Fall Army Worm
JF-Expert Member
- Jan 8, 2015
- 19,355
- 14,408
Habari wana JF,
Kuna hii salamu inayotumika sana na watu wengi wa kila kabila hapa nchini na hata nje ya nchi ya ''SHIKAMOO''halafu jibu lake likiwa ni''MARA HABA''.
Mimi niliwahi kuambiwa na mwalimu wangu wa HISTORY kuwa SHIKAMOO, M.Ynipo chini ya miguu yako, sasa kama ni hivyo, je watu wanaielewa kweli maana hiyo?
Salamu hii ninachojua mimi hutumika kuashiria heshima kwa mtu anayekuzidi umri, lakini huwa ninashangaa baadhi ya maeneo unakuta Mtu mkubwa eti anamsalimia mdogo SHIKAMOO, na siyo kwamba hajui kama amemzidi umri, la hasha! anakuwa anajua bali hufanya hivyo kutokana na kipato alichonacho yule mdogo kwamba japo ni mdogo lakini utajiri wake hufanya watu wakubwa zaidi yake kumpa SHIKAMOO, Je hii ni sawa?
Karibuni kwa maoni..