Asili ya maneno 'Shikamoo' na 'Marahaba' ni utumwa, kwanini tunaendelea kuyatumia?

Huku Tanga hatunaga shikamoo.. Iwe mtu mzima wa umri gani..salamu yetu ni Asalam aleikum..
 
Reactions: Dyf
Shikamoo kimsingi hainaga maana tutazunguka wee mara ooh m ni mila zetu mara sijui nini Africa ni upuuzi mtupu
Pale unayejifanya kumuheshimu anafanya mambo ya aibu
 
Toa heshima we ni bwana mdogo husilewe cheo!!!Ila mazoea acha just wape heshima yao lakini swala kuwabana kazini usililetee heshima OVer!!!
Bado unatoka nje ya mada...Nawapa heshima zao sana tu BT sio Shikamoo mkuu
 
Ni salamu ha kiarabu enzi za utumwa! Akimaanisha niko chini ya miguu yako( mweusi to mwarabu) but mwenyewe kwa wenyewe hawakusalimiana hvy. Hao hao wanaolilia shikamoo ukiwaambia good morning wanakuwa wapole
 
Reactions: Dyf
Tatizo waswahili tunaupenda utumwa sana kupitiliza. Mtu mzima ukimwambia "habari za asubuhi" atawaka eti huna heshima eti umwambie shikamoo. But huyo huyo ukimwambia "Goodmorning" atakujibu kwa furaha .....mpk wajiuliza sisi tuna matatizo gani??? Nani katuroga!?
 
Huku Tanga hatunaga shikamoo.. Iwe mtu mzima wa umri gani..salamu yetu ni Asalam aleikum..

Sheikh hiyo itakua ni Tanga mjini na maeneo ya Muheza. Kule kwetu Korogwe neno shikamoo lipo palepale! mbaya zaidi kwa wenzetu wadada na wamama wanapoolewa basi hawana budi kuwasalimia wakwe zao(baba mkwe na mama mkwe) kwa neno hili ''Mwinyi!!'' halafu baba mkwe/mamamkwe anaitikia ''Mwinyi wa Said!!'' ha ha ha ha ha!

Hapo unatakiwa kila utakapokuwepo kule basi kila asubuhi uanze kupitia nyumba moja baada ya nyingine na kuwasalimia ndugu wa ukoo wako hasa wale waliokuzidi umri, kinyume cha hapo hueleweki! utaonekana u mtoto mkaidi maana huko ndiko kule milimani ambako watu wanaishi kikoo.
 
Tatizo sio shikamoo. Ninachokiona mimi unapoingia sehemu mpya lazima uwasome watu, unapojifanya mjuaji itakuumiza. Wasikilize, wahoji kirafiki baadaye wabadilishie kibao lakini usichelewe. Wasije wakajenga mazoea.

Shikamoo: I am kneeling before you.
Marahaba: not enough (hata mara ngapi)
 
Shikamoo maana yake nini kwa Kiingeleza?
Maana waingeleza wana Good Morning
 
Reactions: Dyf
Thanks mkuu kwa mchango wako....iko haja pia kwa wadau Wa lugha kuangalia matumiz ya neno SHIKAMOO
 
Aisee nilikuwa sifahamu maana ya shikamoo. Now that I know hamna shikamoo tena hata uwe nani au umenizidi umri kiasi gani
 
Reactions: Dyf
Aisee kwanza nikupe hongera kwa kutupa ufahamu juu ya huu utumwa mambo leo,mimi mwenyewe nimekuwa najiuliza sana kwanini sisi waswahili tumekuwa tunafwata kila jambo ambalo tumelikuta babu zetu wakitumia na fika tukijua kuwa babu zetu walikumbana na utumwa,nadhani ifikie mahali TAKI wafanyie marekebisho baadhi ya maneno ya kiswahili hasa haya yanayo endeleza utumwa mambo leo.
 
Reactions: Dyf
Babu zako wenye nguvu na akili kiduchu waliwauza babu zako waliokuwa mapunguani.

Kama hilo ni neno la kitumwa vipi na ile mila ya wanawake kupigia magoti wanaume wakiwaamkua?

Isitoshe, utumwa haujaisha hadi leo hii na Tanzania ni moja ya nchi zilizo juu juu kwenye list ya nchi zenye kuendeleza utumwa duniani.
 
Mbona povu linakutoka bibi kutetea shikamoo??? Au sababu limetokea kuleeee?? Kwa waleee??? Maana wewe wakiguswa tu wale unakuwa mbogoo sana

Sent from my HUAWEI Y530-U00 using JamiiForums mobile app
 
MwanaFalsafa1 said: ↑

Nakubaliana wewe kwa 100% kwa sababu maana ya shikamoo haijabadilika Ni ile ile ya "niko chini ya miguu yako", lazima tuukubali ukweli kuwa shikamoo haina maana yoyote ya kiheshima.
 
MwanaFalsafa1 said: ↑

Nakubaliana wewe kwa 100% kwa sababu maana ya shikamoo haijabadilika Ni ile ile ya "niko chini ya miguu yako", lazima tuukubali ukweli kuwa shikamoo haina maana yoyote ya kiheshima.

Hapana, si kweli. Hiyo si maana ya neno shikamoo.

Kiswahili kitamu.
 
Tukishaitoa hiyo shikamoo,
Je tutakua tunawasalimia vipi wakubwa waliotuzidi umri?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…