Asili na Maana ya Jina/majina ya sehemu mbalimbali Tanzania

Asili na Maana ya Jina/majina ya sehemu mbalimbali Tanzania

Asante Mkuu. Naona zipo version tatu ya kwanza ni ya 1971, ya pili ni ya 2005 na ya tatu ni ya 2010. Ni some ipi ?
Pamoja. Kitabu kilichapishwa mara ya kwanza mwaka 1957. Hizo zingine zitakuwa ni matoleo maalum. Stori itakuwa bado ni ileile.
 
Pale Barabara ya Msimbazi inapokutana na Barabara ya Nyerere, pamezoeleka kwa jina la "Kamata". Baadhi ya vijana, hawaelewi kwa nini panaitwa hivyo. Wengine mpaka wanajiuliza nani akamatwe?

Miaka ile ya zamani, serikali ilikusudia kujenga Ujamaa na Kujitegemea. Na kufikia ndoto hiyo, ililazimu kukata "mirija" ya "makupe" wanyonyaji wote, yaani "mabepari". Na hivyo serikali kuanzisha biashara mbalimbali ili kufikisha huduma karibu kabisa na wananchi.

Mojawapo ya kampuni hizo ilikuwa ni kampuni za mabasi za mikoa, na lile baba lao, Kampuni ya Mabasi ya Taifa (KAMATA).

Hiyo kampuni ya KAMATA ilikuwa na makao makuu yake pale kwenye jengo lililo makutano ya Msimbazi/Nyerere.

Ndio kisa cha eneo hilo kujulikana kama KAMATA.

Umenifahamu?
Sawa tumekumanya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pamoja. Kitabu kilichapishwa mara ya kwanza mwaka 1957. Hizo zingine zitakuwa ni matoleo maalum. Stori itakuwa bado ni ileile.
Asante sana. Ngoja nianze na 1971 iliyokaribu na original (1957).
 
Asante Mkuu. Naona zipo version tatu ya kwanza ni ya 1971, ya pili ni ya 2005 na ya tatu ni ya 2010. Ni some ipi ?
Hicho kitabu, japo cha hadithi, ni cha kifalsafa. Kama dibaji ya falsafa ya Ayn Rand, video ifuatayo inaweza kuwa ya manufaa.

More introduction to Objectivist Philosophy put forward by Ayn Rand.

Asante sana nimejifunza kitu.

From understanding the reality around us and to reason based on the knowledge we have this brings us to the selfishness or egoism when we consider the ethics issues.

At that point we may consider the way of living in the society (politics), which include capitalism, where sacrifice to others is forbidden! Here, the presenters 'demonizes' the communalism/socialism by citing the example of " You can not exchange the throat with your colleague" in capitalism but only trading values can work. For that matter, this mark the aestheticism, i.e. value oriented matters. All of these sums up to the 'Objectivism'.

Mambo mengi mazuri ameyasema. Kwa kuwa ni mara yangu ya kwanza kuhudhuria lecture ya namna hii. Nitairudia tena.

Asante sana kwa mara nyingine.
===
Mkuu nimeendelea kumfuatilia mwandishi wa kitabu cha "Atlas shrugged". Nimefanikiwa kupata speech yake ya mwisho ya Nov 21, 1981 aliyoitoa kwenye warsha ya wafanyabiashara huko New Orleans. Warsha hiyo ilidhaminiwa na the National Committee for Monetary Reform. Fuatilia link hapa chini.

Nimefuatilia speech yake mpaka dakika ya 11 ya clip hii.

Objectively: Mama alisema ukweli juu ya msingi wa uimara na ukuawaji kimapato wa wafanyabiashara
kuwa ni kutokujitolea kwa ajili ya wengine. Na akasisitiza wakijitolea/jitoa muhanga kwa ajili ya
wengine watondolewa kwenye biashara mara moja maana hawatapata faida.

Subjectively: Nimeshtushwa kwa namna US ilivyofanikiwa kumrubuni raia wa iliyokuwa Soviet kiasi cha
kumfanya nguli wa kupiga propaganda za kuinua 'u-capitalism' kwa ari ya hali ya juu.
 
Pale Barabara ya Msimbazi inapokutana na Barabara ya Nyerere, pamezoeleka kwa jina la "Kamata". Baadhi ya vijana, hawaelewi kwa nini panaitwa hivyo. Wengine mpaka wanajiuliza nani akamatwe?

