Asili na Maana ya Jina/majina ya sehemu mbalimbali Tanzania

Asili na Maana ya Jina/majina ya sehemu mbalimbali Tanzania

1.KIBORILONI & KIBOSHO[MOSHI].
Kiboriloni ni neno lililotokana na maneno mawili KIBO ALONE. Hii ilikuwa sehemu ambapo wazungu walisimama na kuona kilele cha Kibo pekee bila kukiona kilele cha Mawenzi, Kibo na Mawenzi ni vilele vya Mt. Kilimanjaro.Kibosho lilitokana na maneno KIBO SHOW, hii ni sehemu ambapo Kibo kilionekana vizuri zaidi.

2.KARIAKOO.
Inasemekana Kariakoo ilikuwa kituo cha Askari wa kikoloni CARRIER COP, Wabantu wakarahisisha kwa kupaita Kariakoo.

3.KOLOMIJE[BUNDA].
Inasemekana mahali hapo alifika Mzungu aliyeitwa James.Yule Mzungu akataka watu wamwiite 'J' badala ya kutamka jina lote. Hivyo akawaambia CALL ME J, wabantu wakatamka KOLOMIJE na kutengeneza jina la lile eneo.

4.CHEKERENI[MOSHI].
Hili ni eneo ambapo barabara inakatiza kwenye reli.Sasa wazungu waliweka alama ya bararani ya tahadhari kabla ya kuvuka reli CHECK THE LINE, watu wakatamka CHEKERENI na kuliita hivyo lile eneo hadi leo.

5.NEWALA [MTWARA].
Inasemekana kwamba waingereza walipofika Mtwara walikuta kisima kilichojengwa na wajerumani ambacho kilikuwa cha kizamani kwa wakati huo.Hivyo walijenga kisima kipya na kukiita NEW WELL, watanganyika wakatamka NEWALA, hatimaye likawa jina la ile sehemu.

N:B SOURCE yake ni HEARSAY STORIES....unaweza kusahihisha ama kuongeza majina mengine.
LUKULEDI (Look ladies) Wazungu walikuwa wakioneshana wanawake wakati wanaoga mtoni, baadae ikawa jina la mto
 
Idodomyia wagogo eneo la ardhi lilikua linazama wakawa wanasema idodomyia= dodoma now baada ya kushindwa sema kirugha chao
 
Kimara baruti kulikua na ghala ya jeshi la kuifadhi baruti
 
Foleni = four line. Ilikuwa ni utamaduni wa manamba kuhesabiwa ktk mistari minne
 
Sea breeze= Chibirizi (Kigoma)

Ila samahani mleta mada kuna majina huku Manyara yanaishia na consonant sijui chanzo chake mf. Katesh, Hanang, Endabash, Endasaq,
Huko wabarbeig ndo wakata majina wazuri wa maeneo walikopitia alafu wairak wanazikolezea
 
Mkuu Wairaq sidhani kama ni wabantu wenzetu[Mimi siyo mbaguzi] wao pamoja na jamii mbalimbali za wafugaji wana asili tofauti na ya watu wengine.

Ndio maana Lugha zao hazijachangia neno lolote kwenye lugha ya Kiswahili[pia sina uhakika] hivyo kuziondoa miongoni mwa lugha za kibantu na ndio sababu iliyonifanya niseme siyo wabantu......Kuna neno linatamkwa Haidom nalo lina niacha hoi sana.
Ukiangalia maeneo mengi yanayokaliwa na wairak majina ya hayo maeneo ni ya kibarbaig
 
Mikocheni asili yake ni jina la mzungu Mike Chain aliyeishi mitaa hiyo, kama tunavyosikia majina kama kwa Warioba (njia ya Kawe) au kwa Mwinyi (njia ya Buza) au kwa Mkoremba, Kwa Mpalange, kwa Azizi Ally nk

Kariakoo ilikuwa ni sehemu ya kuchukulia mizigo na kuipeleka bandarini kwa hiyo iliitwa '' Carry and Go'' na wazaramo wakasema Kari-a-koo
 
Dah yaani linaleta mantiki kabisa Mkuu.....hii lugha ilikuja kwa meli aisee.
Yale maeneo ya Iringa yalivamiwa na wagiriki walima tumbaku na wajerumani, sasa wakati wanapima mashamba yao ili wagawane wakawa wanasema keep on zero kama reference point. Wahehe wakajua pale ni kiponzero !!!!!!

Nawapenda Wahehe, sababu mkoa mzima hakuna majina ya kizungu kwenye mitaa yao, ila kijiji kimoja tu, Pomern (jerumani), kipo kilolo.
 
kakueleza ni kijerumani. Nenda google ulizia maana yake. Tunatumia kijerumani sababu ndo walioanzisha shule bara. Tanga ikiwa kianzio.
Nafahamu ni la Kijerumani, ila mimi nilitaka maneno ya Kingereza.

Hata hivyo Shule siyo jina la eneo kwani karibu kila mahali kuna Shule.
 
Yale maeneo ya Iringa yalivamiwa na wagiriki walima tumbaku na wajerumani, sasa wakati wanapima mashamba yao ili wagawane wakawa wanasema keep on zero kama reference point. Wahehe wakajua pale ni kiponzero !!!!!!

Nawapenda Wahehe, sababu mkoa mzima hakuna majina ya kizungu kwenye mitaa yao, ila kijiji kimoja tu, Pomern (jerumani), kipo kilolo.
Hahahahaaa......dah! nimecheka sana aisee....kutoka keep on zero hadi Kiponzero? kweli Wahehe hawapendagi ujinga,....unawaongelesha kithungu kwani uliwapeleka Shule?
 
Back
Top Bottom