Kwanza inabidi ufahamu Mungu ni jina la cheo sio jina mahusus( Specific), kama vile mtu anavyoweza kusema Rais/Mfalme bila ku specify ni rahisi yupi/nani wa wapi, Rais ni cheo kama tu vile Mungu,mkuu wa mkoa,CEO na kila cheo kina sifa zake.
Katika lugha mbalimbali Mungu kama cheo ametajwa kwa majina mbalimbali mfano God (English) Allah (Arabic) Elohim (Hebrew) sio Yehova/Yahweh Deus na kadhalika
Lakini wayahudi/ wana Waisrael walikuwa na jina specific la Mungu wao ambalo ndio walikatazwa kulitaja bure kwa sababu ya utakatifu wake ambalo ni YHWH ( tetragrammaton) ambalo kwa sababu za kimatamshi westerns walilitohowa na kuliwekea irabu ndio likawa YAHWEH, ila Jina Yehova walilitumia wayahudi katika desturi zao za kumtaja Mungu kwa majina ya sifa badala ya jina lake halisi kwa sababu ya utakatifu wake ili kuepuka kulitamka bure na kijukuta wamevunja ile amri na sifa hizo ziliendana na kitu alichofanya au jinsi alivyo, mfano Yehova Rapha,Mungu mponyaji, Yehova Sabaoth, Mungu wa majeshi n.k.
Lakini kwa wagiriki walikuwa na desturi ya kuwa na miungu wengi tofauti na wayahudi na majina yao yalikuwa mengi pia, mfano Saturn,Venus,Uranus,Apollo etc.
Lakini kwa waarabu wao wamemtaja Mungu kama cheo (ALLAH) bila ku specify jina lake specific (sio la sifa)
Conclusion: Kwa hiyo usihadaike kwa mtu kusema tu Mungu wetu, je ni Mungu gani, unauhakika asilimia ngapi Mungu anayemmaanisha ndio huyo unaye muamini wewe, Ni swala lisilopingika ya kuwa Mungu wa kweli ni mmoja, lakini je ni Mungu yupi, anaitwa nani na wapi na anasifa zote za uungu, Kwa maana hata Lucifer anaitwa Mungu wa dunia hii, lakini je ni Mungu wa kweli?.
Na wengi wetu tumeingizwa katika ibada za miungu tusioijua kwa kigezo cha Mungu ni mmoja, Mungu ni wetu sote, Mungu ni yule yule, bila kujua Mungu ni cheo ambacho kinaweza kuwa na yeyote bila kujali kakidhi vigezo au laa, Ninyi nyote ni mashaidi kuna watu wanajiita marais, mara rais wa wasafi Rais wa manzese Rais wa watu je ni Marais kweli au wamejiita tu hivyo hivyo na kwa Mungu, Kuna Mungu wanajiita,(zumaridi) wengine wanaitwa na watu, hata mtaani kwetu yupo naye mjua anajiita Mungu na watu wanamuita hivyo, Lakini je ni kweli anavigezo
Note: Mungu wa kweli ni mmoja Muumba wa vyote vyenye kuonekana na visivyoonekana, wa milele, mweza yote,mjua yote, afanyaye kila jambo kwa shauri la mapenzi yake pekee, mwenye uwezo wa kuua na kuhuisha hata roho (je Mungu wako ana fit hapo?) Kama hatoshani na sifa hizo tafakari kisha chukua hatua.
Naomba kuwasilisha.