Miaka ile ya zamani, serikali ilikusudia kujenga Ujamaa na Kujitegemea. Na kufikia ndoto hiyo, ililazimu kukata "mirija" ya "makupe" wanyonyaji wote, yaani "mabepari". Na hivyo serikali kuanzisha biashara mbalimbali ili kufikisha huduma karibu kabisa na wananchi.

Mojawapo ya kampuni hizo ilikuwa ni kampuni za mabasi za mikoa, na lile baba lao, Kampuni ya Mabasi ya Taifa (KAMATA).

Hiyo kampuni ya KAMATA ilikuwa na makao makuu yake pale kwenye jengo lililo makutano ya Msimbazi/Nyerere.

Ndio kisa cha eneo hilo kujulikana kama KAMATA.

Umenifahamu?
Ila ndoto za wazee wetu nazo zilikuwa na walakini,
Yaani walitaka mabasi yote yaendayo mikoani kama shabiby,AbC,Kimbinyiko,Flexxer,maning nice,hamanju,na mengineyo yote yamilikiwe na Serikali?
Hebu piga picha kama mabasi yote pale nyegezi stand,Mbeya stand,Kahama stand,Singida stand,msamvu,mpaka mbezi stand yawe yapo chini ya mamlaka ya Serikali?
Kama Tanesco na ttcl zimewashinda,wangeweza huu mziki?!!!!
 
Nadhani huyu Mama Iran/Ayn anahitaji uzi wake maalum. Nina imani Mkuu Kiranga atakuwa na madini mengi juu yake kwani accidentally rather coincidentally wako imani moja ya kutokumuamini Mungu. Ha ha haaa!
===

Subjectively: Nimeshtushwa kwa namna US ilivyofanikiwa kumrubuni raia wa iliyokuwa Soviet kiasa cha
kumfanya nguli wa kupiga propaganda za kuinua 'u-capitalism' kwa ari ya hali ya juu.

Asante kushukuru.

Kwa nini mzigo wa kuwa mbepari unamnyang'anya Ayn mwenyewe na kuwatwika Wamarekani? Yeye mwenyewe kwa utashi wake, kaamua hayo aliyoyaamua.

Huyu mama amekuwa credited kuanzisha falsafa nzima ("objectivism"). Binadamu huwa tunazo falsafa zinazoongoza maisha yetu. Mama Rand kaongezea nyingine tunayoweza kuijadili na kuitafakari. Mama Rand ni mashuhuri sana miongoni mwa wahafidhina Marekani, japo wao wengi ni waamini wa imani kumhusu Mwenyezi Mungu. Kwa hiyo siyo lazima kukubaliana naye na falsafa nzima, ili kuweza kukubaliana na yale unayoyaona yana mantiki. Mawazo hayapigwi rungu -- JK.

Hivyo, falsafa ("Kupenda tu kufahamu") inatutaka tusikilize hata yale tusiyokubaliana nayo. Yakiwapo ya kuyapinga, tuyapinge kwa hoja kinzani.

Kwa kawaida, falsafa hushughulika na maswali magumu kuhusu maisha ya binadamu.
 
Siasa (Politics), Maadili (Ethics) yote hayo ni matawi yatokanayo na shina la falsafa. Kadhalika tunajuaje kwamba tunajua (Epistemology) na Namna ipi tunafikia kujua (Ontology), yana matokeo kwenye maisha yetu ya kila siku., n.k.
 
Pale Barabara ya Msimbazi inapokutana na Barabara ya Nyerere, pamezoeleka kwa jina la "Kamata". Baadhi ya vijana, hawaelewi kwa nini panaitwa hivyo. Wengine mpaka wanajiuliza nani akamatwe?

Miaka ile ya zamani, serikali ilikusudia kujenga Ujamaa na Kujitegemea. Na kufikia ndoto hiyo, ililazimu kukata "mirija" ya "makupe" wanyonyaji wote, yaani "mabepari". Na hivyo serikali kuanzisha biashara mbalimbali ili kufikisha huduma karibu kabisa na wananchi.

Mojawapo ya kampuni hizo ilikuwa ni kampuni za mabasi za mikoa, na lile baba lao, Kampuni ya Mabasi ya Taifa (KAMATA).

Hiyo kampuni ya KAMATA ilikuwa na makao makuu yake pale kwenye jengo lililo makutano ya Msimbazi/Nyerere.

Ndio kisa cha eneo hilo kujulikana kama KAMATA.

