Ashugulikiwe aliyepo nyuma ya Kagame na M23 yake kukomesha umwagaji damu mashariki ya DRC

Ashugulikiwe aliyepo nyuma ya Kagame na M23 yake kukomesha umwagaji damu mashariki ya DRC

Mdude_Nyagali

Member
Joined
Dec 11, 2022
Posts
79
Reaction score
1,444
Fikiria hawa ni raia wameuawa na M23 huku askari wetu wawili wa JWTZ na askari wanne wa South Africa waliokuwa wakiwalinda raia nao wakiuawa kikatili.

Nchi ya Congo ingekuwa haina madini na rasilimali zingine sidhani kama huyu Paul Kagame na Kaguta Museveni wangekuwa na kashfa ya kuwa nyuma ya Mzozo wa DRC wakisizingia kutafuta waasi wanaopinga serikali zao waliokimbilia huko. Ukiona dikteta yoyote anakaa muda mrefu madarakani halafu huoni mataifa ya Ulaya yakimlalamikia kaa ukijua kuwa dikteta huyo ni kibaraka wao. Ndivyo ilivyokuwa kwa Mubutu Sese seko.

Mobutu alikuwa kibaraka wa mataifa ya magharibi na walimuweka baada ya mataifa hayo kumuua baba wa taifa la Congo DCR Patrice Lumumba aliyepigania uhuru wa taifa hilo kutoka kwa wabelgiji. Walifanya hivyo ili iwe rahisi kuvuna rasilimali za Congo kwani ilikuwa ngumu kuvuna chini ya Patrice Lumumba ambaye alikuwa ameshaanza kuwafungia vioo. Baada ya kumuua Patrice Lumumba walianza kuvuna rasilimali za Congo kwa wanavyotaka huku wakimlinda Mobutu. Licha ya udikteta wa Mobutu wa kuteka na kuua wapinzani wake hawa nchi za magharibi hawajawahi kumkemea kwa sababu alikuwa kibaraka wao huku wakimtajirisha.

Kuna wakati akina Nyerere, Kaunda na wengine walimtenga Mobutu kwenye Mulungushi Club. Wakati huo marais wa nchi za kusini mwa Africa ambao kwa sasa ni SADC waliokuwa mstari wa mbele kupigania uhuru wa nchi za kusini mwa Africa waliunda Club iliyoitwa Mulungusi ambayo kazi yake ilikuwa ni mikakati ya kusaidia nchi za kusini mwa Africa ambazo zilikuwa hazijapata uhuru ikiwemo Zimbabwe na South Africa.

Mobutu kibaraka wa nchi za magharibi akawa anavujisha siri kwa mabwana zake mikakati yote ya Mulungusi Club. Inabidi mwalimu Nyerere na wenzake wamteme.

Baada ya anguko la Mobutu sasa Kagame akabadili nafasi hiyo ya ukibaraka wa kuwatumikia mataifa ya magharibi kufanya machafuko mashariki mwa Congo ili kupata mwanya wa kuvuna rasilimali za nchi hiyo katika eneo hilo. Kisingizio cha Kagame ni kuwatafuta waasi wa kihutu waliokimbilia Congo tangu wakati wa mauaji ya kimbali nchini Rwanda mwaka 1994. Ukweli ni kwamba huu ni uongo na waasi hao wanatumika kama kichaka tu cha kuficha uovu wa Kagame na wafadhili wake wa nchi za magharibi.

Leo tujiulize madini yanayouzwa kwenye soko la dunia kutokea Rwanda yanatoka wapi kama sio Congo? Kwanini Kagame anakuwa dalali wa kumwaga damu za waafrica wenzake kwa faida ya wazungu wa mataifa ya magharibi? Kagame anasoma biblia hivi hajui kwamba damu ina tabia ya kisasi?

