Asili ya maneno 'Shikamoo' na 'Marahaba' ni utumwa, kwanini tunaendelea kuyatumia?

Asili ya maneno 'Shikamoo' na 'Marahaba' ni utumwa, kwanini tunaendelea kuyatumia?

waenglish safi sana ni goodmorng.. goodafternoon... goodevening... haijalishi umemzidi umri au anakuzidi au mnalingana... hii yetu ya shikamoo kweli itakuwa ni ya enzi zile za kitumwa...
 
Sasa utakuta mjomba wako unaye muheshimu na ana umri mkubwa ambao hata mama yako anatoa shikamoo halafu huyo mjomba wako ameoa msichana ambaye ki umri wewe unamzidi hata miaka 7.

sasa je, utamsalimia mjomba wako shikamoo halafu mkewe umwambie za sahizi? sio kwamba tunawapa shikamoo kwa kupenda wakati mwingine ni mazingira.
 
Hapo umechukua uhalisia wa neno, lakini katika kiswahili neno hili linatumika kama salamu, tazama mfano mwingine:

mambo: haina maana ya salamu lakini watu wanatumia kama salamu.

upo hapo?

"mambo" ina maana ya salaam ingawa imefupishwa. kwa kirefu waweza sema "mambo yako yapo vipi? maana salaam ni aidha kumjulia/kumuulizia mtu (na mambo yake) hali au kumtakia wasaa/wakati mzuri
 
kwanza nadhani kuhalalisha shikamoo ni utakatishaji wa salaam ya kifedhuli..kama tunaweza kutengeneza maneno na tukayaincorporate katika kiswahili kuendana na sayansi na ugunduzi mpya kwa ujumla tunashindwa nini kutafuta neno litakaloleta maana yenye heshima kusimamia salaam katika kiswahili?

ni kichekesho kwamba mtoaji na mpokeaji wa "shikamoo/marahaba" wote tunajua chimbuko lake ni baya lakini tunang'ang'ania kama vile tumefikia mwisho wa ubunifu!!!


na ukizama zaidi utaona ukiiondolea maana yake halisi ya "nipo chini ya miguu yako/mara haba/mara chache/haijatosha" basi hayo maneno yatakuwa hayana maana yoyote na tafsiri yake haitakuwepo bali mtu akiulizwa tafsiri ataishia kutoa matumizi!!!

ukisema mwadela baba/tata olaillota na mengineyo mtu akikuuliza tafsiri utajibu tu ni "umelalaje baba" sasa shikamoo/marahaba tafsiri yake ni nini?
 
Iko hivi. Kwa waliosoma historia ya waarabu enzi za utumwa watakuwa wanaelwa maana ya shkamoo.

Shikamoo ni neno la kiarabu lenye maana ya nipo chini ya miguu yako. Na lilitumiwa hasa na wafungwa ambao walikuwa wakilitumia kuwasalimia waarabu(Wakoloni wao).

Na Marahaba maana yake ni 'Ninakubali' likimaanisha amekubali salaam yake.

Kwa Hivyo: Kila lugha inakopa baadhi ya maneno kutoka lugha nyingine ili kukamilika, kwa hiyo hata kiswahili kilikopa baadhi ya maneno ya kiarabu na kutoka lugha nyingine za kibantu.

Ni hayo tu.

tafsiri yako ndugu nusu inapotosha ukweli kidogo..kwa upande wa shikamoo ni sawa "nipo chini ya miguu yako" lakini "marhabaa" au "marahaba" ilimaanisha "haijatosha/hairidhishi" (angalia mara in terms of "times" na "haba" kuonyesha uchache au kutotosha) ikiwa na maana kwamba bwana anamwambia mtwana "no matter what you do, you can never satisfy me"
 
ni kweli tafsiri ya lugha ya kiarabu ndiyo hivyo na ilikuwa na maana hiyo enzi hizo za utumwa.

Lakini mkumbuke lugha yeyote duniani lazima ikuwe, hivyo, kwa mila na desturi za kiswahili chetu haina tena maana ile ya enzi za mtumwa na mtwana. ina maana na tafsiri hii tunayoijua mimi na wewe na si vinginevyo. Kama zitafanyika jitihada za kurudisha maana ile ya zama zile itachukua miaka kadhaa kama siyo miongo kadhaa.

