MwanaFalsafa1,
Kwa asili neno hilo kweli lilimaanisha hicho ulichosema. Lakini ujue lugha inazaliwa, inakua na kubadilika kadiri jamii inavyobadilika kufuatana na wakati. Kumbe katika lugha nyingi - si Kiswahili tu - misamiati imenyumbuka, kubadilika na hata kuwa na maana tofauti na ile ya mwanzo. Ndiyo maana kuna kitu kinaitwa etymology ya neno au msamiati.
Kwa hiyo neno "shikamoo" lenye asili ya Kiarabu lilimaanisha kujidunisha chini ya bwana. Lakini kadiri muda ulivopita, na hasa neno lilivoingia katika lugha ya Kiswahili, lilibadilika maana yake badala ya ile kitumwa likamaanisha Heshima ya mdogo kwa mkubwa wake. Kumbe likawa na maana chanya badala ya ile hasi.
Kumbe wanaokataa kupokea "shikamoo" hawajui tu. Waelimishwe wajue kwamba kwa leo tena kwa Kiswahili lina maana nzuri tu japo kiasili likuwa na maana hasi ya kudhalilisha.