SHIKAMOO - MARAHABA SHIKAMOO MARAHABA.
Shikamoo ilikuwa ni salamu za watumwa kwa mabwana zao.
je, sisi watanzania tuna sababu ya kuendelea kutumia salamu hii yenye historia mbaya? Aulizaye anataka kujua na ni jambo jema, naombeni msaada wenu.
Mkuu Shemeji Aweda, asante kuliulizia hili!, lugha inazaliwa, inakuwa na mwishowe inakufa!, lugha nyingi za kale saa hizi ni marehemu na lugha mpya za kisasa zinaibuka!.
Kukua kwa lugha kunatokana na kuingia kwa maneno mapya kila uchao, na huku maneno ya zamani yakitoweka.
Hata kama shikamoo kwa lugha ya Kiarabu ilimaanisha hivyo, kwa Lugha ya Kiswahili ni neno la heshima kwa mdogo kwenda kwa mkubwa, hivyo lina positive canotation meaning ya heshima, halina sababu ya kufutwa kwa sababu kwa sasa Shikamoo ni salaam ya heshima kwa lugha ya Kiswahili na sio ile ya kitumwa ya Kiarabu!.
Neno likiwa na positive canotation meaning, linapaswa kuendelea kutumika kwa positivity ya canotation meaning yake!. Vivyo hivyo lugha ya Kiswahili imeundwa kwa maneno ya kukopa kutoka lugha mbalimbali zikiwemo lugha za Kibantu, mfano neno "nina", "mae", "mayo" na "nyoko" maana yake ni mama kwa lugha za Kibantu, kufuatia mtindo wa kumtukania mtu mama yake, kwa kukitaja kile kiungo cha "K" na linafuatia jina la "K... mama yako", "K... mae", "K...nyoko", "K... nina", tusi ni ile "K" linalofuatia ni jina la mama!. Kufuatia bad canotation meaning ya tusi hilo, sasa imefikia hata mtu akisema neno "nyoko", linatafrisiwa kama tusi, wakati kihalali kabisa "nyoko" ni "mama!".
Shikamoo iendelee kwa sana, tena zaidi ya heshima, pia siku hizi shikamoo hutumiwa na wadada kama kinga, ili ile mibaba inayopenda dogo dogo, ikiisha amkiwa tuu shikamoo, hapo binti anakuwa ameweka kinga libaba lisimtokee!, na hata akitokea mtu ni size yako kabisa tena halali yako, akikuamkia shikamoo ujue sio heshima tena bali ni kinga kukuzuia us advance!.
Mimi nikikutana na hizi "shikamoo za kunyimana" huwa siziitikii "marahaba" bali naitikia "poa", ili nikiamua nisikutane na kizingiti cha "shikamoo!".
Thanks.
Pasco.