Asilimia 60 chali matokeo ya kidato cha nne

Kama ilivyotarajiwa, idadi kubwa ya wanafunzi waliofanya mtihani wa kidato channe mwaka jana wamefeli. Kati ya wanafunzi 367,750 waliofanya mtihani na ambaomatokeo yao hayakuwa na kuzuizi, wanafunzi 240,903 wamefeli kwa kupata daraja la0 (Tazama umbo Na.1). Hii ni sawa na asilimia 65.5 ya wanafunzi wote waliofanyamtihani wa kidato cha nne.
Umbo Na. 1: Idadi ya Wanafunzi kutokana na madaraja waliopata katika mtihani wakidato cha nne 2012​
Aidha wanafunzi 103,327 ‘wamefaulu' kwa kiwango cha daraja la nne, ambao nisawa na asilimia 28.1 (Tazama Umbo Na. 2). Kitaaluma, hawa nao wamefeli kwasababu kwa mfumo wa elimu wa Tanzania kwa sasa ngazi nyingi za elimu baada yakidato cha nne kinahitaji ufaulu wa kiwango cha chini cha daraja la tatu. Kwa hivyoukijumlisha idadi ya wanafunzi waliopata daraja la IV na 0 unapata wanafunzi1,641 6,453 15,426103,327240,903367,750-50,000100,000150,000200,000250,000300,000350,000400,000Daraja I Daraja II Daraja III Daraja IV Daraja 0 Jumla
2​
344,230 waliofeli kwa kiwango cha daraja la IV na 0; idadi hii ni sawa na asilimia 94(Tazama Umbo Na. 2)!! Kwa hiyo ni asimia sita (6) pekee ya wanafunzi waliopatamadaraja ya I, II na III na ambao kimsingi ndio wenye sifa za kujiunga na ngazimbalimbali za elimu baada ya kidato cha nne.​
Umbo Na. 2: Asilimia ya watahiniwa waliofaulu na kufeli katika madarajambalimbali​
Pamoja na kwamba watu wengi wameonekana kushtushwa na matokeo haya,akiwemo waziri mwenye dhamana ya elimu nchini, kwa wataalamu na wafuatiliajimakini wa mambo ya elimu matokeo haya hayashangazi. Tatizo moja la sisiwatanzania tumekuwa ni watu wa kusubiri matokeo na kutokujali sana mchakatounaoletekeza matokeo hayo. Sote tunajua kwamba hizi shule zinazoitwa shule zasekondari kimsingi nyingi zao hazina hata sifa ya shule nzuri ya shule ya msingi.Utafiti wa karibuni unaonyesha kwamba ni asilimia nne tu ya shule zote za sekondarinchini ndio zenye kukidhi vigezo vya kichini kabisa vya shule ya sekondari. Sotetunatambua kuwa walimu siku hizi hawana moyo wa kufundisha baada ya kupuuzwana kudharauliwa kwa muda mrefu. Walipojaribu kugoma wakatishwa na kusimangwana mwajiri wao. Wakarudi madarasani wakiwa wamenuna na wakatuwaaambiawaziwazi kwamba ‘mtaona'. Baadhi ya walimu wakadiriki hata kusema kwamba0.4% 1.8% 4.2%28.1%65.5%6.4%94.6%0.0%10.0%20.0%30.0%40.0%50.0%60.0%70.0%80.0%90.0%100.0%Daraja I Daraja II Daraja III Daraja IV Daraja 0 Daraja IIIIDaraja IV+0​
3​
watafundisha madudu na mwalimu mmojawapo akatoa mfano ubaoni kuwawatafundisha ‘7+7=77'. Badala ya kuungana na walimu kuibana serikali sotetukanywea, na mitihani ilipokaribia tukaenda madhahabuni kumuomba Mungu iliwatoto wetu wafaulu mitihani yao.Matokeo ya mwaka huu ni mabaya zaidi kutokea tangu nchi yetu ianze kuwa namfumo wa elimu wa kidato cha nne. Haijawahi kutokea hata mwaka mmojawanafunzi wa kidato cha nne wakafeli kwa kiwango hiki. Kiwango kibaya chakufaulu kilikuwa mwaka 2010 ambapo asilimia 50.4 tu ya wanafunzi waliofanyamtihani wa kidato cha nne ndio waliofaulu, wakati asilimia 49.6 walifeli (Tazamaumbo Na. 3). Ukichunguza kwa makini utaona kwamba kiwango cha kufaulu kilianzakushuka zaidi baada ya wanafunzi waliopitia mfumo wa shule za sekondari za katawalipoanza kumaliza, hasa kuanzia mwaka 2010, tulipoanza rasmi kutekeleza sera yawingi kwanza ubora baadaye.​
