Asili na Maana ya Jina/majina ya sehemu mbalimbali Tanzania

Mule ndani ya jengo la kamata kulikua na ofisi ya scandinavia na mpaka leo kuna basi zake....
Baada ya tamati ya KAMATA, kampuni ya mabasi ya Scandinavia iliparithi kama kituo chake kikuu Dar es Salaam. Wengine wakaanza kupaita Scandinavia. Lakini jina halikupiku lile la KAMATA. Na ikichagizwa na kupotea kwa mabasi ya Scandinavia sokoni.
 
Ilianzishwa katika misingi ya Ujamaa na wabadhirifu hawakuwa wanaadhibiwa. Lakini misingi yake ilikua mizuri sana. Ninakumbuka madereva walikua wanalala Mbeya Hoteli, airings Hoteli nk.
Ndio hivyo, Tragedy of the commons - Wikipedia . SU wakati ule walikuwa wakiita "Soma Ule".

Classmate mmoja, M.P.M., alipata kusema kusema Tanzania hatukuwa na mashirika ya umma. Yale yalikuwa mashirika ya serikali yaliyopewa jina la umma. Ingekuwa ni mashirika ya umma, mwananchi mmojammoja wangekuwa na hisa kwenye mashirika hayo.

Sky Eclat , falsafa ya Ujamaa naturally hufeli. Mbadala ni matumizi ya nguvu -- gulags, re-education camps, n.k.

Vitabu vya mwanamama Ayn Rand, japo vingine ni fictional, lakini vinaelezea falsafa ya soko huria ilivyo na manufaa. Pia inaelezea The Tyranny of the Majority kwamba ni detrimental to economic progress na prosperity. If you have the time, start with her book titled Atlas Shrugged. That book should be a required reading kwa watunga sera wetu wa uchumi na maendeleo.
 
Pale Barabara ya Msimbazi inapokutana na Barabara ya Nyerere, pamezoeleka kwa jina la "Kamata". Baadhi ya vijana, hawaelewi kwa nini panaitwa hivyo. Wengine mpaka wanajiuliza nani akamatwe?

Miaka ile ya zamani, serikali ilikusudia kujenga Ujamaa na Kujitegemea. Na kufikia ndoto hiyo, ililazimu kukata "mirija" ya "makupe" wanyonyaji wote, yaani "mabepari". Na hivyo serikali kuanzisha biashara mbalimbali ili kufikisha huduma karibu kabisa na wananchi.

Mojawapo ya kampuni hizo ilikuwa ni kampuni za mabasi za mikoa, na lile baba lao, Kampuni ya Mabasi ya Taifa (KAMATA).

Hiyo kampuni ya KAMATA ilikuwa na makao makuu yake pale kwenye jengo lililo makutano ya Msimbazi/Nyerere.

Ndio kisa cha eneo hilo kujulikana kama KAMATA.

Umenifahamu?
Wahadithie watoto wenzako stori hizo za vijiweni.
Mambo iko hivi.

Dar es salaam tokaenzi za Ukoloni kulikuwa na kampuni ya mabasi jijini ikiitwa DMT-Dar es salaam Motor Transport.
DMT ilikuwa kampuni ya waingereza toka 1947.
Mwaka 1967 DMT ikataifishwa na serikali na kutengenezwa kampuni mbili.

Kampuni hizo ni:

UDA- Usafiri Dar es salaam, kwa usafiri jijini, na
KAMATA- Kampuni ya Mabasi ya Taifa, kwa usafiri mikoani.

Kampuni hizi zilijaa matatizo makubwa ya uendeshaji Na hatimaye zote zilikufa na kubaki kwenye makaratasi.
Makao makuu ya UDA yalikuwa Kurasini na KAMATA, ni hapo Msimbazi / Nyerere Rd.
 
Classmate mmoja, M.P.M., alipata kusema kusema Tanzania hatukuwa na mashirika ya umma. Yale yalikuwa mashirika ya serikali yaliyopewa jina la umma. Ingekuwa ni mashirika ya umma, mwananchi mmojammoja wangekuwa na hisa kwenye mashirika hayo.
Wakati mashirika ya umma yanaanzishwa hakukuwepo soko la hisa na hivyo kuifanya Serikali kuwa na umiliki wa hisa kwa asilimia mia. Matokeo ya usanii huo ni kuwatajirisha viongozi waliopewa jukumu la kuyaendesha na kuyaacha mufilisi.