Mfano jirani zetu ni kawaida sana kukuta kichwa cha habari kuwa Waziri amewa"dindia" wabunge kuhusiana na jambo fulani, lakini kwetu huku nani anaweza sema fulani amewa"dindia" watu fulani?
 
Ni utamaduni wa kiafrika kumpa heshima anaekuzidi umri au yupo usawa na wazazi wako. Angalia makabila ambayo huwezi kumwamkia mkubwa na wewe umekaa aumafao uko juu ya basikeli , pia kuna makabila wawake wanapiga magoti wanapo msalimu mtu wa makamo. Huu sio utumwa bali kuonesha heshima.

Mtu mweye umri sawa na wewe unamwamkia habari za asubuhi / jioni au umemakaje / umeshindaje

Shikamoo ni msemo tu hana maana wewe ni dhalili kwa huyo unayemwakia anaposema marahaba ni kuwa kapokea salam na anakusalimu wewe pia ni sawa na kusema hello.
 
Kwa nilivyosikia mimi neno shikamoo maana yake ni "niko chini ya miguu yako.

Pia nimesikia hilo neno ni la kitumwa na lilikuwa linatumiwa na watumwa kuwaonyesha heshima wakuu wao.

Kuna baadhi ya watu nawajua hawapendi kupewa shikamoo na hata wakipewa hawajibu marahaba.

Je kama hili neno ni la kitumwa, kwanini sisi tuendelee kulitumia kama neno linaloashiria heshima?

Kama lilitumika kuwakandamiza mababu zetu kwanini na sisi tulipe nafasi? Au tunalitumia kama wenzetu Wamarekani weusi wanavyo tumia neno "nigga" ambalo lilitumika kudharau mababu zao na kulifanya la kwetu sasa?

Mi naona tayari umeshajipa jibu..kwamba maana ya neno,hubadilika kwa wakati.Ni kama huo mfano wa nigger.
 
Habari,

Nashangaa watu Tanzania peke yake hutumia neno shikamo kama salamu ya kumtunikia mtu heshima ilhali ni utumwa wa kisaikolojia, shikamo ni neno la kiharabu humaanisha nipo chini ya miguu yako.

Huu ni ujinga uliopitiliza hata mataifa yote hamna kitu kama hichi, kwanza hata tafsiri yake hakuna iwe kwa lugha yeyote duniani na kingine uende dukani useme eti naomba hahaha hii nchi ni vichekesho unaomba huku unatoa sarafu.

Ndio maana hata mkiambiwa laleni hakuna kufanya lolote mnafanya kweli ujinga mwalimu aliukemea nyie mkaukumbatia.
 
Shikamoo ni lugha ya utumwa kweli lakini saa hivi imezoeleka kama salamu kuonyesha heshima. Na kweli wengi hawajui maana yake. Mi huwa naitikia poa mtu akiniambia shikamoo kwanza siipendi.
Ila kusema naomba ni lugha ya ustaarabu kuliko kusema nipe.
 
Naamini neno lolote maana yake yenye nguvu ni tafsiri ya watumiaji wa neno hilo.
 
Habari,

Nashangaa watu Tanzania peke yake hutumia neno shikamo kama salamu ya kumtunikia mtu heshima ilhali ni utumwa wa kisaikolojia, shikamo ni neno la kiharabu humaanisha nipo chini ya miguu yako.

Huu ni ujinga uliopitiliza hata mataifa yote hamna kitu kama hichi, kwanza hata tafsiri yake hakuna iwe kwa lugha yeyote duniani na kingine uende dukani useme eti naomba hahaha hii nchi ni vichekesho unaomba huku unatoa sarafu.

Ndio maana hata mkiambiwa laleni hakuna kufanya lolote mnafanya kweli ujinga mwalimu aliukemea nyie mkaukumbatia.

Hii ni tamaduni yetu, na hatuwez kuiacha!!! Mama FaizaFoxy shikamoo
 
Last edited by a moderator:
ushaamkia sana, kichaa cha ukubwani kimekupanda unakileta hapa. Nenda hukohuko uarabuni kama we mwarabu
 
Back
Top Bottom