Maelezo marefu yanatolewa na mtu anayewafahamu vizuri viongozi wa kiAfrika namna walivyo na haiba zenye kushabihiana!
Kwa taarifa yako ni kwamba, viongozi wa Afrika mostly ni kama nyumbu.
Nyumbu hawezi kutoa msaada kwa nyumbu mwenzake aliyekunjwa shingo na simba, kwa sababu, aliyeangushwa kuliwa si yeye, kwa hiyo jambo hilo linakuwa halimhusu.
Hata hicho kikao cha SADC na EAC kilichoitishwa Dar siku ya Juma mosi, kama hakitaweza kutoka na agenda moja yenye maamuzi ya kimshikamano, basi tujue kuwa kwa sababu mdhila ya raia wa Congo DR si yao, hivyo hayawahusu.
Uamzi uliotakiwa kufanywa kukomesha longolongo pamoja na kutoa msaada wa maana kwa DRC ni kuunda jeshi la pamoja kwa nchi zote wanachama ili kuingia kijeshi/kivita kuinusuru Congo.
Na gharama za kuliwezesha jeshi hilo zibebwe na nchi wanachama husika.
Kutegemea jeshi lolote linalopelekwa kulinda amani kwa mwamvuli wa Umoja wa mataifa ni kutokuitakia mema nchi husika.
Maana misheni nyingi za UN za walinda amani huwa haziruhusiwi kupigana ama kujibu mapigo, si za kutegemea kulinda usalama wa watu, hazisaidii na hazifai.
Kwa hiyo bw. Mdude ikitolewa hoja ya kuunda jeshi la pamoja kwenda kuwafurusha M23 na wawezeshi wa jeshi hilo wakawa ni nchi husika zitakazounda jeshi hilo, hao magaidi watabakia kuwa ni historia.
Lakini viongozi wakienda na hoja za blah blah za UN na takataka zingine za kufanana na UN, hakuna lolote lamaana linaloenda kutokea.