Leo hii tunapojaribu kutafakari yaliyotokea, tuelewe kuwa bado makosa yale yale yaliyofanyika enzi hizo bado yanaendelea kujirudia. Mifano kama ATCL, TRL, Shirika la Posta, Shirika la meli za taifa, Simu na mengine mengi tu, Serikali inayamiliki kwa asilimia mia.

Nadhani Serikali ingelitumia vema soko la hisa kwa kuoorodhesha makampuni na mashirika yote ya umma kwanza kisha, kuuza asilimia 20-40 ya hisa zake kwa wananchi na taasisi.. Nashindwa kuelewa ni kwa nini hili linashindikana wakati TBL na TCC wamefanikiwa.
 
Nadhani Serikali ingelitumia vema soko la hisa kwa kuoorodhesha makampuni na mashirika yote ya umma kwanza
Sikumbuki ni awamu ipi, lakini mojawapo ya awamu zilizopita ilipata kusema kwamba "si kazi ya serikali kufanya biashara." Kwa hiyo kuenlist mashirika yote DSE, kungefanya maendeleo yawe makubwa.
 
Kwa sana tu kaka, kuna watanzania wana hela za kutosha tu, zinatumika kwenye matanuzi hasa kwenye mabaa, mashirika haya yangeorodheshwa DSE watu wakahamasishwa kununua hisa, mtaji wa kutosha ungepatikana na wananchi walionunua hizo hisa wangewasimamia wakurugenzi kisawa sawa.
 
Wahadithie watoto wenzako stori hizo za vijiweni.
Mambo iko hivi.

Dar es salaam tokaenzi za Ukoloni kulikuwa na kampuni ya mabasi jijini ikiitwa DMT-Dar es salaa Motor Transport.
DMT ilikuwa kampuni ya waingereza toka 1947.
Mwaka 1967 DMT ikataifishwa na serikali na kutengenezwa kampuni mbili.Kampuni hizo ni:

UDA- Usafiri Dar es salaam, kwa usafiri jijini, na
KAMATA- Kampuni ya Mabasi ya Taifa, kwa usafiri mikoani.

Kampuni hizi zilijaa matatizo makubwa ya uendeshaji Na hatimaye zote zilikufa na kubaki kwenye makaratasi.
Makao makuu ya UDA yalikuwa Kurasini na KAMATA, ni hapo Msimbazi / Nyerere Rd.
Sawa kabisa kwamba asili ya UDA na KAMATA ni DMT. Lakini si sawa kwamba mwaka1967 ndipo zilizaliwa hizo kampuni tanzu mbili. Hilo lilitokea baadaye. Nitaeleza kidogo ninachokumbuka kuhusu DMT.

Baada ya DMT kutaifishwa, kampuni iliendelea kufanya biashara na jina hilo hilo la DMT na biashara yao ilikuwa mjini Dar tu. Vijana wafahamishwe pia kuwa kulikuwa na mabasi ya DMT ya gorofa kama ya London. Hiyo ndiyo asili ya wimbo wenye maneno "Heri ufe kwa kugongwa na basi la gorofa la kwenda Ilala. Usikiombee kifo cha mpenzi cha kugongwa na gari la 'tela' la kwenda Zambia".

Baada ya miaka kadhaa ya DMT kufanya biashara ya kusafirisha wakazi wa Dar kama shirika la Umma, wakaanzisha safari za kwenda mikoani wakiwa bado wakiitwa DMT. Walikuwa wakienda Morogoro, Tabora, Mwanza, Bukoba, Arusha, Musoma, n.k. Wakati kila basi la DMT la kwenda mikoani likiwa na madereva watatu (hata ya kwenda Morogoro) wakipokezana, Tanganyika Bus walikuwa wanatumia dereva mmoja tu kutoka Mwanza kuja Dar. Vivyo hivyo mabasi ya Teeteeko ya kutoka Dar kwenda nyanda za Kusini au Hood Bus kutoka Morogoro kwenda Dar au Iringa. Achilia mbali mabasi ya Wachaga ya kutoka Dar kwenda Moshi/Arusha. Wakati ratiba ya DMT ilikuwa watumie saa 23 kwa safari ya Dar-Tabora, Tanganyika Bus walikuwa wakitumia saa 24 kwa safari ya Dar-Mwanza. Ratiba za mabasi ya DMT ya kwenda mikoani zilikuwa hazifuatwi. Zama hizo mabasi yalikuwa yanaruhusiwa kusafiri usiku. Lakini ilikuwa kila basi la DMT likifika Singida 'linaharibika' na inabidi kulala hapo. Asubuhi basi wala halijashughulikiwa abiria mnaambiwa limepona mnaendelea na safari. Inasemekana madereva walikuwa na wasichana wao hapo ambao lazima wasimame kuwasalimia. Hayo ni baadhi ya matatizo yaliyofanya DMT ya Umma isifanye vizuri kibiashara.

