ILALA = Ni kutokana na sauti za misikitini wakati huo -- Lai la la aila (sijui ni hivyo?)
SHAURIMOYO = Ilitokana na ujambazi uliokuwepo maeneo ya mitaa hiyo wakati huo. Watu wakawa wanasema inabidi uushauri moyo wako kabla ya kukatiza eneo hilo.
Nadhani mpaka sasa mtaa ule unaendeleza asili yake maana pale kwenye kona ya shauri moyo na nyerere ukizubaa tu unalizwa especial mida ya giza giza kisha wanatokomea kwenye miti ya relini au chini ya daraja.
Singida
Mitunduruni - Kulikuwa na miti ya mitunduru mingi
Kibaoni - Kulikuwa na kibao Karibu singida
Dodoma - idodomiya (tembo alidodomea sehemu ya kikuyu "shule ya mazengo")
Mnadani - kwasababu kulikuwa na mnada
Uhindini - kwa kuwa wanaoishi sehemu hiyo majority ni wahindi
Kilimani - kuna kilima kuelekea mlima wa mkalama
Kikuyu - Kwa sababu kuna miti mingi ya mikuyu
Mahemani - kwasababu kulikuwa na mahema enzi hizo
Tanga
Kwedikwazu - Kwa dikwazu mtu maarufu aliejulikana kwa jina la dikwazu
Majani mapana - asili yake ni mti ya mitiki
Mabanda ya papa linajieleza
Komesho - Chuo cha Commercial