Umbo Na. 3: Kiwango cha ufaulu kidato cha nne 2001-2012​
Matokeo haya, kama yalivyokuwa ya miaka ya nyuma, yana athari nyingi, za mudamfupi na muda mrefu ujao. Kwa muda mrefu ujao, matokeo haya yanafifisha azima77.486.3 88.1 91.5 89.3 89.1 90.383.672.550.4 53.634.51020304050607080901002000 2002 2004 2006 2008 2010 2012​
%Waliofaulu​
4​
ya taifa ya kuwa na taifa la watu walioelimika ifikapo mwaka 2025 kamailivyoanishwa kwenye dira ya maendeleo ya taifa ya 2025. Kwa matokeo haya namengine ya miaka mitatu iliyopita, mfumo wetu wa elimu ya sekondari (na hatamsingi) unatutengenezea taifa la watu mbumbu ambao itakuwa vigumu kuwafanyawaamini sayansi, achalia mbali wao wenyewe kuibuka kuwa wana sayansi.Lakini pengine athari ambazo zitaanza kuonekana sasa hivi ni vyuo kuanza kukosawanafunzi wa kudahili. Kwa mfano, idadi ya wanafunzi wanaohitajika kujiunga namafunzo ya ualimu ngazi ya cheti na kidato cha tano kwa mwaka huu ni 57,983,lakini ni wanafunzi 23,520 tu waliomaiza mwaka jana ndio wenye sifa za kujiunga nataasisi hizi za elimu. Hivyo kutakuwa na upungufu wa wanafunzi zaidi ya asilimia 50wa kujiunga katika vyuo vya ualimu ngazi ya cheti na kidato cha tano ukizingatiakwamba sifa ya chini ya kujiunga na ngazi hizi za elimu ni kidato cha nne na ufauluwa kiwango cha daraja la tatu. Ni wanafunzi hawa waliomaliza mwaka janawanaotarajiwa kujiunga na vyuo vya elimu ya juu ifikapo mwaka 2015. Kwa upandewa vyuo vikuu pekee, kutakuwa na nafasi zizipungua 27068 mwaka 2015. Hata kamawanafunzi wote waliofaulu kwa kiwango cha daraja la I-III wataenda kidato cha tanona wote hawa wakafaulu mtihani wa kidato cha sita mwaka 2015, bado hawatawezakujaza nafasi za vyuo vikuu zitakazokuwepo mwaka 2015. (tazama maumbo Na. 4 na5).​
5​
Umbo Na. 4: Mahitaji ya Idadi ya Wanafunzi katika Ngazi Mbalimbali kati ya2013 na 2015​
17,09340,89012,36027,06897,411-20,00040,00060,00080,000100,000120,000Cheti chaUalimu 2013Kidato chaSita 2015Stashahda yaUalimu 2015Shahada 2015 Jumla​
6​
Umbo Na. 5: Mahitaji ya Wanafunzi vs Idadi ya Wenye Sifa za Kujiunga katikaNgazi Mbalimbali 2013-2015​
Hata hivyo, kwa maoni yangu, hatari kubwa inayotukabiri sio ubaya wa matokeohaya. Hatari kubwa ni kutokujali kwetu. Tena katika hili la elimu ndio kabisa litapitaupesi kwa sababu wengi tunaopiga hizi kelele watoto wetu ni miongoni mwa haoasilimia mbili waliopata madaraja ya I na II na ambao wanahudhuria mfumo tofautikabisa wa elimu! Tutapiga vikelele kidogo kisha tutanyamaza tukisubiri matokeomengine pengine mabaya zaidi mwakani tusipochukua hatua yeyote ya maana. Nahatua ya kwanza ya maana kabisa na ya muda mfupi ni kuwajali walimu. Katikabajeti ijayo serikali iwaongezee walimu mishahara angalau mara mbili ya wanaopatasasa hivi. Tukichukua hatua hii tutaanza kuanza matokeo tofauti. Nimesema marazote na narudia tena leo kwamba elimu bora ni walimu bora. Hatua za muda mrefu nikuuangalia upya mfumo wetu wa elimu. Hili litahitaji wataalamu wa elimu wawekevichwa vyao chini. Lakini hili haliwezekani kama serikali yetu itaendelea na serayake ya ‘wingi kwanza, ubora baadaye'!​
Mwandishi wa Makala haya ni Mhadhiri Mwandamizi katika Elimu na Saikolojiana Mkuu wa Kitivo cha Elimu katika Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es​
Salaam (DUCE).
 
