Asili ya maneno 'Shikamoo' na 'Marahaba' ni utumwa, kwanini tunaendelea kuyatumia?

Asili ya maneno 'Shikamoo' na 'Marahaba' ni utumwa, kwanini tunaendelea kuyatumia?

Kuna mchangiaji hapa ( Mkuu Mkalibari ) alidai kuwa kila neno la Kiswahili unaweza kutafsiri kwa Kiingereza.

Nikamuomba anitafsirie Shikamoo / Marahaba.

Mpaka leo, hajarudi na jibu.
 
Shikamoo ni salamu ya kiswahili sawa na Unogile .... au the like.... kuna watu waliwahi sema eti ni salamu ya waarabu... wakati si kweli kabisa kwa mwarabu marhaba.... means ''Karibu''
 
To
Shikamoo ni salamu ya kiswahili sawa na Unogile .... au the like.... kuna watu waliwahi sema eti ni salamu ya waarabu... wakati si kweli kabisa kwa mwarabu marhaba.... means ''

To be honesty ni salamu ya kijinga, upumbavu na umungu mtu ndio kipaumbele hapo. tafsiri iliotolewa hapo juu ndio hio ambayo hata mimi nimekuwa nikiijua-Huwa natamani nisifundishe watoto salamu hii
 
siitambui salamu hii mimi sababu sio asili yangu katika kabila langu hakuna hata kabila lolote tanzania hakuna zaid ya mwarabu alivyonyanyasa babu zetu na salamu hii mfano kabila lenu mnasalimianaje kuobesha heshima sisi tunaweka cheo kama heshima mfano mwadela mayo /baba
 
umeongea ukweli asilimia mia, ila umesahau hata kiswahili unachoongea ni lugha ya kitumwa,
ishara ya msalaba ni ishara ya kitumwa,
kusujudu kwa kuinama chini ni utumwa,
ukristo na uislamu ni utumwa,
majina yako na ya wazazi wako ni ya kitumwa
mfumo mzima wa serikali ni wa kitumwa, binadamu tumeikuta ardhi ila serikali inasema ni ya kwao, na wana mamlaka ya kukufukuza na kubomoa sehemu uliyojenga.
mfumo mzima wa imani tumeletewa, huo nao ni utumwa, haiwezekani Abdallah amchukie Johnson au Jackson amchukie Hashim kisa wapo dini mbili tofauti wakati wote ngozi zao ni nyeusi.

H U U N I U P U M B A V U W A H A L I Y A J U U.
 
  • Thanks
Reactions: Dyf
Habar zenu waku ,,unapomsalimia mtu (shikamo) ina kua na mana gan hasa na kwa nin tunaipend salam hio watanzania ??ad wengin salam tulizo funzwa na dini tumesahau ,,nin maana ya shikamo na kwanin inapendwa saana kutumiwa kma salamu kuu. hapa inchin kwetu!!
 
Hiyo salamu haina maana zaidi ya habari za asubuhi /mchana /jioni
Watu wa Taasisi ya Taaluma za kiswahili ( TATAKI) waje watueleze na kutusaidia zaidi tusijekuwa tunatembelea kivuli cha Mkoloni.
 
Habar zenu waku ,,unapomsalimia mtu (shikamo) ina kua na mana gan hasa na kwa nin tunaipend salam hio watanzania ??ad wengin salam tulizo funzwa na dini tumesahau ,,nin maana ya shikamo na kwanin inapendwa saana kutumiwa kma salamu kuu. hapa inchin kwetu!!
Nadhani asili yake ni kipindi cha waarabu kati ya watwana na watumwa,
mimi toka kidato cha nne niliachana na hii salam na nashukuru familia ilinielewa, mdingi ili kuweka msawazo nilikua namsalimia kiinglishi tunamaliza, kijijini nako wameelewa so nahisi niko huru na hii salam
 
shikamoo ni kama saluti ktk majeshi yetu... shikamoo haiwezi kumjulia mtu hali maana mgonjwa na mzima wote huitikia sawasawa...lengo la shikamoo ni kumjulisha huyu ni mdogo kuliko huyu wala sio salaam ya kumjulia mtu hali
 
Mimi nadhani sisi waswahili hatujaibeba shikamoo kwa maana ya kitumwa wala kiudhalilishaji bali tumeichukua kama alama ya heshima kwa yule mtu aliyekuzidi umri.....ni kama zilivyo alama zingine za heshima kama ilivyo kupiga magoti kwa baadhi ya makabila pindi wasalimianapo hapa nchini....kwa hiyo sidhani kama ni ishara ya utumwa kwa wakati huu......
Mkuu jibu limejitosheleza kabisa.
 
Kwa majirani zetu wa Comorro, unapompa kitu chochote, mfano chakula mezani au zawadi mkononi yeye ndo atasema 'Shikamoo' akimaanisha 'Ahsante'...nawe utajibu 'Marhaba', ukimaanisha 'Ahsante' pia au kama wanavyosema wazungu 'You are welcome'...

Huo ndo mkanganyiko wa lugha...na labda ndo tunarudi kule kule kwenye maana yenyewe ya lugha kwamba lugha ni sauti za nasibu...tukimaanisha kwamba hizi ni sauti tu zinazoleta maana kwa watu waliozizoea na hazileti maana kwa watu hawajazoea kuzisikia/ au hazileti maana ile ile...sauti zilizozoeleka kwa jamii moja hazina maana kwa jamii nyingine au zina maana tofauti!
 
Ndio maana linatumika kumsalimia mtu aliyekuzidi umri, kwa ajili ya heshima uliyonayo kwake.......
tena awe amekuzidi kweli kweli hasa kama nawe ni mtu mzima, ndio maana huwezi kukuta mtu wa miaka 30 anamsalimia mtu wa miaka 45 shikamoo, yaani shikamoo ni reserved kwa mtu mwenye umri ambao anaweza kuwa mzazi wangu. nikiwa na miaka 30 shikamoo naitoa kwa aliye na umri wa at least miaka 50
 
Hebu tujaribu kufanya utafiti tena wa wazi hapa hapa JF kwa kila kabila jinsi wanavyosalimiana kilugha na maana yake kwa kiswahili halafu tuone ni makabila yapi yatakayokuwa na neno lenye maana ya "Shikamoo" katika kusalimiana kwao.

Tusipopata wingi wa makabila maana yake hilo neno tulitupilie mbali.
 
Back
Top Bottom