MAPUMA MIYOGA
JF-Expert Member
- Jan 30, 2013
- 3,792
- 2,365
Kama ilivyotarajiwa, idadi kubwa ya wanafunzi waliofanya mtihani wa kidato channe mwaka jana wamefeli. Kati ya wanafunzi 367,750 waliofanya mtihani na ambaomatokeo yao hayakuwa na kuzuizi, wanafunzi 240,903 wamefeli kwa kupata daraja la0 (Tazama umbo Na.1). Hii ni sawa na asilimia 65.5 ya wanafunzi wote waliofanyamtihani wa kidato cha nne.
Umbo Na. 1: Idadi ya Wanafunzi kutokana na madaraja waliopata katika mtihani wakidato cha nne 2012
Aidha wanafunzi 103,327 ‘wamefaulu' kwa kiwango cha daraja la nne, ambao nisawa na asilimia 28.1 (Tazama Umbo Na. 2). Kitaaluma, hawa nao wamefeli kwasababu kwa mfumo wa elimu wa Tanzania kwa sasa ngazi nyingi za elimu baada yakidato cha nne kinahitaji ufaulu wa kiwango cha chini cha daraja la tatu. Kwa hivyoukijumlisha idadi ya wanafunzi waliopata daraja la IV na 0 unapata wanafunzi1,641 6,453 15,426103,327240,903367,750-50,000100,000150,000200,000250,000300,000350,000400,000Daraja I Daraja II Daraja III Daraja IV Daraja 0 Jumla
2
344,230 waliofeli kwa kiwango cha daraja la IV na 0; idadi hii ni sawa na asilimia 94(Tazama Umbo Na. 2)!! Kwa hiyo ni asimia sita (6) pekee ya wanafunzi waliopatamadaraja ya I, II na III na ambao kimsingi ndio wenye sifa za kujiunga na ngazimbalimbali za elimu baada ya kidato cha nne.
Umbo Na. 2: Asilimia ya watahiniwa waliofaulu na kufeli katika madarajambalimbali
Pamoja na kwamba watu wengi wameonekana kushtushwa na matokeo haya,akiwemo waziri mwenye dhamana ya elimu nchini, kwa wataalamu na wafuatiliajimakini wa mambo ya elimu matokeo haya hayashangazi. Tatizo moja la sisiwatanzania tumekuwa ni watu wa kusubiri matokeo na kutokujali sana mchakatounaoletekeza matokeo hayo. Sote tunajua kwamba hizi shule zinazoitwa shule zasekondari kimsingi nyingi zao hazina hata sifa ya shule nzuri ya shule ya msingi.Utafiti wa karibuni unaonyesha kwamba ni asilimia nne tu ya shule zote za sekondarinchini ndio zenye kukidhi vigezo vya kichini kabisa vya shule ya sekondari. Sotetunatambua kuwa walimu siku hizi hawana moyo wa kufundisha baada ya kupuuzwana kudharauliwa kwa muda mrefu. Walipojaribu kugoma wakatishwa na kusimangwana mwajiri wao. Wakarudi madarasani wakiwa wamenuna na wakatuwaaambiawaziwazi kwamba ‘mtaona'. Baadhi ya walimu wakadiriki hata kusema kwamba0.4% 1.8% 4.2%28.1%65.5%6.4%94.6%0.0%10.0%20.0%30.0%40.0%50.0%60.0%70.0%80.0%90.0%100.0%Daraja I Daraja II Daraja III Daraja IV Daraja 0 Daraja IIIIDaraja IV+0
3
watafundisha madudu na mwalimu mmojawapo akatoa mfano ubaoni kuwawatafundisha ‘7+7=77'. Badala ya kuungana na walimu kuibana serikali sotetukanywea, na mitihani ilipokaribia tukaenda madhahabuni kumuomba Mungu iliwatoto wetu wafaulu mitihani yao.Matokeo ya mwaka huu ni mabaya zaidi kutokea tangu nchi yetu ianze kuwa namfumo wa elimu wa kidato cha nne. Haijawahi kutokea hata mwaka mmojawanafunzi wa kidato cha nne wakafeli kwa kiwango hiki. Kiwango kibaya chakufaulu kilikuwa mwaka 2010 ambapo asilimia 50.4 tu ya wanafunzi waliofanyamtihani wa kidato cha nne ndio waliofaulu, wakati asilimia 49.6 walifeli (Tazamaumbo Na. 3). Ukichunguza kwa makini utaona kwamba kiwango cha kufaulu kilianzakushuka zaidi baada ya wanafunzi waliopitia mfumo wa shule za sekondari za katawalipoanza kumaliza, hasa kuanzia mwaka 2010, tulipoanza rasmi kutekeleza sera yawingi kwanza ubora baadaye.