GOLOKO,

Umenifurahisha sana mzee kwa hili pia inaonesha ni namna gani siasa zinaharibu elimu yetu
 
Mkuu vyuo vya mitaani mwaka huu vitapiga deal sana vile vya k.koo, magomeni, llala, buguruni n.k
 
ukosefu wa wawalimu kuwafundisha lugha. vitabu vingi sana vya elimu vipo katika lugha ya kiingereza. swala la kiswahili kutumika kufundishia shule za msingi likomeshwe maana lugha ya kiswahili haina vitabu vingi vya kusoma . jitihada za kutafsiri vitabu vingi kuwa vya kiswahili ziligonga mwamba baada ya serikali kukwepa ghalama ya copy right.

sasa ni vizuri serikali ikaamua moja kuwa lugha ya kiingereza itumike mara moja kufundishia mashuleni ili gharama ya kutafsiri vitabu vya sayansi na vingine ikwepeke.

60% ya wanafunzi kufeli kidato cha nne ni haibu ya kitaifa. hii imeonesha kuwa wanafunzi walikuwa hawajui wanaulizwa nini katika mtihani. halafu serikali lazima ipige marufuku tuition mara moja. walimu wengi sana wazuri wa masomo ya sayansi wamekimbilia Dar Es Salaam kufundisha tuitio. hivyo serikali ikipiga marufuku tuition lazima walimu watarudi mikoani kufundisha mashuleni/

Tafadhali serikali piga marufuku tuition mara moja! mikoani hamna walimu , walimu wote wamekimbilia mijini !
 
Mim Nadhan hizo shule zipo kwenye majimbo yao..hivyo wanazipa majina kama FAHARI...

Wala sio hivyo mkuu, kwa mfano hiyo J.M. Kikwete ipo kwenye jimbo la David Silinde
 
Sijaiona Yusuf Makamba, ile ndo huwa kiboko
 
kaka ukristo tena unatokea wapi kaka?
Ni kaugonjwa fulani ka Siri kalianzia Zanzibar kakaenea kwa kiasi kubwa Mbagala, Geita, matokeo ya mwaka jana ya somo fulani, na sasa kamebadili dalili zake kuwa hata kauli tu inaweza ikawa ni kaugonjwa hako.
 
Sababu
1. Serikali - hakuna mitaala, vifaa, ....usimamizi na ukaguzi wa shule
2. Walimu wachache, hawalipwi vizuri
3. wazazi hawafuatilii watoto
4. Wanafunzi hawasomi kwa bidii
 
kazi ipo mimi naona wanasiasa ndio wanaharibu shule zetu maana wanajipendekeza shule ziitwe majina yao hili nao ni bora kuyafuta haya majina ili tubaki kama hapo mwanzo.
 
