Asili ya uchawi na kuabudu Maiti, Jua na Mwezi ni Babeli siku chache baada ya gharika ya Nuhu

Kwa kiasi fulani umejenga hoja...
Lakini kama tuliridhiri kitu kimoja mbona IQ zetu zinatofautiana..mbona zisiwe sharp kama za wazungu
Acha kufikiri kitoto namna hiyo. IQ sio kipimo maridhawa juu ya uwezo wa mtu kufikiri au kung'amua mambo.

Ukitaka kujua ukweli wa haya mambo anagalia kipimo cha IQ kimejikita katika mambo gani ?
 
Hujatuambia baabel kulikuwa na uchawi wa aina gani.

Ukinijibu nitakupa ziada ya faida juu ya suala hili.
 
Nakubali kukubaliana kutokukubaliana kwenye maadhi ya mambo.
Paganism nimekupa maana uliyohitaji. Haizuhii kuwa na mitazamo kinzani na tofauti.

Kukataa mafuriko ya Nuhu inabidi ukatae kwa mtiiririko wa hoja pale juu kama ushahidi wa watu kuwa wamoja hapo bondeshi shinari. Pamoja na upinzani mwingi wa maandikp hayo ninayoyaaminni 100% bila shaka. Kuna ushahidi wa kijiolojia, Palentology, Archaeology unathibitisha uwepo wa Mafuriko kwa viwango vya bibilia. Hii haizuhii kupingwa kwa fact hizo.

3:Kuhusu Waebranania, na laana sijakuelewa weka vizuri maelezo.

6: Hapo unajichanganya na kupoteza consistency ya unayoyaamini. Maana ni wewe uliyewahi kuniambia JOSEPHUS na maandiko yake ni fablication sio uhalisia ukipinga uhalisa wa Uwepo wa Yesu, japo nilikupinga. Kuitumia source unayoikataa mahala pengine ili unullify biblical stories ni kujichanganya kunakostahili kutopewa umakini.

7:Sipingi mavumbuzi ya Egypt na mapyramid. ila nayo yanapewa changamoto nyingi na huo unaodhaniwa ukale wao kuliko Babilonia ya Kwenye Bibilia.
Kwanza kama moja niliyokupa huko nyuma. Pili hata dating zinazodhaniwa kuwa ni za zamani huko kwenye mmapyramid Kulingana na Mainstream historians, Lakni hata hizo pyramid kuna baadhi ya sources zilichakachuliwa na farao mmoja ambaye aliedit kila sanamu za kale na kuzipa majina yake.
Kuna watu weusi Wanalalamika wanasema baadhi ya makumbusho ya huko Sanamu zimechakachuliwa na kung'olewa mapua au kuyaharibu ili isionekane Wale jamaa walikuwa ni watu weusi. Hii na mikanganyiko mingine inanifanya niamini yale matukio ni halisi na ukweli ila dating rating ninaamini zaidi kwa mujibu wa matukio ya bibilia. Kama mtu mwingine akichukua story za bibilia akazibackdate ili zionekane ni za zamani kuliko matukio ya bibilia haiwezi kufanya bibilia kuwa ya Uongo.
 
Hujatuambia baabel kulikuwa na uchawi wa aina gani.

Ukinijibu nitakupa ziada ya faida juu ya suala hili.
Uchawi wote mkuu. Msingi wa mada kuwa hapo ndipo palipokuwa na asili ya uchawi wote kwa sababu baada ya gharika ya Nuhu watu wote walikusanyika hapo na wakatawanywa. Chochote cha kichawi kinachoonekana duniani mabara yotoe asili yake ni hapo.
Muunganiko wowote wa kidunia au NWO haiwezi kuwa na utoafuti ule wa pale bonde la shinari.
Ndio maana Mungu alipomuita Ibrahimu alimuagiza aachane na mambo yote ikiwemo system za Kihammurabi aliambiwa aachane nazo ili kupitia yeye Mungu ajiinulie taifa ambalo kupitia yeye Dunia nzima iliyotawanyika Ifahamishwe Juu ya Uwepo wa Mungu mwenye Fadhili, Upendo na Huruma, ambaye ataangamiza Uovu na wote watakao kataa kumfuata ili wanaomuamini Waokolewe awape zawadi ya Uzima wa Milele Kupitia Kumwamini Yesu.
Ila kabla ya Kufungwa kwa historia ya Ulimwengu. Kutakuwa na Muunganiko kama ule wa pale Babeli (Modern Babylon) na kumuasi Mungu. Ila safari hii Hawachafuliwi Lugha Bali ni Moto.



Karibu mkuu, nimeandika mengi ila unaweza kuendelea ulipolenga kuchangia mkubwa. Ila msingi wa Uchawi wote ni Worship of demons through Natural objects.
 
kuwa real israelite/yehova chosen lazima kutimiliza laana zote zinazotajwa kwenye deuteronomy 28:15-68 na leviticus 26:14-46
hapa jiulize kama wale waliopewa israel/palestina mwaka 1947 wanafulfill hizo laana zote?

kuhusu josephus sijawahi kusema story yake ni fake,niliandika kuwa wakatoliki kupitia eusebius waliongeza maneno kwenye maandiko yake karne ya 5

kuhusu mafuriko tafuta siku tudebate hilo sababu najua na nakumbuka ulichemka last time nimekumwagia evidence humu

hizo sehemu nyingine kuhusu egypt na babylon hebu tukubaliane kukubaliana but siku nikipata mda nitagusia
 
huo msingi wa kuwa real Israelite lazima utimize hizo laana na baraka unautolea wapi mkuu. nimesoma mwanzo, kutoka walawi na vitabu vyote sijaona kama laana na baraka za kumb 28 na walawi ndio ID ya Muebrania au muisrael. naona kama unapoint unataka kuilink na kilichotokea 1947 lkn utetezi wake haunielei kiasi nashindwa kuunga au kupinga concept yako.

