Asili ya maneno 'Shikamoo' na 'Marahaba' ni utumwa, kwanini tunaendelea kuyatumia?

Asili ya maneno 'Shikamoo' na 'Marahaba' ni utumwa, kwanini tunaendelea kuyatumia?

..Narudia tena swali langu, na waswahili wanasema kuuliza siyo ujinga na wala si dhambi je, sisi watanzania tuna sababu ya kuendelea kutumia salamu hii yenye historia mbaya? Aulizaye anataka kujua na ni jambo jema, naombeni msaada wenu.
Sababu za kuendelea na salamu hiyo bado zipo pamoja na historia yake mbaya.

Kwanza, maana yake kwa sasa inakubalika na watumiaji (ukiacha wachache kama hao kina Rakeshi). Hilo la kukubalika ni la muhimu sana kwa sababu kama watumiaji hawapo tayari kutumia neno/salamu mbadala hata huo mbadala uwe bora kiasi gani utabakia vitabuni tu/kwenye kamusi.

Pili, bado hakuna mbadala ambao utaweza kukubalika na jamii zote za wazungumzaji wa kiswahili (pengine swali litakuja, ni lazima kuwepo na mbadala?) - jubu langu ni 'ndiyo' kwa sababu tofauti ya umri bado itaendelea kuwepo na salamu hiyo inaweza kuondoka au isiwe muhimu au isihitaji mbadala kama utamaduni wa wa mdogo(aghalabu kwa umri! ingawa inaweza kuwa wadhifa, madaraka etc katika jamii/koo) kulazimika kuonesha/kuashiria kuwa anamuheshimu au anatambua au anaamini ukuu/ukubwa wa anayempa shikamoo utatoweka.

Practically, kuna nyakati shikamoo inakuwa ndio salamu pekee inayoweza kutolewa - kwa mfano, mtoto (mzungumzaji wa kiswahili) wa miaka mitano anakuja kwako na anataka kukusemesha (say hamjakutana kabla), anaweza kukupa salamu gani? Binafsi, kwa mfano, akiniambia "habari za saa hizi?" nitashangaa. Watoto mara nyingi hawatumii salamu nyingine au ya nyongeza juu ya hiyo "shkamoo" au "skamoo" au kwa wale wanaopevuka/balehe wanasema "shii" au "shiik"!

Its so funny, ukutane na kundi la watoto wadogo na kila mmoja anataka kukusalimu.....ni lazima uitikie moja moja mpaka waishe...usipoitika wanarudia!
 
yaani nchi ipo kwenye saga nyingi kama IPTL, kusafirishwa kwa Twigwa na kuchakachuliwa kwa katiba halafu mtu anaona topic ya shikamoo marahaba ndo ishu ya maana ya kuongelea. Maana ya kitu hubadilika jinsi miaka inavyoenda. Tafsiri ya kitumwa haipo tena. Lugha ndivyo inavyokua.
 
Kupitia salamu Watz tunaukubali mfumo wa mabwana na watwana.
Salamu zetu ni za kikoloni
Hivyo
Uongozi wetu ni wa kikoloni
Uchumi wetu ni wa kikoloni
Elimu yetu ni ya kikoloni
....na akili zetu zimeukubali ukoloni wa mtu mweusi
 
Duniani kwingineko, watu hawasalimiani kwa kuulizana maswali (eg Habari za asb ???) ambapo jibu lake huwa ni la uongo (Nzuri).

Au mtu mmoja kujishusha kwa mwingine (shikamoo - marahaba) ambayo hujenga akili za utumwa.

Wenzetu husalimiana kwa kutakiana kheri tu (Good morning) na jibu lake huwa nawe pia.
Na matokeo yake watu hao wanakuwa na kheri.
 
Mikael P Aweda

Nami nakuuliza kwa NIA njema,

Je, ni lugha gani hiyo....!?
Ambayo "MAR HABA" inakuwa =MARA SABA....!?
 
Last edited by a moderator:
mi naona hakuna tatizo nikimwamkia shikamoo mama au baba (nashika miguu yako ) nao wakijibu shika mara saba ok wanastahili tatizo liko kwa wale wazee wa dot.com ukiwaamkia wanazuga au kuuchuna kabisaa

Kwa nyinyi kina dada sawa.

Tatizo unakuta dume, lina ndevu mpaka zina mvi, shikamoo, ... kisa bosi !!!