Umbo Na. 3: Kiwango cha ufaulu kidato cha nne 2001-2012
Matokeo haya, kama yalivyokuwa ya miaka ya nyuma, yana athari nyingi, za mudamfupi na muda mrefu ujao. Kwa muda mrefu ujao, matokeo haya yanafifisha azima77.486.3 88.1 91.5 89.3 89.1 90.383.672.550.4 53.634.51020304050607080901002000 2002 2004 2006 2008 2010 2012
%Waliofaulu
4
ya taifa ya kuwa na taifa la watu walioelimika ifikapo mwaka 2025 kamailivyoanishwa kwenye dira ya maendeleo ya taifa ya 2025. Kwa matokeo haya namengine ya miaka mitatu iliyopita, mfumo wetu wa elimu ya sekondari (na hatamsingi) unatutengenezea taifa la watu mbumbu ambao itakuwa vigumu kuwafanyawaamini sayansi, achalia mbali wao wenyewe kuibuka kuwa wana sayansi.Lakini pengine athari ambazo zitaanza kuonekana sasa hivi ni vyuo kuanza kukosawanafunzi wa kudahili. Kwa mfano, idadi ya wanafunzi wanaohitajika kujiunga namafunzo ya ualimu ngazi ya cheti na kidato cha tano kwa mwaka huu ni 57,983,lakini ni wanafunzi 23,520 tu waliomaiza mwaka jana ndio wenye sifa za kujiunga nataasisi hizi za elimu. Hivyo kutakuwa na upungufu wa wanafunzi zaidi ya asilimia 50wa kujiunga katika vyuo vya ualimu ngazi ya cheti na kidato cha tano ukizingatiakwamba sifa ya chini ya kujiunga na ngazi hizi za elimu ni kidato cha nne na ufauluwa kiwango cha daraja la tatu. Ni wanafunzi hawa waliomaliza mwaka janawanaotarajiwa kujiunga na vyuo vya elimu ya juu ifikapo mwaka 2015. Kwa upandewa vyuo vikuu pekee, kutakuwa na nafasi zizipungua 27068 mwaka 2015. Hata kamawanafunzi wote waliofaulu kwa kiwango cha daraja la I-III wataenda kidato cha tanona wote hawa wakafaulu mtihani wa kidato cha sita mwaka 2015, bado hawatawezakujaza nafasi za vyuo vikuu zitakazokuwepo mwaka 2015. (tazama maumbo Na. 4 na5).
5
Umbo Na. 4: Mahitaji ya Idadi ya Wanafunzi katika Ngazi Mbalimbali kati ya2013 na 2015
17,09340,89012,36027,06897,411-20,00040,00060,00080,000100,000120,000Cheti chaUalimu 2013Kidato chaSita 2015Stashahda yaUalimu 2015Shahada 2015 Jumla
6
Umbo Na. 5: Mahitaji ya Wanafunzi vs Idadi ya Wenye Sifa za Kujiunga katikaNgazi Mbalimbali 2013-2015
Hata hivyo, kwa maoni yangu, hatari kubwa inayotukabiri sio ubaya wa matokeohaya. Hatari kubwa ni kutokujali kwetu. Tena katika hili la elimu ndio kabisa litapitaupesi kwa sababu wengi tunaopiga hizi kelele watoto wetu ni miongoni mwa haoasilimia mbili waliopata madaraja ya I na II na ambao wanahudhuria mfumo tofautikabisa wa elimu! Tutapiga vikelele kidogo kisha tutanyamaza tukisubiri matokeomengine pengine mabaya zaidi mwakani tusipochukua hatua yeyote ya maana. Nahatua ya kwanza ya maana kabisa na ya muda mfupi ni kuwajali walimu. Katikabajeti ijayo serikali iwaongezee walimu mishahara angalau mara mbili ya wanaopatasasa hivi. Tukichukua hatua hii tutaanza kuanza matokeo tofauti. Nimesema marazote na narudia tena leo kwamba elimu bora ni walimu bora. Hatua za muda mrefu nikuuangalia upya mfumo wetu wa elimu. Hili litahitaji wataalamu wa elimu wawekevichwa vyao chini. Lakini hili haliwezekani kama serikali yetu itaendelea na serayake ya ‘wingi kwanza, ubora baadaye'!
Mwandishi wa Makala haya ni Mhadhiri Mwandamizi katika Elimu na Saikolojiana Mkuu wa Kitivo cha Elimu katika Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es
Salaam (DUCE).