Makubwa, kwa nini taifa limemsahau??
Mohammed Iqbal Dar (picha hapo juu) ndiye aliyebuni jina la Tanzania, wakati huo akiwa na umri wa miaka 18 akiwa mwanafunzi wa Shule ya Sekondari. Mohammed anasema alikuwa Maktaba akijisoma gazeti la Tanganyika Standard, siku hizi Daily News, akaona Tangazo linasema Muungano wa Tanganyika na Zanzibar unafahamika kama Republic of Tanganyika and Zanzibar jina likaonekana refu sana kwa hiyo Wananchi wote wakaombwa Washiriki kwenye shindano la Kupendekeza jina moja litakalo zitaja nchi zote mbili yaani Tanganyika na Zanzibar Mohammed Iqbal Dar anasema aliamua kuingia kwenye Shindano na hivi ndivyo alianza Safari ya Kubuni Jina la Muungano.
Kwanza anasema alichukua karatasi akaandika Bismillah Raahman Rahimu hii ni kutokana na Imani yake na baada ya hapo akaandika jina la
Tanganyika baada ya hapo akaandika
Zanzibar halafu akaandika jina lake
Iqbal halafu akaandika jina la Jumuiya yake ya
Ahmadiya baada ya Hapo akamrudia tena Mwenyezi Mungu akamwomba amsaidie ili apate jina zuri kutoka katika majina hayo aliyokuwa ameyaandika. Baada ya hapo Mohammed Iqbal Dar alichukua herufi tatu kutoka Tanganyika yaani
TAN na kwa upande wa Zanzibar akachukua Herufi tatu za Mwanzo
ZAN ukiunganisha unapata
TANZAN alivyoona hivyo akachukua
I herufi ya kwanza katika jina lake la Iqbal na akachukua
A kutoka jina la dini yake yaani Ahmadiyya kwa maana hiyo ukiongeza herufi hizi mbili
I na
Akwenye
TANZAN unapata jina kamili
TANZANIA akalisoma jina akaliona ni zuri lakini akajiridhisha pia kwamba akiongeza herufi hizo za
I na
A kwenye
TANZAN italeta maana kwakuwa nchi nyingi za Afrika zinaishia na
IA, mfano
EthiopIA,
ZambIA, NigerIA, TunisIA, SomalIA, GambIA, NamibIA, LiberIA, MauritanIA alivyoona hivyo akaamua apendekeze kuwa jina
TANZANIA ndio litumike kuwakilisha nnchi hizi mbili yaani Tanganyika na Zanzibar kwa maana hiyo jina
TANZANIA limezaliwa kutoka majina manne majina hayo ni
Tanganyika, Zanzibar, Iqbal na
Ahmadiyya.
Mohammed Iqbal Dar baada ya kupata jina hilo akalituma jina hilo kwenye kamati ya kuratibu Shindano. Baada ya Muda mwingi kupita baba yake na Mohammed Iqbal Dar alipokea barua nzito kutoka Serikalini akijulishwa kuwa alikuwa ni mmoja ya wabunifu 16 walioshinda jumla ya Tshs 200 na mgao wake ilikuwaTshs 12.50 na alilipwa kwa hundi zama hizo (1964).