Tatizo ni kuwapa nafasi ya kuwatangaza wanafunzi walipandika matusi na vitu visivyokubalika.
Miaka ya Kizazi cha Nyoka yaani hata kuacha karatasi ya majibu wazi wao wanaandika matatizo ya Nyumbani.
Mara mpenzi kaniacha,hatujala leo,
Kazi ni nzito ndg zangu
Muda unavyozidi kwenda hali ya matokeo inakuwa mbaya yaani kama walikwenda kutembea.
Tabu ni watoto wa shule za ada 20000/- ndiyo wengi na pia ndiyo walikuwa tegemeo ili waje wazikwamu familia zao.
 
dah mbuzi wa maskini hazai maana nilidhani majina ya wadogo zetu yatakuwa live kwenye Google(accessible)
 
Majina ya viongozi ni sifa kubwa sana ktk shule wivu wa kike tu unawasumbua
 

Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani (Necta), Dk Joyce Ndalichako

WIZARA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi inaweza kukumbwa na kashfa kubwa kutokana na matokeo mabaya ya kidato cha nne ya 2012 yaliyotangazwa juzi na Waziri wake, Dk Shukuru Kawambwa.
Kashfa hiyo inatokana na aina ya majibu yaliyoandikwa na baadhi ya watahiniwa katika mitihani hiyo, huku wengine wakikusanya vitabu vya majibu bila kujibu chochote, hali inayohusishwa na uhaba mkubwa wa walimu katika baadhi ya shule za sekondari nchini.

Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani (Necta), Dk Joyce Ndalichako alisema wasahihishaji walikutana na mambo ya ajabu yakiwamo matusi, michoro ya vitu visivyoeleweka, mashairi na nyimbo za muziki wa kizazi kipya (bongo fleva). “Mwaka jana tulikutana na ‘single’ yaani waliandika mashairi kwa uchache, lakini mwaka huu tumepata albamu nzima… ni vituko vitupu,
wengine wanaandika mapenzi, mwanafunzi anatumia ukurasa mzima kumlalamikia mpenzi wake.

Miongoni mwa yaliyoandikwa ni
mpenzi, umeniacha, natamani kunywa sumu, usiku silali nakuwaza wewe…”
alisema Dk Ndalichako.

Akizungumza katika mahojiano maalumu na gazeti hili ofisini kwake Dar es Salaam jana, Dk Ndalichako alisema wanafunzi wengine waliandika malalamiko dhidi ya wabunge na uendeshaji wa Bunge. “Unakuta mwanafunzi anaeleza anavyolishangaa Bunge… mtu anaandika…
nawashangaa wabunge, wamekaa kama wapo kijiweni, wabunge wamekosa ustaarabu, badala kujadili kero za wananchi waliowachagua, wanapokea timu zilizoshinda makombe… timu ikishinda Kombe la Kagame inapokelewa bungeni. Bunge limekuwa kama kijiwe, bungeni siyo ukumbi wa starehe kama mnataka kupokea timu hizo nendeni katika ofisi zao au viwanjani…” alisema. Alisema wanafunzi walioandika vitu visivyoeleweka walikuwa ni wengi na walichangia kwa kiasi kikubwa matokeo kuwa mabaya.
Dk Ndalichako alionyesha baadhi ya michoro hiyo ambayo inaonyesha vikaragosi ambavyo wanafunzi hao
waliviita Messi (Lionel, mchezaji wa Barcelona) na zombi
(ni picha za kutisha) ambazo huonyeshwa kwenye televisheni.


Sababu za kufeli
Dk Ndalichako alisema hawezi kuwa na jibu la moja kwa moja juu ya kwa nini matokeo ya mwaka huu yamekuwa mabaya, lakini akadokeza kuwa huenda yametokana na wanafunzi wengi kukosa maarifa.
Anasema mbali na waliojaza matusi na michoro, wanafunzi wengine waliofanya vibaya ni wale ambao hawakujaza chochote kwenye karatasi zao za majibu.
“Kuna baadhi ya shule unakuta darasa zima watoto hawajajibu somo fulani kwa mfano Biolojia, wanaingia tu na kuandika namba. Tuliamua kuwapigia simu walimu wao, majibu waliyokuwa wakitupa ni kuwa hawajawahi kuwa na walimu wa somo husika kwa hiyo watoto hawakuwa na cha kujaza.”

