sijui kama itadumu ....bado ina uhai kidogo sana siku si nyingi kila mtu na lwake.....nchi mbili zitazaliwa upya na moja itazaliwa kwa mara ya kwanzajamaa ni jembe jina tamuuu! Idumu tanzania na itadumu.....uamsho!
majina ya asili yatarejea baada ya kuvunjika muungano usihofu ndugumatatizo yetu yanaanzia mbali aisee, yaani nchi tunamoishi haina hata jina bali lilibuniwa na mtu wa kuibuka tu!!!
Ama kweli.
Katika misemo ya kwetu hapa kuna mmoja unasema kuwa daima jina lina reflect mwenye nalo (eibala libi lita nyinalyo). Mbona wenzetu wna majina ya asili zao mfano kenya, uganda, malawi/nyasa, rwanda, burundi na hata congo walilirejesha kutoka zaire.
ni kweli hili jina halina uhai mrefu kutoka sasaanataka watanzania wathamini vpi mchango wake..? Yeye anaishi huko uk.. Halafu alilipwa kwa kazi aliofanya.. Na isitoshe muda ci mrefu jina lenyewe la tanzania litakufa..
sijui kama itadumu ....bado ina uhai kidogo sana siku si nyingi kila mtu na lwake.....nchi mbili zitazaliwa upya na moja itazaliwa kwa mara ya kwanza
ni kweli hili jina halina uhai mrefu kutoka sasa
lazima lirudiLitarudi Tanganyika mkuu..
Mwaka 1964, wakati nipo darasa la 8, nilisoma gazeti la the Standard na kulikuwa Shindano hili la kulipa jina nchi yetu. Wakati huo nchi yetu ilikuwa inaitwa the United Republic of Tanganyika & Zanzibar. Wakati ule, shuleni tulikuwa tunasoma jiografia ya Australia na nakumbuka kisiwa cha Tasmania. Hii ilinipa hint ya jina la Tanzania. Mimi niliandika barua wizara ya Habari. Nakumbuka kupokea hundi ya Sh. 12.50 ikiwa ni share yangu ya kuipa jina Tanzania.
Maelezo katika barua ya Katibu Mkuu ilisema: Kwa sababu kulikuwa washindi 16, kwa hiyo hizo zawadi ya Sh. 200 itagawiwa miongoni mwa washindi. Pia, barua hiyo iliniambia kwamba jina hasa lililokubaliwa ni United Republic of Tanzania and sio Tanzania, kama nilivyoandika mimi.
Nakumbuka pia kwamba gazeti la September 1, 1964 au October 1, 1964 ilikuwa na headline, " From today, we are Tanzanians"
Huyo Mohamed Iqbal kama ni katika watu 16, basi anaweza kukubaliwa. Lakini kama anasema ni peke yake aliyechagua jina hili, basi ni mwongo. Best solution ni kwa Wizara ya Habari kupekua file zao na kujua ukweli. I am pleased to be part of history of Tanzania. Ikiwa wengi katika hao 16 walikuwa watu wazima mwaka 1964, basi wengi watakuwa wameshaaga dunia na itakuwa mushkeli kujitokeza. Mimi wakati huo nilikuwa kijana wa miaka 13 lakini nilikuwa na bahati kusoma gazeti la kiingereza kwa sababu ya baba yangu, ambaye alikuwa anapenda sana kusoma magezeti.
Asili yangu ni kihindi na nilisoma Chuo cha Sokoine 1974. Sasa hivi nipo Marekani na imekuwa bahati tu kusoma forum hiyo kwa sababu ya mambo ya Lowasa.
Ahsante,
Mustafa Yusufali Pirmohamed
muungano ukivunjika nchi mbili zinarudi katika uso wa dunia nazo ni TANGANYIKA NA ZANZIBAR baada ya hapo Zanzibar itagawanyika na kupata Zanzibar Republic and pemba republic maana ndicho wanachokitafuta uamshoKwa kweli kwa jinsi UAMSHO ilivyo ikalia vibaya..haina siku nyingi, Juzi nilimsikia alijificha na kuibuka kuwa alikamatwa na kuchapwa bakora na polisi anasema mpaka tone la damu ya mwisho lazima visiwa vijitawale..!
pemba wanataka kujitengaHongera kaka. Sisi wenzako wakati huo hata kuzaliwa ilikuwa bado. Kwa bahati mbaya jina Tanzania linatishiwa kutoweka pia kutokana na Zanzibar kutaka kujitenga
muungano ukivunjika nchi mbili zinarudi katika uso wa dunia nazo ni TANGANYIKA NA ZANZIBAR baada ya hapo Zanzibar itagawanyika na kupata Zanzibar Republic and pemba republic maana ndicho wanachokitafuta uamsho
hili swala mbona liko wazi sana wapemba walio wengi wanataka muungano uvunjike na waunguja wengi wanataka muungano uendelee...uamsho walichoma maskani za ccm(OFISI) na wala sio za cuf kwa nini?kwa sababu ccm haitaki muungano uvunjike na chama hiki kinaungwa mkono na waunguja zaidi kuliko wapemba wanaounga mkono zaidi cuf ...ukitaka kujua waunguja na wapemba wanatofautiana tembelea mtandao wa MZALENDO NET HUKO wanatukanana mpaka basiBwana Mpalu, Nyerere aliwahi kusema watu wanapata jeuri ya kujiita mimi ni Mzanzibari na yeye ni Mtanganyika kwa sababu wako ndani ya Muungano, ukivunjika muungaano wataaanza mimi Mpemba na yeye Muunguja, na kwa jinsi UAMSHO wa kina Mohammed Said na wenzie wanvyoutaka watakuja juta kwanini walivunja muungano! ngoja tuone...TIME SHALL TELL>>>>>>>.
Mohamed Iqbal Dar kwa mujibu wa gazeti la mwananchi la jumapili wiki hii.Wana jamvi naomba mnijuze aliyebuni jina la TANGANYIKA ni nani?
Mohamed Iqbal Dar kwa mujibu wa gazeti la mwananchi la jumapili wiki hii.
Sio siri kuna hoja anataka kujenga, kama walikuwa 16 walioshinda wakagawana hundi, hivyo sio peke yake aliyetunga hilo jina, wengine pia waliweza kutoa wazo kuwa iitwe tanzania, je hao wengine ndio wanaoheshimiwa kuliko yeye au yeye anataka heshima zaidi?.Baada ya Muda mwingi kupita baba yake na Mohammed Iqbal Dar alipokea barua nzito kutoka Serikalini akijulishwa kuwa alikuwa ni mmoja ya wabunifu 16 walioshinda jumla ya Tshs 200 na mgao wake ilikuwaTshs 12.50 na alilipwa kwa hundi zama hizo (1964).