Asikwambie mtu, Mgao wa umeme wamiliki wa viwanda wanaisoma Namba

Asikwambie mtu, Mgao wa umeme wamiliki wa viwanda wanaisoma Namba

The Burning Spear

JF-Expert Member
Joined
Dec 23, 2011
Posts
4,118
Reaction score
9,864
Hivi ndivyo ninavyoweza kusema kwa ufupi, hali ni mbaya sana kwa wamiliki wa viwanda Tanzania tangu kuondoka kwa uncle mambo yamebadilika sana.

inawezekana baadhi ya wawekezaji walifurahia kuondoka huyu mwamba ila wakati wanaopitia kwa sasa mungu mwenyewe anajua.

iko ivi viwandani huwa wanaenda na Targets yaani Daily, monthly hadi mwisho wa siku wanapata annual production volume, kinachotokea kwa zaidi ya miezi sita sasa na zaidi production targets hazifikiwi.

Na unapozungumzia production maana yake ni hela, inafika mahali soko lipo ila bidhaa ya kwenda sokoni hamna, kwa lugha nyepesi ni kwamba wanapata hasara kwa sababu running costs zipo pale pale kama mishahara etc.

Matatizo ya umeme ni mengi hata kama siyo mgao lakini hitilafu haziishi, hii imepelekea niamini kupata wawekezaji wa viwanda kutoka ulaya Tanzania ni ngumu sana tutabaki na hawa Baniani.

To convince serious investors Electric power must be: -
1.Available
2.Stable
3.Reliable.



CC; Mzee Makamba. Maharage
 
Vyanzo ni vingi si lazima kutegemea grid ya taifa.
Mfano una mashine ya kukokoboa mpunga, kuranda mbao, garage ya kumwaga oil una nishati tosha ni wewe tu kuigeuza oil chafu, maranda, nk kuwa tu umeme.
 
Mfano China wanavipower plant saize uitakayo unafua umeme kulingana na matumizi ya kiwanda chako. Mfano tuna makaa tele uhangaika na tanesco ya nini
 
Mfano China wanavipower plant saize uitakayo unafua umeme kulingana na matumizi ya kiwanda chako. Mfano tuna makaa tele uhangaika na tanesco ya nini
Power plant za kutumia ni Genereta tu iwe ni kiwanda ama mtu binafsi nje ya hapo utaambiwa ni muhujumu uchumi wewe
 
Power plant za kutumia ni Genereta tu iwe ni kiwanda ama mtu binafsi nje ya hapo utaambiwa ni muhujumu uchumi wewe
Siku hizi mchina anauza solar generators za ukubwa wowote,, hii inapata umeme wa jua ka kuuhifadhi kwA matumizi,,
Wanaunda wind turbines za ukubwa kuanzia hata wat 1000,2000,5000,etc, unanunua na kuweka juu ya paa, upepo ukiwepo kanafua umeme wa kuwasha nyumba na kuendesha mitambo midogo,,
Nashangaa wanaoenda china hizi vitu hawaviona au ushamba unasumbua🙆‍♀️
 
Mi naona kama mgao umepungua sana, sio kama oktoba na November
Mtafute mtu wa saloon ,Welding watakwambia wanayo ya pitia maana hao 100% wanategea umeme,mfano leo umeme tokea 12 hamna,now nipo mzigoni sijui kama ,umerudi.Sema sisi Watanzania wazee wa hewala tushazoea,japo kuna watu ambao biashara zao zinategemea umeme wanaumia .
 
Power plant za kutumia ni Genereta tu iwe ni kiwanda ama mtu binafsi nje ya hapo utaambiwa ni muhujumu uchumi wewe
Sio kweli, mbona viwanda vya sukari,vya karatasi njombe ,nk utumia,
 
Wananchi wangejua ccm wanavyotumia dhanama ya ccm kukopa mihela kibao na kuandika proposal kibao wangekomaa kuwaondoa but, people don't know
Halafu mwenyekiti wao amewaambia kabisa kila mbuzi 🐐 na ale kwa urefu wa kamba yake...!!
 
Viwanda vilikua na adha hii toka kipindi cha hayati. Kipindi cha hayati umeme mwingi ulikua unaelekezwa kwa wananchi na viwandani wanapewa kwa mgao. Viwanda vingi tu huko tanga vilifungwa.

Bado serikali yetu ina siasa chafu kwa kuyapa kipaumbele mambo yasiyo muhimu na kuacha muhimu yapite
 
Back
Top Bottom