Dk Ndalichako alisema kwa ku mbukumbu zake, hakuna matokeo mabaya kama ilivyo kwa mwaka huu yaliyowahi kutokea.
“Tukiangalia tu kuanzia 2000, hakujawahi kutokea matokeo mabaya kama haya, kwa kweli hali haipendezi. Hata kabla ya kuyatangaza nilikuwa nayaangalia mara tatu tatu, sikuyapenda na inasikitisha kwa kweli,” alisema Dk Ndalichako.

Udanganyifu
Dk Ndalichako alisema hakukuwa na uvujaji wa mitihani wala udanganyifu wa ndani kwani vitendo hivyo vilidhibitiwa. Alisema baadhi ya wanafunzi wamefutiwa mitihani yao kutokana na majibu yao kukutwa na mfanano usiokuwa wa kawaida na kutoa mfano wa wanafunzi tisa katika shule ambayo hakuitaja kwamba majibu yao yalifanana katika somo la Kiswahili.
Alisema katika somo hilo, kulikuwa na swali lililotaka wanafunzi waandike shairi la kuonyesha umuhimu wa mwalimu na kwamba wanafunzi hao waliandika shairi moja la majigambo lililofanana kwa kila kitu. “Ni vigumu wanafunzi wote tisa kuwaza na kuandika kitu kimoja, shairi hilo lilifanana kila kitu na kwenye kiitikio wote walikosea kwa kuandika neno ‘hacheni’ niitwe mwalimu badala ya ‘acheni’ niitwe mwalimu,” alisema. Dk Ndalichako alisema udanganyifu mwingine ulionekana katika somo la hisabati, hali iliyothibitisha kuwapo kwa maandalizi ya pamoja ya majibu. Katika shule moja wanafunzi 90 walifanya kosa linalofanana.


Awasifu wasimamizi
Dk Ndalichako aliwamwagia sifa wasimamizi wa mitihani hiyo akisema walitimiza wajibu wao kikamilifu.
Alisema kutokana na umakini wa wasimamizi hao wanafunzi waliokuwa wameficha madaftari sehemu za siri walibainika.
“Kuna mmoja wa kike alikuwa ameficha daftari kwenye sehemu za siri, msimamizi akamwona anahangaika kweli hata kutembea hawezi, akatuma walinzi wa kike kumkagua akakutwa ameficha daftari sehemu za siri,”
alisema Ndalichako: “Kwa hiyo wasimamizi walifanya kazi ya ziada, kumfutia matokeo lazima kuwe na ushahidi wa kutosha. Mfano wanakuta mtu amejiandika kwenye kiganja cha mkono ama kanyagio la mguu, huwezi kukata na kuleta kama ushahidi lakini walitafuta mpigapicha wakapata picha wakaleta kama ushahidi.” Alisema mitihani yote iliyotungwa ilikuwa ndani ya mihutasari na ilitokana na mambo ambayo wanafunzi hao wangetakiwa wayasome ndani ya miaka minne.


CWT: Mgomo hauhusiki
Rais wa Chama cha Walimu Tanzania(CWT), Gratian Mukoba alisema matokeo hayo ni kitu ambacho kimekuwa kikikua kila siku na kwamba kufeli huko hakuhusiani na mgomo wa walimu wa mwaka jana.
“Matokeo haya ni ‘trend’ ya miaka mingi ila watu walikuwa hawajajipanga kuyapokea kama ya sasa. Ni tatizo lililojitokeza kidogo kidogo hadi lilipofikia sasa,”alisema Mukoba na kuongeza: “Suala hili lisipotafutiwa ufumbuzi, tutazalisha kizazi kitakachokuja kutulaumu kwa sababu hatukukiandalia mazingira mazuri.”

Mukoba alisema matokeo hayo yasihusishwe na mgogoro wa walimu kwani wakati mgomo ulipoanza tayari walimu walikuwa wameshafundisha zaidi ya nusu mwaka na wanafunzi wangeweza kufanya mtihani. “Matokeo mabaya hayahusiani na mgogoro, kwa sababu ulidumu kwa muda mfupi. Hata hivyo, wakati wa mgogoro ilikuwa nusu ya mwaka imeshafundishwa,” alisema Mukoba.



