Asili na Maana ya Jina/majina ya sehemu mbalimbali Tanzania

LUKULEDI (Look ladies) Wazungu walikuwa wakioneshana wanawake wakati wanaoga mtoni, baadae ikawa jina la mto
 
Idodomyia wagogo eneo la ardhi lilikua linazama wakawa wanasema idodomyia= dodoma now baada ya kushindwa sema kirugha chao
 
Kimara baruti kulikua na ghala ya jeshi la kuifadhi baruti
 
Foleni = four line. Ilikuwa ni utamaduni wa manamba kuhesabiwa ktk mistari minne
 
Sea breeze= Chibirizi (Kigoma)

Ila samahani mleta mada kuna majina huku Manyara yanaishia na consonant sijui chanzo chake mf. Katesh, Hanang, Endabash, Endasaq,
Huko wabarbeig ndo wakata majina wazuri wa maeneo walikopitia alafu wairak wanazikolezea
 
Ukiangalia maeneo mengi yanayokaliwa na wairak majina ya hayo maeneo ni ya kibarbaig
 
Mikocheni asili yake ni jina la mzungu Mike Chain aliyeishi mitaa hiyo, kama tunavyosikia majina kama kwa Warioba (njia ya Kawe) au kwa Mwinyi (njia ya Buza) au kwa Mkoremba, Kwa Mpalange, kwa Azizi Ally nk

Kariakoo ilikuwa ni sehemu ya kuchukulia mizigo na kuipeleka bandarini kwa hiyo iliitwa '' Carry and Go'' na wazaramo wakasema Kari-a-koo
 
Dah yaani linaleta mantiki kabisa Mkuu.....hii lugha ilikuja kwa meli aisee.
Yale maeneo ya Iringa yalivamiwa na wagiriki walima tumbaku na wajerumani, sasa wakati wanapima mashamba yao ili wagawane wakawa wanasema keep on zero kama reference point. Wahehe wakajua pale ni kiponzero !!!!!!

Nawapenda Wahehe, sababu mkoa mzima hakuna majina ya kizungu kwenye mitaa yao, ila kijiji kimoja tu, Pomern (jerumani), kipo kilolo.
 
kakueleza ni kijerumani. Nenda google ulizia maana yake. Tunatumia kijerumani sababu ndo walioanzisha shule bara. Tanga ikiwa kianzio.
Nafahamu ni la Kijerumani, ila mimi nilitaka maneno ya Kingereza.

Hata hivyo Shule siyo jina la eneo kwani karibu kila mahali kuna Shule.
 
Hahahahaaa......dah! nimecheka sana aisee....kutoka keep on zero hadi Kiponzero? kweli Wahehe hawapendagi ujinga,....unawaongelesha kithungu kwani uliwapeleka Shule?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…