Asili ya watoto katika familia

Asili ya watoto katika familia

Ben Zen Tarot

JF-Expert Member
Joined
Dec 13, 2014
Posts
4,298
Reaction score
7,612
Inawezekana hujawahi kusoma popote maelezo mfano wa haya niloyaandika leo ila utaamini baada ya kunielewa na ukafanya utafiti.

Katika maisha ya mke na mume, au hata kama hamjaona ila mnaishi pamoja kama wanavyoishi mke na mume basi maisha hayo yataathiliwa pakubwa na aina ya mtoto mtakaeanza kumpata.

Kama mtaanza kuzaa mtoto wa kike basi mtakuwa na wepesi katika maisha yenu, mtaishi kwa upendo na hata biashara ama kazi mtakazozifanya zitakuwa na nuru na kuwaletea rizki ya kutosha.

Lakini pia mkianza na mtoto wa kiume basi ujue ''vyuma vitaumana''.
Mtapitia misukosuko mikubwa katika maisha yenu ya ndoa, magomvi kila kukicha, chuki zisizofahamika wapi chanzo chake, mara kodi hamna, mara kazi zimekwama, mara biashara hazitoki. Na usipokuwa makini mtajikuta mnazoea kushinda na njaa.

Kama utaamua kufanya uchunguzi utagundua huko mtaani wanawake wengi waloachiwa watoto ''masingle mama'' wengi wao ni wale wenye watoto wa kiume

''''Mwisho kabla sijawaeleza inavyosema katika utabiri naomba msiniulize kwanini nampenda zaidi mtoto wangu wa kwanza wa kiume kuliko wa kike''''.

Katika utabiri inasema unapotoka kwenda safari yoyote ile, na njiani ukakutana na mtoto wa kike usiyemfahamu yupo uchi. Basi ujue safari yako itakuwa njema yenye mafanikio. Lakini ukikutana na mtoto wa kiume usiyemfahamu yupo uchi. Basi tambua safari yako itakumbana na ugumu, kutofanikisha unachokifata ama hata ajali.
 
Wangu wa kwanza ni wa kiume na vyuma viliumana haswaaa ila wa pill nae wa kiume baada ya kupata huyo vyuma viliachia hadi tukasema huyu mtoto kaja na baraka,vipi hapo?
 
Wangu wa kwanza ni wa kiume na vyuma viliumana haswaaa ila wa pill nae wa kiume baada ya kupata huyo vyuma viliachia hadi tukasema huyu mtoto kaja na baraka,vipi hapo?
Uyo wa kwanza Kama ulivyosema ni wa kiume uyo ndo wa kujadili wa pili hata Kama ni wa kiume tena hana shida.
 
Back
Top Bottom