Jee ni kweli Mohamed Iqbal Dar, mwenye asili ya kihindi, aliyekuwa akiishi Tanga, mnamo mwaka 1964 ndiye aliipa nchi yetu jina zuri la "Tanzania"
Kama ni kweli huyu mtu yuko wapi kwa sasa? Na serikali yetu inaweka kumbu-kumbu gani za kihistoria kwa huyu mtu kwa vizazi vijavyo? ili vipate kujuwa nani aliipa nchi hii jina lake.Au mchango wake hauna maana yeyote, ni jina tuu, kwa hiyo potelea mbali Nadhani hata vizazi vya sasa, ambavyo havipo mbali 1964 hatuna uhakika na ndio maana tunauliza.Naomba anaejuwa kuhusu hilo atuelimishe.ili yasitokee kama ya Ngosha. Wa Nembo ya aTaifa />================/UNAPOTAJA historia ya nchi Tanzania, ni dhahiri kwamba hutaacha kutaja majina ya wapigania uhuru na viongozi mbalimbali walioiongoza tangu enzi za ukoloni, hadi kupata uhuru
Hata hivyo, katika kila historia ya taifa lolote iliyojengwa, kuna watu waliofanikisha historia hiyo, lakini kwa sababu moja au nyingine, michango ya baadhi yao imesahaulika na pengine kutotajwa kabisa kwenye historia hizo.
Wengi wa Watanzania tunafahamu kuwa jina la nchi yetu Tanzania, limetokana na majina ya nchi mbili zilizoungana na kuwa moja ambazo ni Tanganyika na Zanzibar. Hivi ndivyo tulivyofundishwa shuleni.
Wengine wanaamini kuwa Rais wa kwanza na muasisi wa taifa hili, Hayati Mwalimu Julius Nyerere ndiye aliyebuni jina la Tanzania.
Lakini ukweli ni kwamba, jina la Tanzania lilibuniwa na mmoja wa wananchi walioshiriki mchakato wa kutafuta jina la nchi hii, baadaya muungano wa Tanganyika na Zanzibar mwaka 1964.
Mohammed Iqbal Dar ndiye aliyebuni jina la Tanzania, wakati huo akiwa na umri wa miaka 18 akiwa mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Mzumbe.
Ilikuwaje?
"Nilikuwa maktaba najisomea, nilishika gazeti la Daily News, wakati huo likiitwa The Standard, ndipo nikaona tangazo hilo," anaeleza Dar alivyopata hamasa na kuongeza
Siku hiyo hiyo, nikafanya majaribio ya kutafuta jina bila hata ya kuishirikisha familia yangu. Nilichuka karatasi na kalamu, lakini kabla sijaanza kufanya chochote, nilimwomba Mungu aniwezeshe kwa maana naamini Mungu, ndiye kila kitu wakati wa kufanya jambo lolote."
Kwa hiyo kwenye ile karatasi nikaandika Tanganyika na Zanzibar kisha, nikaandika majina yangu mawili; Iqbal na Ahmadiya," anasema Dar na kufafanua kuwa Iqbal ni jina lake na jina la ubini na Ahmadiyya ndiyo dhehebu lake.
Kupata jina Tanzania
Akisimulia alivyopata jina Tanzania, anasema kuwa ilimchukua dakika tano tu kufikiria na kulipata jina hilo.Nilichukua Tan kutoka kwenye Tanganyika na kuongeza Zan kutoka kwenye Zanzibar na kupata Tanzan, niliona halitimii vizuri,"anasimulia Dar.
Anabainisha kuwa baadaye alifikiria na kugundua kuwa majina mengi ya nchi za Afrika yanaishia na mfano akitoa mfano wa Ethiopia, Gambia, Tunisia, Nigeria, Algeria, Somalia, Zambia, Namibia na kwamba baada ya kubaini hilo aliamua kuongezea herufi hizo mbili na kupata jina Tanzania.
Nilituma maombi yangu katika shindano hilo, bila kumwambia mtu yeyote nyumbani," anasema Dar. Baada ya muda mfupi baba yake, mzee Tufail Ahmad Dar, alipokea barua kutoka Wizara ya Habari na Utalii (wakati huo), ambapo ndani yake kulikuwa na ujumbe wa pongezi ya kwamba kijana wake ameshinda katika shindano hilo.
"Wakati naandika, sikuwa na matumaini kama nitashinda kwa kuwa shindano hilo lilikua wazi kwa watu mbalimbali, hivyo sikuwa na tarajio lolote kama ningeshinda, Jioni wakati narudi nyumbani, baba mzazi alinifungulia mlango wakati si kawaida yake kwani mama ndiye alikuwa akinifungulia siku zote, hapo nikajua kuna kitu hakipo sawa. Lakini, nilikaribishwa na tabasamu la baba, pamoja na pongezi nyingi, nilifurahi sana," anaeleza.
Ushuri:
Ni vyema serikali Iikaweka kumbumkumbu mapema ,
Kuzuia kila mtu kuibuka na madai Kwa muhimu .
Kama ni huyu au ni mwingine ????.
Chanzo: Jamii Forum