Asili ya maneno 'Shikamoo' na 'Marahaba' ni utumwa, kwanini tunaendelea kuyatumia?

Usipate tabu na shkamoo zungumza na watu kwa lugha yako tu watakuelewa
 
Kwanza huna adabu je utaijua shikamoo? Maana baba yako mzazi huwezi kumwita baba unamwita mdingi kama teja vile.[emoji35] [emoji35] [emoji35]
 
Kwanza huna adabu je utaijua shikamoo? Maana baba yako mzazi huwezi kumwita baba unamwita mdingi kama teja vile.[emoji35] [emoji35] [emoji35]
No kupanga ni kuchagua mkuu,
Dingi, baba, mshua, mzee ni maneno yanayotumika sehemu tofauti kwa wakati tofauti. Kwangu shikamoo sio namna ya kuonesha adabu zaidi ya kuonesha aina ya utumwa mamboleo.
 
Wengine eti baada ya kuiona hii post hapa JF wanajifanya huwa hawasalimii na wakati wa kipindi cha nyuma hii salamu waliikuta na waliitumia..Ila baada ya kuona hii post ndio wanajifanya wamejanjaruka..

Sio mbaya lakini, maisha bila unafiki hayasongi mbele.
 
Siyo unafiki. Hawakujua. Sitaitumia tena. Sitapokea tena. Wataalamu wa kiswahili watafute msamiati mbadala. Haiwezekani! Msamiati huo mbadala uingizwe mashuleni haraka. Sisi siyo watumwa.
 
Siyo unafiki. Hawakujua. Sitaitumia tena. Sitapokea tena. Wataalamu wa kiswahili watafute msamiati mbadala. Haiwezekani! Msamiati huo mbadala uingizwe mashuleni haraka. Sisi siyo watumwa.
We unawaza hivyo mkuu (utumwa)..Ukimsalimia na kuendelea na shughuli yako utaumia mahali??
 
Siyo unafiki. Hawakujua. Sitaitumia tena. Sitapokea tena. Wataalamu wa kiswahili watafute msamiati mbadala. Haiwezekani! Msamiati huo mbadala uingizwe mashuleni haraka. Sisi siyo watumwa.
Kwa hiyo mnataka kutwambia shikamoo ni neno la Kiarabu?
 
Safi sana mkuu, wataalamu wa 'Linguistics' huita mabadiliko haya AMELIORATION.
 
Ni utamaduni wa kiafrika kuamukia aliyekuzidi umri tofauti na kuamukia mtu mlie na umri sawa ,kwa hiyo sio utumwa bali ni jadi,kila watu au kabila au taifa lina jadi yake,kuamukia mtu shikamoo sio utumwa
 
Kwani hasa unachokereka kwenye 'shikamoo' ni nini?

Unataka mtoto wako akwambie 'Mambo vipi baba'
au amwambie baba /mama vipi hujambo nadhani anayekereka hana wazazi au watu wazima kwao wa kuwaamukia shikamoo
 
kuna idadi kubwa ya watu wanatumia neno shikamoo kama sehemu ya kuonyesha heshima au salamu kwa mtu aliyekuzidi umri. Ila ni muhimu sana tukaelewa maana na historia ya na maneno “Shikamioo” na “Marahaba”. Kama ifahamikavyo kuwa kila jambo huwa na mwanzo na mwanzo huwa na sababu za kufanya hilo jambo kuibuka. Ni hivi kabla ya miaka ya 600 BK au BM, Wabantu walikuwa wameshafika Pwani ya Afrika mashariki. Na ukweli ni kwamba Wabantu walishapata kuishi hapo na hata wageni waliofika walikiri suala hilo. Na kwa kuwa Wabantu walipata kuishi hapo walikuwa na mitindo yao wa maisha na walikuwa wakiheshimiana. Kikubwa zaidi Wabantu walikuwa na salamu zao. Kwa mfano Wazaramo (historia yao itaandikwa) walikuwa na salamu yao kama ifuatavyo, aliyekuwa akiamkia alionyoosha mikono mbele na kusema “simbamwenee” na kisha anayeamkia huitikia “utwaaa”. Na kila mtu alikuwa akifurahia salamu hiyo, iliyokuwa nzuri kuitamka mdomoni. Lakini mambo yalibadilika pale walipokuja Waarabu na kuanzisha biashara ya utumwa. Na hapo tukapata makundi mawili yaani “mtumwa” na “bwana” na mtumwa alipaswa kumuamkia Bwana kwa neno la “Nashika Miuu” akiwa na maana ya “Nashika Miguu”. Na kila mtumwa alipaswa kujua na kutambua salamu hii. Na mtumwa alipaswa kutoa salamu hii hata mara 100 kwa siku moja. Lengo la salamu hii ilikuwa ni kutenganisha kati ya mtumwa na bwana wake. Kuanzia miaka ya 600-1700, salamu hii ilikuwa ikitumika maeneo ya Pwani tu. Na kuanzia miaka ya 1700 mwishoni na 1800 mwanzoni Waarabu walianza kuingia maeneo ya ndani ya Afrika mashariki. Na kila walipofika salamu hii waliitumia na baadhi ya machifu waliipenda sana salamu hii. Na kujikuta wakiwa na matamshi tofauti juu ya salamu hiyo. Na kwa wakati wote huo ilikuwa ni salamu ilikuwa ni "Nashika Miuu" na sio "Shikamoo" kama ilivyo sasa. Kutokana na watu tofauti kutumia salamu hii, wapo waliotamka "Shikamuu" kama neno moja. Na mpaka miaka ya 1930, kipindi ambacho Kiswahili kinafanyiwa usanifishaji ndipo tukapata neno "shikamoo." Na kuhusu neno "Marahaba", lina maana ya "asante". Na neno hili huitikiwa na Yule anaeamkiwa (Bwana) ambaye miguu yake imeshikwa na mtumwa. Na mpaka sasa salamu hii inatumiwa sana na Watanzania wengi licha ya kuwa na salamu zao za kikabila. Hii ndio historia fupi ya neno "Shikamoo" na "Marahaba". Shukrani za pakee ziwafikie "Historia ya Afrika" Je wewe mpendwa una maoni yapi juu ya salamu hii?, JE inafaa kuendelea kuenziwa au haifai?
 
aliyekuwa akiamkia alionyoosha mikono mbele na kusema “simbamwenee” na kisha anayeamkia huitikia “utwaaa”. Na kila mtu alikuwa akifurahia salamu hiyo, iliyokuwa nzuri kuitamka mdomoni. Lakini mambo yalibadilika pale,

Hiki kifungu kisome tena. Rekebisha .
 
Sasa ni sawa umetulipisha hela tuangalie movie kwenye kibanda umiza halafu umetokomea movie hujaweka. Maliza story bana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…