Nauli ya Dar-Tabora ilikuwa Sh.49 ambapo kwa safari za jijini nauli ilikuwa ikibadilika kufuatana na wapi unakwenda, kima cha chini kikiwa Senti 25. Posta-Kurasini nauli ilikuwa Senti 55; Kariakoo-Ubungo Senti 60; Kariakoo-Chuo Kikuu Senti 65; Posta-Pugu Sekondari Senti 90. Baadaye wakaanzisha safari ndefu zaidi kama Kariakoo-Kibaha kwa Sh. 2.50 na wakawa wanaenda hadi TANITA, Kwa Mfipa, Kongowe, Kisarawe, nk.

DMT za mjini zilikuwa zikifanya kazi saa 24, ingawa kadiri usiku unavyokomaa, idadi ya mabasi inapungua. Kwa mfano kuanzia saa sita usiku linabakia basi moja tu la kuzunguka kutoka Temeke kwenda Chuo Kikuu kupitia Morogoro Road na linaendelea mpaka Mwenge na kurudi mjini kupitia Bagamoyo Road na Morocco.

Kufuatana na uhaba wa mabasi ya DMT, mabasi ya binafsi yakaanza kufanya kazi kwa kificho wakitoza Senti 50 bila kujali unapokwenda. Hivyo yakawa yakiitwa Thumuni-Thumuni. Trafiki walikuwa wakiyapiga vita na ndiyo maana walikuwa wakitoza kima kikubwa zaidi ili akishikwa ajione kwamba angalau ameshikwa kwa kuchuma kiasi kinachoeleweka.

Ni dhahiri mabasi ya mjini yalikuwa yakiingiza pato kubwa zaidi ya yale ya kwenda mikoani. Miaka ya sabini katikati ndipo biashara ikagawanywa: usafirishaji wa abiria jijini Dar ukaundiwa kampuni tanzu ya UDA na usafirishaji wa abiria kwenda mikoani ukaundiwa kampuni ya KAMATA, kila kampuni ikijitegemea. Mara baada ya UDA kuundwa, wakaleta mabasi ya Icarus yenye 'tela' ambayo yalikuwa yakichukua abiria karibu ya mia. Kituo kikiwa kimejaa abiria, Icarus ikija inazoa wote. Kampuni ya UDA walikuwa na bendi ya mziki, wakajiita Icarus Kumbakumba. Badiliko jingine waliloleta UDA mara baada ya kuundwa upya ni kuanzisha tikiti za msimu. Unanunua tikiti ya Sh.60 ukaitumia kwa mwezi mzima kwa njia moja k.m. Kariakoo-Ubungo. Ukiwa kwenye njia yako, hata usafiri mara 50 kwa siku hutozwi zaidi. Utatozwa unapoingia njia nyingine tu. Mbali na hiyo, unaweza kununua tikiti ya msimu ya Sh 85 kwenda popote UDA inapokwenda kwa mwezi mzima.

Mwishoni mwa miaka ya sabini nauli zilikuwa zimepanda karibu ya mara tatu ya zilivyokuwa mwanzoni. Mabasi ya binafsi nayo yakaongeza kima kufikia Sh.5 po pote uendapo, ambayo ndiyo ilikuwa thamani ya Dola ya Marekani siku hizo. Hiyo ndiyo asili ya jina la Daladala. Nauli hiyo ilikuwa kubwa sana lakini watu walikuwa wakiyapanda tu kwa ajili ya uhaba wa UDA. Trafiki walipambana sana nayo mpaka Waziri Mkuu, Sokoine, alipoingilia kati na kuyahalalisha.

