Ashugulikiwe aliyepo nyuma ya Kagame na M23 yake kukomesha umwagaji damu mashariki ya DRC

Wewe ndiye umetumia akili?
Ndiyo, wewe je?? Vikwazo havijaleta madhara kwa Urusi?? Jibu kwa kutumia akili.

 
Maelezo marefu yanatolewa na mtu anayewafahamu vizuri viongozi wa kiAfrika namna walivyo na haiba zenye kushabihiana!

Kwa taarifa yako ni kwamba, viongozi wa Afrika mostly ni kama nyumbu.

Nyumbu hawezi kutoa msaada kwa nyumbu mwenzake aliyekunjwa shingo na simba, kwa sababu, aliyeangushwa kuliwa si yeye, kwa hiyo jambo hilo linakuwa halimhusu.

Hata hicho kikao cha SADC na EAC kilichoitishwa Dar siku ya Juma mosi, kama hakitaweza kutoka na agenda moja yenye maamuzi ya kimshikamano, basi tujue kuwa kwa sababu madhila ya raia wa Congo DR si yao, hivyo hayawahusu kuyashughulikia kwa ukamilifu.

Uamzi uliotakiwa kufanywa kukomesha longolongo pamoja na kutoa msaada wa maana kwa DRC ni kuunda jeshi la pamoja kwa nchi zote wanachama ili kuingia kijeshi/kivita kuinusuru Congo.

Na gharama za kuliwezesha jeshi hilo zibebwe na nchi wanachama husika.

Kutegemea jeshi lolote linalopelekwa kulinda amani kwa mwamvuli wa Umoja wa mataifa ni kutokuitakia mema nchi husika.

Maana misheni nyingi za UN za walinda amani huwa haziruhusiwi kupigana ama kujibu mapigo, si za kutegemea kulinda usalama wa watu, hazisaidii na hazifai.

Kwa hiyo bw. Mdude ikitolewa hoja ya kuunda jeshi la pamoja kwenda kuwafurusha M23 na wawezeshi wa jeshi hilo wakawa ni nchi husika zitakazounda jeshi hilo, hao magaidi watabakia kuwa ni historia.

Lakini viongozi wakienda na hoja za blah blah za UN na takataka zingine za kufanana na UN, hakuna lolote lamaana linaloenda kutokea.
 
Kuna kitu nimejaribu kuwaza. Nchi za Tanzania na Kenya haziwezi kumwekea vikwazo kwenye bandari kumlazimisha kumaliza hii vita?

Sioni kama ana njia nyingine kupitisha bidhaa zake mbali na Tanzania na Kenya.
Hii ni njia rahisi sana. Lakini ngumu kutekeleza
 
Ni pale unapokuwa na hasira za kumpiga mwizi, kumwangalia vizuri kumbe ndo faza yako. Aliyepo nyuma ya Kagame ndio anaetoa 70% ya misaada yenu yote. Hadi chandarua unacholalia na mke wako ni yeye kakupa bure, kwa hio acha makasiriko.

Ukiwa ombaomba tegemea na wewe kuombwa, sasa usianze kurusha miteke, ukikataa watakamata hiyo miguu, ndio Kongo hiyo, mzigo lazima...
 
Ndiyo, wewe je?? Vikwazo havijaleta madhara kwa Urusi?? Jibu kwa kutumia akili.
Nitajie nchi moja kwenye hizo G7 ambayo haijaathiriwa na vikwazo walivyomwekea Russia. Tatizo mnasoma kile wanachotaka wao msome.
 
Kuna kitu nimejaribu kuwaza. Nchi za Tanzania na Kenya haziwezi kumwekea vikwazo kwenye bandari kumlazimisha kumaliza hii vita?

Sioni kama ana njia nyingine kupitisha bidhaa zake mbali na Tanzania na Kenya.
... kama sio njaa ya Ruto hili lingewezekana, lakini kwa sasa Ruto tayari kaishanunuliwa na anaendeleza wimbo uleule wa M23 NI WACONGOLESE!
 
Dawa ya Paul Kagame siyo kushughulika na wanaomtuma (nchi za magharibi), bali ni kumshughulikia yeye mwenyewe.

Huyu Kagame ni wa kupigwa risasi tu kama ambavyo amekuwa anawaua mahasimu wake.

Na hili haliko mbali
Hata leo Kagame akiondoka hiyo vita haitaisha, M23 ni Congolese sio Rwandese, serikali ya Congo imekataa kuwatambua Banyamurenge kama raia wa Congo na imejaribu mara nyingi kuwafanyia genocide , na huyu mdude ndio yule wa Chadema? Kama ni yeye kwa akili kama hii basi Chadema wanapoteza muda tuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…