Salamu hii Jeshini ilipigwa marufuku
 
Ukirejea historia, utakataa kila kitu au kila neno. Yapo mambo mengine unapaswa kukubaliana na wakati hasa yanapokuwa hayana maana ile ile. Maneno kama kupiga bao, kukaza, tigo, masaburi, kihiyo nk yameshageuzwa. Kuifuta shikamoo na marahaba leo ni kazi kweli kweli. Lakini lugha huzaliwa na kufa. Maneno kama kabwela, bwanyenye, mabeberu, makaburu nk kidogo kidogo yanatoweka. Tusubiri na hii shikamoo-marahaba nayo ipate natural death!!

kweli kabisa, hata neno "ndugu" lilikufa likaja neno mbadala..... "mheshimiwa"
 
Naunga mkono hoja 100%.
Duniani kwingineko, watu hawasalimiani kwa kuulizana maswali (eg Habari za asb ???) ambapo jibu lake huwa ni la uongo (Nzuri).

Au mtu mmoja kujishusha kwa mwingine (shikamoo - marahaba) ambayo hujenga akili za utumwa.

Wenzetu husalimiana kwa kutakiana kheri tu (Good morning) na jibu lake huwa nawe pia.
Na matokeo yake watu hao wanakuwa na kheri.

ayse tungekuwa bar ningekuagizia kilaji
 
Ni sahihi tu mkuu hasa katika mazingira ya sasa kwa kuwa anaeitoa na kuipokea anaichukulia kama heshima tu ya kawaida na wala wote wawili hawaiweki kwenye fikra ya kitumwa. Tatizo langu ni wale wanaokata shikamoo na mwingine anaitikia marhaba bila kukolezea mambo mengine madogo madogo kama mmeamkaje na vitu vingine vinavyoambatana na shikamoo
 
monile....ena monile,habari za kusangaluka....kobwina/hinyahe.

mwangele....ena mwangele numo.
 
ndugu yangu Fundisi c kweli kuwa watalii wanafundishwa salamu iyo ,ila wanafundishwa kusema -jambo, karibu, hakuna matata, asante (sana) ni maneno ambayo n common na yana tafsiri yake . shikamoo & marahaba haina tafsiri kwa mgeni

Hili wala halina ligi. Hiyo jambo ni ya kenya. Huku watalii wanafunzwa hiyo shkamoo marahaba. Ofcoz na mengine pia.
 
Anzieni kwa wazazi wenu afu mnipe majibu!

Mimi sina wazazi kwa sasa watakaonidai salamu hiyo. Hata kaka zangu wakubwa katika mazingira niliyokulia sikuwa natumia salamu hiyo maana salamu ilikuwa ya kiasili. Salamu hiyo nimeanza kuitumia shuleni, na baada ya hapo nimekuwa muhanga wa kuipokea kutoka kwa wanafunzi niliopata kuwafundisha pamoja na watoto. nafikiria kuipiga stop taratibu nyumbani kwangu ila inabidi kuangalia madhara yake kwa jamii inayokuzunguka pale mwanao atakapoonekana hana adabu kwa "kutowapa shikamoo" wakubwa! Kazi kweli kweli. Salamu imeshaota mizizi na labda haina madhara yoyote kwa kuwa asilimia kubwa ya wanaosalimia na kusalimiwa kwa kutumia salamu hiyo hawajui asili yake wala hawajui inamaanisha nini.
 
Huyo aliyekutana na Mwalimu Nyerere kwao ikoje?

Soma hii!

Indian Greeting Customs and Traditions
What is Namaste?
Among all the countries in Asia, India can be placed among the top 2 or 3 most traditional country. We will first start out slowly with India. In this article, I will cover the greeting customs in India. According to psychologists, the first impression you have of a person never changes 95% of the time. For that reason I feel this is a very important subject.
If you have already travelled to India before, then you know about the customs of "Namaste," the traditional greeting in India. The meaning of "Namaste" is "I bow to (respect) that whats good in you." This gesture consists of pressing both palms together and placing them at chest level.
After your palms are in place, you should follow it with a slight nod of your head. Now, the slight nod is different from a bow. Bowing is only for the Japanese or Chinese, but India does not require you to do it. As a matter of fact, you should never bow.
"Namaste" is a common opening line.It is used to start a conversation and does not constitute to good morning, good afternoon, or good night. 'Hi' is used as the greeting among youngsters due to western influence. Also, Namaste is used to show respect to elders. Generally, you do not need to use "Namaste" when you are greeting friend or sibling.
 
Bado ukweli uko palepale kwamba hili neno lilikuwepo kukandamizwa watumwa(haswa sisi weusi), iweje tulichukue na kulifanya letu?

Kama WoS alivyo sema kwani hamna neno mbadala? Iweje kumuambia mtu nipo chini ya miguu yako iwe heshima? Kwani lazima tuige kila kitu? Au sasa ni sisi tunaendeleza utumwa wa kimawazo bila pingu na kengele?

Nawashukuru wachangiaji wote hata wale ambao tuna mawazo tofauti.

Mkuu kama hujui ni kuwa mtu mweusi ameendelea kuwa mtumw ahadi hii leo tunavyozungumza haya,kwahiyo wewe kubali matokeo tuu,watu weusi ni watumwa mpaka mwisho wa uhai,period!!
 
Back
Top Bottom