Hicho ndicho kifupi cha historia ya UDA ninachokumbuka.
 
Du brother umenikumbusha mbali sana na "Kifo cha penzi kibaya".... wimbo uloimbwa na Orchestra Quilado.
Na asante kwa historia iliyo ya kina maana miaka ya 60s nikiishi Temeke.
Nikuulize tu, ulikuwa unafanya kazi UDA?
 
Hapana mkuu sijafanya UDA. nyakati hizo ndiyo namaliza sekondari kabla ya kwenda Form 5 na baadaye Chuo Kikuu.
 
Mule ndani ya jengo la kamata kulikua na ofisi ya scandinavia na mpaka leo kuna basi zake....
... baada ya sera za chama cha mafisadi kushindwa walikuja kuuza mali za umma ovyo na nyingine kujimilikisha. Ndio essence ya hao Scandinavia kuuziwa kifisadi yadi ile ya KAMATA kama walivyouza mali nyingine nyingi za watanzania.
 
Asante sana @Ng’wanamalundi kwa kurejesha kumbukumbumbu mujarabu.
 
Sawa kabisa kwamba asili ya UDA na KAMATA ni DMT. Lakini si sawa kwamba mwaka1967 ndipo zilizaliwa hizo kampuni tanzu mbili. Hilo lilitokea baadaye. Nitaeleza kidogo ninachokumbuka kuhusu DMT.

Baada ya DMT kutaifishwa, kampuni iliendelea kufanya biashara na jina hilo hilo la DMT na biashara yao ilikuwa mjini Dar tu. Vijana wafahamishwe pia kuwa kulikuwa na mabasi ya DMT ya gorofa kama ya London. Hiyo ndiyo asili ya wimbo wenye maneno "Heri ufe kwa kugongwa na basi la gorofa la kwenda Ilala. Usikiombee kifo cha mpenzi cha kugongwa na gari la 'tela' la kwenda Zambia".

Baada ya miaka kadhaa ya DMT kufanya biashara ya kusafirisha wakazi wa Dar kama shirika la Umma, wakaanzisha safari za kwenda mikoani wakiwa bado wakiitwa DMT. Walikuwa wakienda Morogoro, Tabora, Mwanza, Bukoba, Arusha, Musoma, n.k. Wakati kila basi la DMT la kwenda mikoani likiwa na madereva watatu (hata ya kwenda Morogoro) wakipokezana, Tanganyika Bus walikuwa wanatumia dereva mmoja tu kutoka Mwanza kuja Dar. Vivyo hivyo mabasi ya Teeteeko ya kutoka Dar kwenda nyanda za Kusini au Hood Bus kutoka Morogoro kwenda Dar au Iringa. Achilia mbali mabasi ya Wachaga ya kutoka Dar kwenda Moshi/Arusha. Wakati ratiba ya DMT ilikuwa watumie saa 23 kwa safari ya Dar-Tabora, Tanganyika Bus walikuwa wakitumia saa 24 kwa safari ya Dar-Mwanza. Ratiba za mabasi ya DMT ya kwenda mikoani zilikuwa hazifuatwi. Zama hizo mabasi yalikuwa yanaruhusiwa kusafiri usiku. Lakini ilikuwa kila basi la DMT likifika Singida 'linaharibika' na inabidi kulala hapo. Asubuhi basi wala halijashughulikiwa abiria mnaambiwa limepona mnaendelea na safari. Inasemekana madereva walikuwa na wasichana wao hapo ambao lazima wasimame kuwasalimia. Hayo ni baadhi ya matatizo yaliyofanya DMT ya Umma isifanye vizuri kibiashara.

Nauli ya Dar-Tabora ilikuwa Sh.49 ambapo kwa safari za jijini nauli ilikuwa ikibadilika kufuatana na wapi unakwenda, kima cha chini kikiwa Senti 25. Posta-Kurasini nauli ilikuwa Senti 55; Kariakoo-Ubungo Senti 60; Kariakoo-Chuo Kikuu Senti 65; Posta-Pugu Sekondari Senti 90. Baadaye wakaanzisha safari ndefu zaidi kama Kariakoo-Kibaha kwa Sh. 2.50 na wakawa wanaenda hadi TANITA, Kwa Mfipa, Kongowe, Kisarawe, nk.