Yap. Kuhusu Noah Floods, naona wadau wanajadili sana na wameshajadili sana, siku nikipata Muda wa kupitia vyanzo vyangu nitasoma na kupitia documentary zangu kadhaa nichokoze mada.
Kuhusu Josephus unaamini nini na hauaminini nini. Maana jinsi ulivyokmcrash that day sikutegemea kama ungemrefer tena kama chanzo chako cha kupingia bibilia. Binafsi huwa siamini kila anachokisema au alichokisema Josephus kuhusu Matukio ya kwenye bibilia kuanzia Mambo ya Yesu na mengine. Ila naamini maandishi yake ni moja ya vyanzo vinavyothibitisha uwepo wa matukio hayo.
 

point ni kwamba hajulikani nani ni myahudi,kuna kitu kinaitwa fulfillment of the prophecy/curse inayowaidentify hao wanaojiita the chosen ones,verses nilizokupa ni majanga watakayokutana nayo kama laana waliyopewa na mungu wao,yote lazima yatimie..swali nani kayatimiza sababu ethnic groups kibao zinaclaim kuwa israelites

josephus sijawahi kumponda as of my memory
 
Mimi ni mkatoliki.Hakuna mahala popote katika kanisa katoliki panaposema kuna Mungu Mama,eti virgin Mary.Kuna Mungu mmoja tu,ambae ndani yake kuna utatu mtkatifu.Yaani Baba,Mwana na Roho mtakatifu.Sio kila kitu mna google tu,kipuuzi na kuhusianisha matukio pasipo na facts za kutosha.Jikiteni kwenye mada.Maana kuchamba kwingi,mtajikuta mnajipaka kinyesi bureee.Viva Kanisa katoliki.
 
Mtoa mada nimekuelewa sana....ila naumia sana kuona hadi jukwaa hili kuna watu wanawahusudu wazungu kwa kuwapa superiority over us.. ...kila kitachoongelewa lazma ukute kuna jitu linamuusisha mzungu da......tubadilike mind zetu bas coz kuna shaid nyingi znazoonyesha we r not inferior over other races....sisi pia tumeshirik kwa asilimia kubwa kuijenga dunia ya sasa
 
uchawi upo.
Musa alipambana na kikosi cha wachawi cha wamisri wakiongozwa na wababe wawili Yane na Yambre.
Zamani wachawi walikuwa anatambulika hadharani na ni cheo ikulu kabisa unalipwa mafwedha.

Uchawi upo, na ukiufata utakunufaisha ila tambua ni temporary.
Lengo la mkuu wa wachawi shetani baada ya yote hayo ni kukutesa, kukujeruhi na atakuua kbisa.
Kuna mama anatuhuma za kupata mali kichawi, sasa hivi anahangaika kama mwehu, majini yanataka dau kubwa zaidi, au arudishe mali au mtoto wake wa kiume ambaye hakushirikishwa hizo mipango atolewe kafara. hadi sasa dogo ni graduate lkn yanamsumbua hadi mama yake aeleweke.

dawa ya Yote huwa ni Kumpa Yesu maisha. Sisi watu wa imani tumetest tunadhibitisha inalipa hata kama unapita katikati ya bonde la uvuli wa mauti.
 
Nauliza jamani hivi na ile kumbukumbu ya tarehe 14/10 ni Ibada ya wafu? Au ibada za wafu zinazozungumziwa zikoje?
 
Hata sasa tuna waganga.
 
Ongezea na wanaaoabudu siku haswa sabato. Kwao siku ni muhimu kuliko kuacha dhambi
 
Nijuavyo mimi tunaishi kizazi cha nyoka.... Kizazi kile cha Sodoma na Gomora
Kaka mkubwa with due respect I beg to differ with you.

Nijuavyo Mimi tupo kwenye kizazi cha Mungu.

Mungu anasema yeye ni Alpha na Omega Yani Mwanzo na mwisho na sasa tupo nyakati za " mwisho" na " mwisho " ndio Mungu .

Maana yake tupo kizazi cha Mungu
 
Huyo Yesu tunampata wapi?
Ikiwa Mapadre Ela za Sadaka, Wahisan/Wafadhili zinaliwa.
Fedha za kulea Mayatima zinaliwa, waumin wa makanisan nao wanakula Pombe, Zinaaa, wanapiga dilu za ela.
Na hivi sasa kumeibuka wanaojiita Manabii wa uwongk ambak wanapiga Ela halafu wanatembea.
Mmh! Mambo ya Iman Magum sana aisee...
 
UKICHUNGUZA KWA MAKINI UTAGUNDUA MAMBO MENGI HAPA DUNIANI NI BATILI.
SIKU ZA KUMUABUDU MUNGU, NYAKATI ZA SIKU ZIMEBADILISHWA KITU KINACHOFANANA MOJA KWA MOJA NA KILE KILICHOTABIRIWA KWENYE KITABU CHA DANIELI 7:25.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…