Ukimuona mbuzi juu ya mti ujue kapandishwa. Kagame ni mbuzi aliyepandishwa juu ya mti. Huyo aliyempandisha ndiye ashugulikiwe. Kwa hiyo ukitaka kutatua tatizo dili na chanzo cha tatizo na sio tatizo. Viongozi wa SADC na Africa walipaswa kushugulika na aliye nyuma ya Kagame hizi nchi za magharibi ikiwemo ufaransa ambazo ndio zinampa kiburi kama walivyokuwa wanampa kiburi Mobutu. Kwa bahati mbaya nchi za SADC zinadili na Kagame huku zikiogopa kudili na boss wa Kagame nchi za magharibi kwa sababu ya kukosa mikopo na misaada.

Kama Africa bado tuna safari ndefu sana maana ndani yake wapo viongozi waoga, wezi na mamluki wa nchi za magharibi.

Mdude Nyagali 7 x 70 Sumu ya Nyigu.
 
Mkuu Mdude,

Andiko lako zuri, lakini Mobutu asingeweza kuvujisha siri za Mulungushi club kwakuwa hakuwahi kuwa mmoja wa viongozi waliokuwa kwenye hiyo club.

Mulungushi club ilikuwa na viongozi watatu, Nyerere, Kaunda na Obote. Hii ndiyo ilikuja kuzaa kulichojulikana kama nchi zilizokuwa mstari wa mbele kwenye ukombozi kusini mwa Afrika chini ya uenyekiti wa Tanzania (Nyerere), na hatimaye kadri nchi zilivyopata uhuru umoja huo ukakua na kuzaa SADC.

Hata wakati SADC inaanzishwa, Congo chini ya Mobutu haikuwa mwanachama.
 
Kuna mada moja tu hapa.kuweka vikwazo nchi hizi mbili uganda na rwanda yani hakuna katika jumuiya ya SADC na EAC kuzuia kila kitakacho pita.siku mbili tu uganda na rwanda viburi vitakwisha.
Maana hawana bahari wa njia za kupitisha silahaa na mambo mengine.
 
Dawa ya Paul Kagame siyo kushughulika na wanaomtuma (nchi za magharibi), bali ni kumshughulikia yeye mwenyewe.

Huyu Kagame ni wa kupigwa risasi tu kama ambavyo amekuwa anawaua mahasimu wake.

Na hili haliko mbali
Kuna kitu nimejaribu kuwaza. Nchi za Tanzania na Kenya haziwezi kumwekea vikwazo kwenye bandari kumlazimisha kumaliza hii vita?

Sioni kama ana njia nyingine kupitisha bidhaa zake mbali na Tanzania na Kenya.
 
Huyo aliyempandisha ndiye ashugulikiwe.
Samahani,ukitumia akili vizuri hapa umemaanisha Wamagharibi (West), unavyoona kwa sasa kuna taifa linaweza kuwavimbia West??

West kinara wao ni G7, ukitumia akili yako unawaweza hao?? Muangalie Mrusi dude alilopewa jinsi linavyomchosha, Africa itaweza??
 
Kuna mada moja tu hapa.kuweka vikwazo nchi hizi mbili uganda na rwanda yani hakuna katika jumuiya ya SADC na EAC kuzuia kila kitakacho pita.siku mbili tu uganda na rwanda viburi vitakwisha.
Maana hawana bahari wa njia za kupitisha silahaa na mambo mengine.
Hiyo inawezekana kama Tanzania na Kenya zitaamua kwa pamoja.
 
1738589405520.jpg
 
Samahani,ukitumia akili vizuri hapa umemaanisha Wamagharibi (West), unavyoona kwa sasa kuna taifa linaweza kuwavimbia West??

West kinara wao ni G7, ukitumia akili yako unawaweza hao?? Muangalie Mrusi dude alilopewa jinsi linavyomchosha, Africa itaweza??
G7 ndio wamechoka urusi bado ipo ngangari usihAribu uzi
 
Dawa ya Paul Kagame siyo kushughulika na wanaomtuma (nchi za magharibi), bali ni kumshughulikia yeye mwenyewe.

Huyu Kagame ni wa kupigwa risasi tu kama ambavyo amekuwa anawaua mahasimu wake.

Na hili haliko mbali
Very true dawa ni ku-deal na ye mpuuzi huyu
 
Back
Top Bottom