwa!

kumbe mama yangu alisoma na binti wa huyu mama muuaji,huyo binti yake anaitwa furaha hauli na alisoma nae forodhani primary school na walimaliza shule mwaka 1985!(mwaka wa hukumu ya mama yao) mama yangu anasema huyo furaha alikuwa na mdogo /wadogo zake pale shuleni na pia mama yangu nae alikuwa anakaa upanga na hiyo familia ilikuwa inakaa upanga mtaa wa lugalo karibia na flats wanazokaa madaktari.

anasema hawa watoto waliathirika sana kipindi cha ile kesi kisaikolojia na kimaisha, maana mama huyu alikuwa anaishi nao pale upanga na kuwalea vema hawa watoto na anasema siku ya hukumu mama yao alipata fursa ya kuwaaga watoto wake kuwa anaenda kunyongwa-walilia sanasanasana na kugaragara chini.

huyo furaha alifaulu akaenda zanaki, pia mama yangu anasema miaka ya tisini anakumbuka akiwa morogoro aliwahi kumuona huyu furaha na wakaongea sana kuhusu mama asha mkwizu, huyo furaha alikuwa anatoka dodoma, anasema mpaka wakati huo alikuwa hajatoka gerezani!

ndo walikuwa wanafuatilia
 
Hakika wewe ni MTAMBUZI
Visa vyako huniacha hoi.
Nasubilia ile kesi ya kina Uncle TOM na wenzie maana hiyo unipa sababu ya kutaka kujua ni nini kilifanyika na kilifanywaje na ni watu gani walikuwa nyuma ya huo mkakati.
 
Chona;

Naifanyia kazi mkuu.
 
Last edited by a moderator:
chonde chonde wakuu nawaombeni kwa heshima na taadhima kesi ya mama Taji msiisasanue hapa. Kuna siku niligusia jambo hili memba mmoja wa mmu likam touch sana (ana ukaribu na Taji) na akaomba tusilizungumzie hapa,ni kidonda kibichi bado kwake. Nawaombeni tafadhali.
Mimi nina ukaribu na Happiness Senzota.....mwenye hiyo kesi ya Liundi wekeni hapa.....wengi tunamachungu ya baba zetu kupigwa chini,kesi zao kuwekwa hapa JF tena za baba zetu ni wizi na ubakaji...
 
Kesi kama hii na ya mume wa Josephine kwa upande wa pili wa shillingi zinaumana. Hii ilikuwa ni mwanamke kuingilia ndoa na Josephine na Slaa ni ya mwanamme kuingilia ndoa! likitokea la kutokea siku ya siku, tusiseme tulikuwa hatujui.

Tafadhali Rib hebu tuliza kinywa chako. Josehine Slaa alikuwa ameachana na mume wake siku ningi sana kiasi kwamba aliyeanza kuwa na mahusino na mtu mwingine ni mume wake. Waliachana more than two years na kwa sheria za ndoa ukitengana na mwenzi wako kwa kipindi cha miaka miwili mfulilizo bila tendo la ndoa ni tayari ndoa imevunjia inasubiri tu uthibitihso wa karatasi ya talaka. Dr. Slaa naha kosa na pia waliridhiana na mke wake wa awali kutokana na tofauti zao kuwa basi, waliachana kizungu na si kiafrika kama nduguzanguni na ndiyo maana are friends na hawajawahi kutuhumiana hata kidogo hadharani wala otherwise. So please, mdau usidandie train kwa mbele itakusaga. Dr. Slaa is clean hata maaskofu wanamtetea, uliza cha moto alichokipata yule waziri mwenye sura ya kima aliposhambuliwa na maaskofu kwa kumkashifu Dr. He is our next presindent, hata kwa term moja tu asafishe matapishi ili tufurahiye nchi yetu kwa huduma safi za jamii ikiwemo elimu. Hivi unajua kuwa kwa utajiri wetu tunaweza kusoma bila ada hadi chuo kikuuu? But wachache wanatufanya watoto wetu na wajukuu wanasoma kwa kuhemea mkopo na mabomu ya machozi na virungu. Enough is enough, we need change, it is a must!!!
 
Big up Mchambuzi kwa uchambuzi mzuri
naona clouds wamekupa shavu pia kwa kuisoma hii habari
ktk kipindi chao cha leo tena.WAME ACKNOLEDGE SOURCE JAMII FORUM
 
Kaka SON OF ALSKA kumbe upo afadhali mana nilidhani umepatwa na janga kwa mawasiliano kukatika ghafla haya salam zao huko.
 
Yes big up Mtambuzi maana wamekutaja kabisa na jina lako kuwa wewe ni unajulikana humu kama Mtambuzi. Clouds fm bado wanaichakachua kwa kuwasomea wananchi as navyoandika.

Big up to Jamii forums.
 
Yes big up Mtambuzi maana wamekutaja kabisa na jina lako kuwa wewe ni unajulikana humu kama Mtambuzi. Clouds fm bado wanaichakachua kwa kuwasomea wananchi as navyoandika.

Big up to Jamii forums.

nafurahi kama wamemtaja jina inatosha inaonesha ujumbe ulifika... big up LEO TENA KWA HILO .. kuna baadhi ya watu pia wameweka hiki kisa kwenye vi blog vyao ... kweli JF ni kisima
 
kwa kweli Mtambuzi ww ni mtambuzi wa ukweli

asante kwa kazi yako ya kutufunda historia ya
 
nafurahi kama wamemtaja jina inatosha inaonesha ujumbe ulifika... big up LEO TENA KWA HILO .. kuna baadhi ya watu pia wameweka hiki kisa kwenye vi blog vyao ... kweli JF ni kisima

Nakushukuru sana Mkuu Viper kwa kufuatilia habari za mkasa huu jinsi ulivyoshika kasi kwenye mitandao mingine ikiwemo kituo cha redio cha Clouds FM.

Nawashukuru kwa kutambua mchango wangu humu JF, na hii si sifa kwangu pekee bali pia sifa hii ni kwa wana JF wote waliokuwa wakinichagiza niwe naweka kesi za hapa nchini hususan kesi hii ya Asha Mkwizu ambayo iliombwa na wana JF wengi na kwa msaada wa Mahakama kuu niliweza kuipata na kuitafsiri kama ilivyo.

Labda kitu kingine ambacho sikukieleza hapa ni kwamba baada ya kuiandika kesi hii, pia nilipata bahati ya kufanya mazungumzo na Mheshimiwa Jaji A. Bahati ambaye ndiye aliyeisikiliza kesi hii. Mazungumzo yetu hayakujikita kwenye kesi hii ya Asha Mkwizu tu, bali pia tulizungmzia kazi zake za mapema kabla hajastaafu.

Alionesha kufurahishwa na utaratibu huu niliojiwekea wa kuzirejea kesi mbalimbali zilizotokea hapa nchini na kwingineko. Alisema itakuwa ni kumbukumbu nzuri kwa vizazi vijavyo na pia jamii itapata fursa ya kujifunza kupitia kesi hizo.
 
baada ya kusikiliza clouds,na ku admit wameitoa sousrce bjf kwa mtambuzi,ikanibidi nifuatilie.hongera zako mtambuzi.maana dina alivyokuwa akisoma mwanzo mpaka mwisho,nilisikiliza kwa makini,na mwenyewe anavyosema kuwa huyo mama ameokoka
 
Ahsante kwa taarifa, lakini ni vyema hata kule kwenye Blog yake (Dina Marios) aseme hivyo hivyo......................!
 
Back
Top Bottom