Asili ya neno washenzi ni watu wa bara...

Asili ya neno washenzi ni watu wa bara...

Kijakazi

JF-Expert Member
Joined
Jun 26, 2007
Posts
7,093
Reaction score
10,469
Neno Washenzi asili yake haswa lilikuwa likimaanisha watu wote wanaotoka Bara yaani katikati ya Ziwa Tanganyika na ukanda wa Pwani, kwa maana wakati huo walikuwa hawajastaarabika na hivyo Watu wa Pwani wanatuita Washenzi, na hasa wakati wa Misafara ya Utumwa kutoka Kongo Mashariki kupitia Tabora Mpaka Pwani huku tukiwa tumebeba Pembe za Ndovu na mijeredi juu (Ama Kweli Waarabu na Machotara wa Kiarabu walitusesa)!

Wakati huo tulikuwa hatujui kuandika wala kusoma na ndio maana tulikuwa tunaitwa "Washenzi" neno ambalo tunalitumia mpaka leo, nategemea utaenda kulalala ukiwa umejifunza kitu kidogo leo, badala tu ya kuwaza ngono...
 
Na asili ya neon usta-arab ni kuwa Mwarabu. Yaani waarabu ndio walioleta kile tunachoita sasa ustaarabu.
 
Mkuu wahenga wamenena baniani mbaya lakini kiatu chake dawa na usimtukane mkunga uzazi bado ungalipo ni kweli wazungu na waarabu wametutawala na sasa tuna kwenda huko huko kuwapigea magoti ya kuwomba sadaka au misaada nusu karne hii hata mitaro ya maji taka inatushinda kuzibua ni ufisadi tuu na kwa sasa hakuna tafauti na wakoloni weupe na sasa tunatawaliwa na mkoloni mweusi na ukifurukuta tuu mabobu ya machozi na mateke na virungu tena ni huyo ni weusi na hakuna tafauti ya weupe na mweusi
 
mwenye jina lake huyu hapa. shenzi_by_kati_kopa.jpg
 
Duh!!! kazi kwelikweli. Sijui kama tatizo ni umri wako mdogo au ni ka-ubongo kako kadogo kanakokusumbua. Anyway, shule ndogo hapa chini inaweza kukusaidia.
Neno shenzi ni neno la kiswahili ambalo asili yake ni kijerumani, neno la kijerumani ni "Scheiße". Hiyo herufi "ß" kwa kijerumani ni "double s". Wajerumani walikuwa wakiwatukana waafrika "Scheiße", na neno kijerumani linatamkwa "shaitz". Maana yake ni "shit" au "mavi" kwa kiswahili. Sasa waafrika wakaanza kuliiga neno "Scheiße" = "shit" na walikuwa wakitamka shenzi na ndiyo neno shenzi lilipoanza.
 
Jimmy santadiao

Umekakaata mziziwa fitna
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom