SMU
JF-Expert Member
- Feb 14, 2008
- 9,613
- 7,889
Sababu za kuendelea na salamu hiyo bado zipo pamoja na historia yake mbaya...Narudia tena swali langu, na waswahili wanasema kuuliza siyo ujinga na wala si dhambi je, sisi watanzania tuna sababu ya kuendelea kutumia salamu hii yenye historia mbaya? Aulizaye anataka kujua na ni jambo jema, naombeni msaada wenu.
Kwanza, maana yake kwa sasa inakubalika na watumiaji (ukiacha wachache kama hao kina Rakeshi). Hilo la kukubalika ni la muhimu sana kwa sababu kama watumiaji hawapo tayari kutumia neno/salamu mbadala hata huo mbadala uwe bora kiasi gani utabakia vitabuni tu/kwenye kamusi.
Pili, bado hakuna mbadala ambao utaweza kukubalika na jamii zote za wazungumzaji wa kiswahili (pengine swali litakuja, ni lazima kuwepo na mbadala?) - jubu langu ni 'ndiyo' kwa sababu tofauti ya umri bado itaendelea kuwepo na salamu hiyo inaweza kuondoka au isiwe muhimu au isihitaji mbadala kama utamaduni wa wa mdogo(aghalabu kwa umri! ingawa inaweza kuwa wadhifa, madaraka etc katika jamii/koo) kulazimika kuonesha/kuashiria kuwa anamuheshimu au anatambua au anaamini ukuu/ukubwa wa anayempa shikamoo utatoweka.
Practically, kuna nyakati shikamoo inakuwa ndio salamu pekee inayoweza kutolewa - kwa mfano, mtoto (mzungumzaji wa kiswahili) wa miaka mitano anakuja kwako na anataka kukusemesha (say hamjakutana kabla), anaweza kukupa salamu gani? Binafsi, kwa mfano, akiniambia "habari za saa hizi?" nitashangaa. Watoto mara nyingi hawatumii salamu nyingine au ya nyongeza juu ya hiyo "shkamoo" au "skamoo" au kwa wale wanaopevuka/balehe wanasema "shii" au "shiik"!
Its so funny, ukutane na kundi la watoto wadogo na kila mmoja anataka kukusalimu.....ni lazima uitikie moja moja mpaka waishe...usipoitika wanarudia!