Umenifahamu?
KAMATA "haikuanzishwa" na serikali kwa ajili ya kukata mirija kama unavyosema bali ilitokana na kuvunjwa ka kampuni ya mabasi ya Dar es Salaam Motor Transport (DMT) iliyotaifishwa na kuwa makampuni mawili ya Kampuni ya mabasi ya Taifa (KAMATA) ambayo ilikuwa imepewa njia za bara tu, na kampuni ya Usafiri Dar es Salaam (UDA) kuwa ya kusimamia njia za Dar es Salaam tu. KAMATA iliendelea kutumia rangi za DMT na hata nembo yake zilikuwa karibvu sawa, D ikiwakilishwa na KA, M ikiwakilishwa na MA na T ikiwakilishwa na TA. Ila UDA yenyewe ilikuwa na nembo na rangi zake tofauti kabisa
 
ilitokana na kuvunjwa ka kampuni ya mabasi ya Dar es Salaam Motor Transport (DMT) iliyotaifishwa
Ndio kuanzisha kwenyewe. Kwa kuvunja kilichokuwapo. Mf., serikali ilianzisha TBC kwa kuvunja RTD...

iliyotaifishwa na kuwa makampuni mawili ya Kampuni ya mabasi ya Taifa (KAMATA) ambayo ilikuwa imepewa njia za bara tu, na kampuni ya Usafiri Dar es Salaam (UDA)
Kutaifishwa ndio kukatwa mirija kwenyewe kulikokusudiwa, kwani 'makupe' 'mabepari' hayangeweza tena kunyonya faida itokanayo na kampuni iliyokuwa yao. Faida yote ingeenda kwa taifa zima 😳 kwa manufaa ya wote...
 
Pale Barabara ya Msimbazi inapokutana na Barabara ya Nyerere, pamezoeleka kwa jina la "Kamata". Baadhi ya vijana, hawaelewi kwa nini panaitwa hivyo. Wengine mpaka wanajiuliza nani akamatwe?

Miaka ile ya zamani, serikali ilikusudia kujenga Ujamaa na Kujitegemea. Na kufikia ndoto hiyo, ililazimu kukata "mirija" ya "makupe" wanyonyaji wote, yaani "mabepari". Na hivyo serikali kuanzisha biashara mbalimbali ili kufikisha huduma karibu kabisa na wananchi.

Mojawapo ya kampuni hizo ilikuwa ni kampuni za mabasi za mikoa, na lile baba lao, Kampuni ya Mabasi ya Taifa (KAMATA).

Hiyo kampuni ya KAMATA ilikuwa na makao makuu yake pale kwenye jengo lililo makutano ya Msimbazi/Nyerere.

Ndio kisa cha eneo hilo kujulikana kama KAMATA.

Umenifahamu?
Hilo jina silipendagi,ababu pale kamata kama unaelekea airport from towb lazima ukamatwe kwenye foleni
 
Asante sana. Ngoja nianze na 1971 iliyokaribu na original (1957).
Angalizo: Mwandishi ametumia mda mwingi kujenga wahusika wake. Hali kadhalika, kuandaa muktadha wa hadithi yake. Kwa hiyo unaweza kukuta msuli kidogo unahitajika mwanzoni kuupata muktadha. Kadhalika, masuala ya mahusiano nayo kayaweka kwenye hadithi, yanaweza kuwa ni tangent from the story. Lakini ukiondoa hayo, kitabu chake ukikisoma mpaka mwisho utaweza kubaini ni kwa nini kimekuwa mashuhuri hata miaka zaidi ya sitini baadaye...

Na utaweza kuona kwa nini UDA na KAMATA zilifikia masaibu yaliyozikuta. Na kuona tokea mbali matokeo ya utitiri wa "wadhibiti" na bei zao "elekezi" katika sekta anuai.
 
Nikuulize tu, ulikuwa unafanya kazi UDA?
Utani kidogo: Atakubali kwa sababu hatahusishwa na wale waliokuwa wanalazimisha mabasi ya mikoani yafie Singida, lakini asubuhi yanapona bila kutengenezwa na safari inaendelea.
===
Nje ya mada. Mkuu, kwa sababu umeshudia vizazi vya wanamziki wetu kuanzia miaka ya sitini mpaka mwanzoni mwa themanini na hawa wa kuanzia miaka 90 mpaka sasa hivi. Je. Ni siri gani walikuwa nayo hawa kizazi cha wali cha kupiga mziki unaovutia mpaka sasa ( Kidawa mfano) kuanzia ala za mziki mpaka sauti za waimbaji wakati wa kizazi cha sasa muziki ukiendelea kuwa mzuri masikioni zaidi ya miaka 15 mwanamziki anashukuru?
 
Back
Top Bottom