JT2014
JF-Expert Member
- Jan 18, 2014
- 1,863
- 1,368
Mkuu ulivyosema ni sawa,nami nilijaribu sana kufuatilia asili ya salaam hii,ufafanuzi niliopewa niliuamini kwani maswali yangu yalikuwa kama shikamoo ni salaam,kwa nini jibu lake liwe marahaba?
Jibu nililopewa ni kwamba:
Watumwa walikuwa wakikamatwa na wake zao wanafungwa minyororo na kuwekwa kwenye msafara wakibebeshwa mizigo. Aliyekuwa akionyesha kuchoka na kudhoofu na kushindwa kuendelea na safari aliuawa kwa upanga na wengine waliendelea.
Sasa ilipotokea hivyo kwa mke wa mtu,mwenye mke au ndugu wa mhanga akataka kupigana walimtishia naye kumuua na ili ajisalimishe alisema shikamoo yaani niko chini ya miguu yako na alijibiwa mara-haba,ikiwa na maana kwamba usizoee hii tabia maana msamaha kama huu unatokea mara haba.
Ki ukweli baada ya kupewa ufafanuzi huu niliichukia hii salaam,Lkn cha kujikumbusha ni kwamba mashuleni tunajifunza somo la historia,ambalo kwa kweli linatukumbusha machungu waliyoyafanya wakoloni lkn mpaka leo halijafutwa somo hili.
Hivyo na hii salaam inabidi tuizoee kwamba haina tena maana kama ile ya zamani bali ni tendo la kuonyesha heshima ya mdogo kwa mkubwa aliyemzidi na si vinginevyo.