 
Haiwezekani 5% ya wanafunzi wote ndiyo wafaulu mtihani wa kidato cha nne. Yaani ni kama mwalimu una darasa la wanafunzi 100 kisha utoe mtihani, wafaulu watano, halafu unaona kawaida tu.

Nashauri serikali iwarudishe wote shuleni. Haiwezekani idadi yote hii wakawa ni wajinga.

Jana nimeona baadhi ya watu wanawatupia lawama wazazi pamoja na watoto kwa ujumla, ati wanapenda facebook. Sababu hii haina mashiko hata kidogo. Si kweli kwamba idadi kubwa namna hii ya watoto wanamiliki simu za kisasa au laptop zenye Internet.

Tatizo ni serikali kuboresha mazingira ya elimu, wao wanadhani waalimu wamesitisha mgomo, kumbe mgomo bado unaendelea.
 
Jana nilipata bahati ya kuonana na mmoja wa walimu walioteuliwa kusahihisha mitihani ya kidato cha 4, 2012. Swali langu kubwa nilitaka kujua jinsi gani walifanya kazi hiyo, hasa marking scheme. Moja ya jibu lililonishtua ni marking scheme kwa masomo ya lugha, Yaani English na Kiswahili. KUWA KEPENGELE (C) ambako hubeba marks 55% mpaka 60% huwa kuna maswali 3-5 lakini mojawapo huwa ni lazima kulifanya kwa lugha ya kigeni (compulsory ) niliambiwa kuwa katika kusahihisha kipengele hiki msahihishaji alipaswa kuangalia kama mtahiniwa amefanya swali la compulsory, kama mtahiniwa hakulifanya section yote huachwa ikiwa na maana section (C) yote mwanafunzi amepata zero. Hivyo hubaki kusahihishwa section A na B zeney jumla ya marks 40% tu.

Hoja ya msingi: Inabidi iundwe tume huru kujua tatizo katika matokeo ya kidato cha 4 kila mwaka, kuanzia usahihishaji mpaka kupanga matokeo. Watoto wa wakulima 60% hawana pa kwenda wakati tunasema elimu ni ufunguo wa maisha. Ni asilimia ngapi wamekatishwa tama na matokeo haya na ambao watajiingiza katika shughuri zisizo rasmi? Ukizungumza na baadhi ya vijana ambao tangu kidato cha kwanza wamekuwa wakifanya vizuri mpaka kwenye mitihani ya kanda ya majaribio wakifanya vizuri wamekataa kufeli kwa kiwango cha div zero ikiwa ni kupata alama F kwa masomo yote. Wamesema kufeli kwa div four inawezekana. Hivyo kuondoa utata huu tunaomba kujua zaidi katika baraza la mitihani.
 
Habari WANAJF

Hadi sasa kuna shule ya sekondari ya IKUYU MPWAPWA matokeo ya kidato cha pili bado hayajatoka. Ajabu ni kwamba matokeo ya form four yametangulia pia. Hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa na ofisa elimu(W) ya kumuwajibisha Mkuu wa shule. Watoto wanaendelea na masomo ya kidato cha tatu ingawa kwa mujibu wa shule za kata wengi wamefeli. Je serikali, wizara, ofisi za elimu hamlioni hili?
 
Umeoina jf ndio mahali sahihi pakuja kulialia
 
Warudi darasani kwa gharama zipi,
mishahara tu ya watumishi inaielemea nchi,
la maana wahusika wajivue madaraka wakianzia ngazi ya juu hadi ya chini.
 
Jamani ndugu zangu haya matokeo kweli ni fedheha kubwa sana kwa nchi nzima sio serikali pekee na wizara,
Msisahau mitandao ya simu usiku inapoweka bure kuperuzi facebook na social nyingine,hawa nao wamechangia sana kuwaweka busy watoto na mitandao yao,
Lakini hapa lawama nyingi na kubwa ni kwa wazazi,maana haya wanayafanya watoto wazazi wanayaona.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…