Asili ya maneno 'Shikamoo' na 'Marahaba' ni utumwa, kwanini tunaendelea kuyatumia?


= Kiarabu

Si kweli.
 
"Anaa tahat rujulaak" hiyo ndio tafsiri ya kiarabu kuwa nipo chini ya miguu yako. Sikamoo haimo katika kamusi yeyote ya kiarabu hata Iran
 
Brothers and sisters, I want to learn Swahili. Can you guys help me? I was born in Kenya but I left at a young age.
 

Salamu ambayo iliyokuwa official miaka ya nyuma kwa waswahili ilikuwa "Jambo!" Habari gani!?
 
Habar zenu wadau wa JF ,

Mimi ni mwajiriwa katika Taasisi fulani katika position niliopo tupo vijana wachache majority na watu wazima na wazee (40 to 55) kulingana na nature ya kazi yangu wengi wao wanahitaji usimamizi wangu kazini .

Na pale wanapokosea sina budi kuwaadabisha sasa inakuja mahala mtu anataka umwamkie kitu ambacho nlijifunza mahala nilipokua nafanya kazi mwanzoni nilikua nawasalimu wakubwa kwangu but wote walikuja kunidharau na pale nilipotaka kutoa adhabu walinibeza na vijineno" katoka juzi shule sie tunajua maisha wazazi wako ".

Nilitafuta ushauri kwa wakubwa zangu kazini niliambiwa nimeharibu kumwambia shikamoo aliyeko chini yangu badala yake nisalimie "HABARI ZA SAHIZI,ZA LEO,ZA ASBH N.K.

Tangia hapo niliacha kutoa shikamoo kwao mpaka nimehamia Taasisi ingine.Huku ndio wananibeza kusalimia japo msimamo wangu ni uleule SITOI SHIKAMOO TENA.

Nimekua nashangazwa sana pale MTU anapolazimisha salamu japo nawaheshimu kama wanaonizidi .

Swali: Je Shikamoo ndio ishara ya heshima kwa MTU au nini zaidi nifanyeje?

Tushauriane wadau.
 
Usichanganye mambo, shikamoo na cheo havina uhusiano na haviendani kabisa, haijalishi una cheo/mamlaka kiasi gani kama kuna mtu amekuzidi kiumri haijalishi ni nani hata kama wewe ni bosi LAZIMA UMPE haki yake (Shikamoo) kuwa na cheo kusitufanye tuache mila na desturi zetu nzuri za kitanzania, kama wewe ni bosi kazini, walio chini yako haijalishi wana umri gani NI LAZIMA wafuate maelekezo yako wewe mkuu, hata kama wao wamekuzidi umri,

Bado mtu anaweza kukuzidi umri, ukawa unampa shikamoo, unamheshimu, lakini bado anapokosea unayo haki ya kumwambia/ kumrekebisha bila kuathiri heshima yenu iliyopo
Cha muhimu ni kujifunza namna bora ya kuwaambia hao walio chini yako katika masuala ya kazi
Shikamoo ni salamu anayopewa mtu aliyekuzidi umri kama heshima ya kutambua kwamba waliotuzidi umri wanajua mengi, wana uzoefu zaidi wa maisha, wana busara na hekima zaidi,

Wape haki/shikamoo yao na pia shughulika nao watimize wajibu wao kazini
 
Hiyo kauli sasa"kumpa MTU haki yake "sio lazma Shikamoo pia jaribu tafta maana yake ni tafadhal
 
Toa heshima we ni bwana mdogo husilewe cheo!!!Ila mazoea acha just wape heshima yao lakini swala kuwabana kazini usililetee heshima OVer!!!
 
N neno la kitumwa maana yake "Niko chini ya miguu yako" ...................?iko haja ya kuangalia matumizi ya hii salamu..Kwan haiendan na lugha yyt ile Why Kiingereza mtu akwambie Gdmorning or whatever...au kuna neno sawia tafsiri ya Shikamoo ktk makabila yetu??_Hii n kutokana na uelewa wangu
 

Wenzako wamekumbana na kinyume chake - mahala pa kazi unakuwa boss, walio chini yako hata kama ni umri wa wazazi wako, utasikia "shikamoo boss"!! Na mitaani ukiwa na vijisenti utapewa shikamoo na hata bibi & babu yako!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…