DMT za mjini zilikuwa zikifanya kazi saa 24, ingawa kadiri usiku unavyokomaa, idadi ya mabasi inapungua. Kwa mfano kuanzia saa sita usiku linabakia basi moja tu la kuzunguka kutoka Temeke kwenda Chuo Kikuu kupitia Morogoro Road na linaendelea mpaka Mwenge na kurudi mjini kupitia Bagamoyo Road na Morocco.

Kufuatana na uhaba wa mabasi ya DMT, mabasi ya binafsi yakaanza kufanya kazi kwa kificho wakitoza Senti 50 bila kujali unapokwenda. Hivyo yakawa yakiitwa Thumuni-Thumuni. Trafiki walikuwa wakiyapiga vita na ndiyo maana walikuwa wakitoza kima kikubwa zaidi ili akishikwa ajione kwamba angalau ameshikwa kwa kuchuma kiasi kinachoeleweka.

Ni dhahiri mabasi ya mjini yalikuwa yakiingiza pato kubwa zaidi ya yale ya kwenda mikoani. Miaka ya sabini katikati ndipo biashara ikagawanywa: usafirishaji wa abiria jijini Dar ukaundiwa kampuni tanzu ya UDA na usafirishaji wa abiria kwenda mikoani ukaundiwa kampuni ya KAMATA, kila kampuni ikijitegemea. Mara baada ya UDA kuundwa, wakaleta mabasi ya Icarus yenye 'tela' ambayo yalikuwa yakichukua abiria karibu ya mia. Kituo kikiwa kimejaa abiria, Icarus ikija inazoa wote. Kampuni ya UDA walikuwa na bendi ya mziki, wakajiita Icarus Kumbakumba. Badiliko jingine waliloleta UDA mara baada ya kuundwa upya ni kuanzisha tikiti za msimu. Unanunua tikiti ya Sh.60 ukaitumia kwa mwezi mzima kwa njia moja k.m. Kariakoo-Ubungo. Ukiwa kwenye njia yako, hata usafiri mara 50 kwa siku hutozwi zaidi. Utatozwa unapoingia njia nyingine tu. Mbali na hiyo, unaweza kununua tikiti ya msimu ya Sh 85 kwenda popote UDA inapokwenda kwa mwezi mzima.

Mwishoni mwa miaka ya sabini nauli zilikuwa zimepanda karibu ya mara tatu ya zilivyokuwa mwanzoni. Mabasi ya binafsi nayo yakaongeza kima kufikia Sh.5 po pote uendapo, ambayo ndiyo ilikuwa thamani ya Dola ya Marekani siku hizo. Hiyo ndiyo asili ya jina la Daladala. Nauli hiyo ilikuwa kubwa sana lakini watu walikuwa wakiyapanda tu kwa ajili ya uhaba wa UDA. Trafiki walipambana sana nayo mpaka Waziri Mkuu, Sokoine, alipoingilia kati na kuyahalalisha.

Hicho ndicho kifupi cha historia ya UDA ninachokumbuka.

Nasoma uzi wako naona kama usafiri wa mjini Dsm ulikuwa wa ufanisi sana mithili au kufanana kabisa na standard ya nchi zilizoendelea za Ulaya na Marekani ya Kaskazini.

Kumbe biashara ya ushindani ilikuwepo hata kipindi cha awamu ya Mwalimu Nyerere, lakini nikisoma Vitu ktk Google inaonekana kuwa kila kitu kilikuwa kinaendeshwa na serikali kuu chini ya sera ya ujamaa kumbe siyo kweli kulikuwapo makampuni ya binafsi pia.

Shukrani kwa kutupatia historia ya kweli enzi zenu hizo kuhusu upande wa sekta ya biashara ya usafirishaji chini ya utawala wa Mwalimu Nyerere , baba wa Taifa.
 
If you have the time, start with her book titled Atlas Shrugged. That book should be a required reading kwa watunga sera wetu wa uchumi na maendeleo.
Asante Mkuu. Naona zipo version tatu ya kwanza ni ya 1971, ya pili ni ya 2005 na ya tatu ni ya 2010. Ni some ipi ?
 
Back
Top Bottom