View attachment 586451 Ulimwengu tuishimo na vitu vyote vilivyomo umetawaliwa na binadamu. Hata hivyo kutokana na tofauti kubwa ya binadamu kuna ambao wameitawala "nature" lakini wengine bado hiyo "asili" imewatawala. Hiyo ni kwa sababu ya uwezo tofauti wa kiakili ambao wanadamu wanaonyesha. Kulingana na sayansi na historia, binadamu wa leo ni matokeo ya evolution ya muda mrefu iliyotokea miaka milioni 3 iliyopita.
Utofauti wa wanadamu kubadilika kutoka kuwa weusi kisura na kuwa weupe ulianza kati ya miaka 100,000 - 60,000, kipindi ambacho wanadamu weusi walihama barani Afrika kwenda Mabara mengine kupitia eneo la Mlango Bahari ya Bab al Mandab nchini Djibouti lililokuwa limeungana na Arabia. Hiyo ni kwa kuwa nje ya Afrika, eneo kubwa lina baridi.
Mabadiliko ya kiakili yalitokea baadaye baada ya vizazi na vizazi kuishi katika maeneo hayo nje ya Afrika yakiwa na sifa kuu zifuatazo:
- Uwepo wa maji ya kutosha kutokana na mvua na mito mikubwa.
- Uwepo wa udongo wenye rutuba na rahisi kulimika (kwa miti) hasa kwenye mabonde ya mito.
- Uwepo wa vyanzo vya kutosha vya samaki kama mito, maziwa na bahari.
- Uwepo wa mwanga wa kutosha kukuza mazao.
- Uwepo wa mazao yanayositawi kwa urahisi, hasa ngano.
- Kutokuwepo kwa misitu minene na hivyo kuwa rahisi kuanzisha makazi na mashamba.
- Kutokuwepo kwa magonjwa ya kitropiki, hasa malaria, yellow fever na sleeping sickness.
- Kutokuwepo kwa jua linalochoma (scorching sun) na hivyo kuwafanya watunze energy zao.
- Kutokuwepo kwa baridi kali kama iliyoko nchi za Kaskazini mwa dunia.
Sababu hizo ndizo zilisababisha jamii zilizoishi maeneo yenye Hali hizo kuanza Neolithic Revolution kati ya miaka ya 10,000 bc - 8,000 bc ambapo binadamu alianza kupanda mbegu kwa kusia ngano mashambani (maeneo laini yaliyotifuliwa kwa miti) na kuanza kufuga wanyama wakiwemo ng'ombe na mbuzi. Aidha, kutokana na wanadamu hao kufanikiwa kuzalisha chakula kwa wingi kulipelekea kuibuka kwa Civilizations za kwanza kabisa duniani katika eneo la Mesopotamia (Sumerian, Babylonia), Misri na China kuanzia miaka ya 6,000 BC, kutokana na maeneo hayo kuwa na sifa hizo hasa maji ya kutosha licha ya kuwa majangwani.
Jamii hizo za Mashariki ya Kati zilianza matumizi ya zana za chuma mapema kabisa ambapo ilipita miaka mingi kabla ya teknolojia hiyo kufika Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara ambako inakisiwa kuletwa kwetu Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara na Dola ya Meroe (Sudan) kutokea Misri kwenye miaka ya 400 BC. Kwa hiyo Wabantu walihama kutoka Cameroon mwaka 1000 BC kabla hawajapata teknolojia ya chuma.
Hata hivyo, kwetu Afrika, kutokana na uwepo wa mvua nyingi, chakula kilikuwa kikipatikana kwa wingi na kwa urahisi na hivyo kufanya akili za binadamu wa Afrika kutojishughulisha sana kama wenzao wa nje ya Afrika ambao walikuwa katika mazingira magumu ya majangwa na baridi kali. Waafrika waliendelea kupata chakula chao kupitia uwindaji wa wanyama, kuokota matunda ya mwituni na kula mizizi. Hivyo mababu zetu hawakuchanganya akili sana kama wenzao kutokana na kutokuwa na uelewa juu ya kilimo na ufugaji. Hivyo kwa yule Mwafrika aliyekuwa na akili sana bado hakuwa na tofauti kubwa na asiye na akili kwa kuwa wote hawakujishughulisha sana na utafutaji wa chakula kama wale waliohama kutokana Afrika. Kwa wanadamu waliohama Afrika ambao walikuwa dhaifu hawakuweza kustahimili mazingira Magufuli na hivyo vizazi vyao vilifutika duniani na kuacha waliokuwa na nasaba bora wakistahimili mazingira hayo magumu (Refer the Theory of Survival of the Fittest).
Binadamu hao waliotoka Afrika kutokana na kuchangisha sana akili zao waligundua ufugaji wa wanyama hasa ng'ombe, mbuzi, kondoo, mbwa, kuku na bata, miaka kati ya 10,000 - 8,000 BC. Vilevile, waligundua namna ya upandaji wa mbegu kwenye mashamba yaliyolimwa kwa kutumia miti (kipindi kabla hawajagundua kuyeyusha Chama) kwenye udongo laini wa mabonde ya mito. Na hawa ndio waliogundua chuma na hivyo kuweza kuzalisha chakula kingi zaidi na kuimarisha ulinzi dhidi ya wanyama wa mwituni na wanadamu wengine maadui. Uwezo wa chakula cha ziada, ulipelekea kukua kwa shughuli za huduma na maspecialists, kama waashi, wahunzi, askari wa kudumu, viongozi wa dini, na wengine wengi. Nadhani mtakumbuka ujenzi wa Mnara wa Babeli, ambao ni matokeo ya uzalishaji mkubwa chakula cha kulisha watu wengi wasiolima.
Mambo haya hayakuwezekana kamwe kwenye jamii za kiafrika kipindi hicho kutokana na kutozalisha chakula cha ziada, hivyo kila mtu alipaswa kujua karibia kazi zote (Mpaka sasa sisi Waafrika specialization bado iko nyuma kwani mwanachuo analazimishwa kusoma vita vingi mno).
Teknolojia ya ufuaji wa chuma na utengenezaji wa zana za chuma ilipelekea kuongezeka kwa watu wengi Afrika lakini ilikuja kwa kuchelewa sana kutoka Mashariki ya Kati, tofauti na mabara mengine ya Old Lands ambayo yalianza kutumia zana za chuma zaidi ya miaka 3,000 bc.
Ili muone faida ya mapinduzi ya zana za chuma, Wabantu walitokea Cameroon baadaye baada ya miaka ya 400 BC waliweza kuvamia na kuzishinda jamii nyingine zote za Kusini na Mashariki ya Afrika zikiwemo za San na Pygmy (na hata Cushites - Mbulu, Gorowa na Mbugu) ambazo hazikuwa na tekonolojia ya chuma. Hata hivyo uhamaji huo wa Wabantu ulishindwa kwa Nilotes pekee (walitokea Kaskazini) mfano Wajaluo kwa Tanzania.
Nawasilisha hoja.